Majadiliano:Mwanaanga

Latest comment: miaka 10 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Maneno yasiyo kawaida

Maneno yasiyo kawaida

hariri

Makala hii imehaririwa na mtumiaji:Nyabsino kwa kubadilisha lugha mara kadhaa. Nina wasiwasi kuhusu maneno mbalimbali aliyoleta. Naomba atoe ufafanuzi kuhusu maneno aliyobadilisha. Hii ni hasa maneno kama fasikebu, fasi, wafalki, mwanafasi, fataki.

Sipendi kukamtisha tamaa mwanawikipedia mpya kwa kurudisha mabadiliko haya moja kwa moja lakini nina wasiwasi kama maneno aliyetumia ni kweli lugha fasaha kwa mambo yanayojadiliwa. Kamusi zote ninazoona kama vile KKS, KMM na hasa KAST hazijui maneno aliyoleta kinyume zinaonyesha maneno aliyobadilisha sasa.

Naomba ataje vyanzo vyake. Halafu alirejea "taaluma ya Falaki". Naomba aangalie marejeo katika makala astronomia yanayotaja sababu ya kutotumia tena neno "falaki" kwa fani hii.

Kwa sasa nimelinda makala hii pamoja na chombo cha angani Kipala (majadiliano) 09:03, 4 Septemba 2014 (UTC)Reply

Umejaribu kuwasiliana nae? Hata mie hapa mgeni!--MwanaharakatiLonga 10:50, 4 Septemba 2014 (UTC)Reply
Mabadiliko ya mtumiaji:Nyabsino hayana msingi wala katika kamusi za Kiswahili wala katika matumizi kwenye intaneti. Nahisi alijaribu kutumia neno "falaki" (kwa maombi ya wataalamu wa fani hii tumeamua kutoendelea na neno hili kwa habari za kisayansi na badala yake tunatumia "astronomia" - tazama majadiliano:Astronomia. menginevyo nahisi ya kwamba alijaribu kuunda neno "fasi" kwa "space" (kutoka neno "nafasi"?). Ilhali hajarudi kujieleza narudisha mabadiliko yake. ~ Kipala (majadiliano)
Rudi kwenye ukurasa wa " Mwanaanga ".