Majadiliano:Peace Corps
Latest comment: miaka 14 iliyopita by Kipala
Samahani jamani, Mimi sijakuta mtu anayosema "Kikosi cha Amani", nasikia "Peace Corps". Nadani watu wanafahamu hivyo, hata isiyokuwa Kiswahili kamili. Adwani ya ofici yake inasema Peace Corps tu. labda isiruke kutoka Peace Corps hadi Kikosi cha Amani? Thadk (majadiliano) 12:17, 3 Desemba 2010 (UTC)
- Sikia babu, a) wewe ndiye uliyeanisha makala hii? Kuna makosa mengi sana ya kisarufi na kitahajia. B) watu hawajakurupuka kuandika makala kwa jina la Kiswahili ilhali hawakuona kama kuna ulazima wa kuliita hivyo. C) Wikipedia hufuata majina maalumu iwapo kila Wikipedia itatumia jina moja na si badala. Kwa hili, naona kila Wikipedia imeandika kwa makala hii kwa muktadha wa lugha zao. D) ukiweza toa mifano hai na mwendelezo ikiwa ni pamoja na kuboresha makala iwe bora zaidi kisarufi. Karibu sana Mmarekani wewe!!! Wako,--MwanaharakatiLonga 12:45, 3 Desemba 2010 (UTC)
- Nakubali. Kikosi cha amani nilipoiona nilifikiri inahusu vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani. Tena "Corps" ni gimba kubwa kushinda kikosi. Jeshi la amani - la afadhali iwe Peace Corps. Je wenyewe wanajiitaje wakiandika Kiswahili? Au hawaandiki?Kipala (majadiliano) 13:42, 3 Desemba 2010 (UTC)
- Eh, tena hata mimi sijapa kusikia habari za hili shirika. Labda turejeshe jina la Peace Corps? Umetazama Mawikipedia mengine? Yote yametafsiri kwa mujibu wa maana za kikwao.--MwanaharakatiLonga 15:55, 3 Desemba 2010 (UTC)
- Ni kweli interwiki inaonyesha wengine wametafsiri na kutotumia "Peace Corps". Lakini wengi wao wana neno lilelile "corps" katika lugha zao kwa hiyo ni rahisi wanaacha "corps" (kwa umbo lao) jinsi ilivyo na kutafsiri "peace" pekee. Lakini kwa Kiswahili sijui neno kwa "corps" ambayo ni kitengo cha kijeshi kwa kawaida kikiunganisha "division" kadhaa (hata hii sijui kwa Kiswahili maana JWT hawana ngazi hii nisipokosei). Basi nahamisha. Kipala (majadiliano) 08:49, 4 Desemba 2010 (UTC)
- Eh, tena hata mimi sijapa kusikia habari za hili shirika. Labda turejeshe jina la Peace Corps? Umetazama Mawikipedia mengine? Yote yametafsiri kwa mujibu wa maana za kikwao.--MwanaharakatiLonga 15:55, 3 Desemba 2010 (UTC)
Haya, hongera kwa azimio lako. Labda aliyetafsiri alitumia mfano wa Carrier Corps kwa Kikosi cha Wachukuzi - au?--MwanaharakatiLonga 12:02, 4 Desemba 2010 (UTC)
- Labda alichukua huku. Si lazima. Kamusi zina maneno machache tu kwa vitengo vya kijeshi (tumshukuru Mungu ya kwamba Afrika ya Mashariki haikuwa na haja bado kuwa na jeshi kubwa sana hadi division-corps-armies) na hapa kikosi kinachukuliwa.Kipala (majadiliano) 15:01, 4 Desemba 2010 (UTC)