Majadiliano:Ndubwi
Latest comment: miaka 15 iliyopita by Muddyb Blast Producer
Ndumbwi au Ndubwi? Hapa kwetu tunaita "Ndubwi" na si "Ndumbwi". Sijui hilo, labda utazame tena ili upate uhakika zaidi. Samahani sana--Mwanaharakati (Longa) 07:53, 11 Desemba 2008 (UTC)
- Bila samahani. Kwanza nafurahi ya kwamba wewe unajua neno. Jinsi nilivyo hapa nategemea kamusi nikiangalia mbili, tatu. Yaani nimekuta neno hili katika KAST pekee na nyingine hamna. KAST wakati mwingine ina maneno yasiyo kawaida kabisa hivyo nafurahi ya kwamba ni neno la kwaida. Kwa sasa naweka REDIRECT kwa sababu nina kamusi ile moja tu najua wanaweza kuwa na makosa (typo) au pia mara inawezekana kuna maumbo mawili ya neno. --Kipala (majadiliano) 12:14, 11 Desemba 2008 (UTC)
- Tutachekwa! Ni bora KUREDIRECT iwe katika "Ndumbwi" kuliko katika "Ndubwi". Yaani, makala kamili iwe "ndubwi". Nimeuliza kama watu wanne watano hivi kuhusiana na jina hili, wote wanasema "ndubwi". Sasa sijui mzee wangu, wewe unaonaje! Ukiona ni vyema kuiacha, sawa. Ukiona ni bora kuhamisha, yote kheri--Mwanaharakati (Longa) 12:37, 11 Desemba 2008 (UTC)
- Asante kwa ushauri nimehamisha. Sasa nisaidie kingine. Kile samaki anachotumia kwa kupumua. Kamusi inanipa "shavu la samaki". Lakini si samaki tu aliye na kitu kile - naona pia "shavu" peke yake haina maana ile. Je, "yavuyavu" ni sawa inaeleweka? --Kipala (majadiliano) 15:45, 11 Desemba 2008 (UTC)
- Mzee wangu, salam! Duh, kuhusu hilo sijui. Ila ninahisi hiyo uliyoisema kuwa "yavuyavu" ni nzuri zaidi. Kwani samaki hufanya yavuyavu! Ukiona haieleweki basi iwekee "yavuyavu" (shavu la samaki), hapo je?--Mwanaharakati (Longa) 05:35, 12 Desemba 2008 (UTC)