Majadiliano:Parare
Latest comment: miaka 9 iliyopita by Muddyb Blast Producer
Babu, wakati ningali mdogo (mimi na wenzangu tulikuwa na tabia ya kubaka "barare" na si "parare" - sijui lugha ya parare). Au labda imebadilika? Panzi je?--MwanaharakatiLonga 11:21, 21 Agosti 2015 (UTC)
- Jinsi ninavyoona parare haina kosa. Yaani wazee wa TUKI/ TATAKA kwenye chuo kikuu wameandika vile, na pia zamani ilikusanywa vile, nimeangalia Sacleux aliyekusanya maneno katika miaka ya 1920s na 30s. Kama mlizoea "barare" nahisi ni aina ya lahaja au matamshi ya kieneo; maana b na p ziko karibu sana. Kipala (majadiliano) 17:41, 21 Agosti 2015 (UTC)
- Muddyb, samahani. Nilichagua parare kwa sababu nafikiri hii ni muundo wa kawaida na barare ni tofauti ya lahaja. Kama Kipala anavyosema b na p ziko karibu sana kama vile r na l. Pengine ninaweka miundo miwili ya majina lakini siyo kila mara. Kwa sababu umeniandikia nitaingiza barare hapa. ChriKo (majadiliano) 18:03, 21 Agosti 2015 (UTC)
- Kipala, suala sio maandishi ya kitabu. Hicho unacho wewe, jamii hatuna. Ataipataje? Naunga ChriKo hoja yako ya kuunganisha kurasa zenye majina yote mawili (halafu katika mabano vilevile barare). Kama utaona inafaa..--MwanaharakatiLonga 06:16, 22 Agosti 2015 (UTC)