Majadiliano:Safari

Latest comment: miaka 14 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Kusudi la makala???

Kusudi la makala???

hariri

Inaonekana ni tafsiri ya makala ya Kiingereza "Safari" kwa Kiswahili. Hii haieleweki. Kwa Kiingereza makala inaeleza maana ya neno "safari" jinsi lilivyoingia katika lugha ya Kiingereza (na nyingine za Kizungu) kwa maana maalumu kama safari ya kitalii katika Afrika ya Mashariki kwa lengo la kutazama (au: kuvinda) wanyamapori. Hii haiwezi kutafsiriwa moja kwa moja kwa Kiswahili chini ya jina la "safari" maana kwa Kiswahili neno hili lina maana pana zaidi (kama Kiingereza "journey" au "travel"); hapa mchangiaji angepaswa kutafuta jina tofauti (kama "neno Safari katika lugha za Kizungu") na kuongeza maelezo. Bila hii ni heri kufuta makala. (pia Kiswahili chake ni kibaya "safari juu ya ardhi" kwa "overland" !!) --Kipala (majadiliano) 17:48, 17 Desemba 2009 (UTC)Reply

Kipala: Naunga mkono hoja hili. Makala nimejaribu kuitazama kwa kina na mimeona ya kwamba maelezo yake au namna ilivyopangwa ni vigumu kutambua nia ya dhati ya kuandika makala hii. Angefuata ya Kiingereza, ingeleta maana zaidi, lakini amenonekana kutia ujanja wake ndani yake na badala yak kapoteza maana. Isipobadilishwa mfano wake, basi ifutwe!--MwanaharakatiLonga 11:41, 21 Mei 2010 (UTC)Reply
Haya, nimebadilisha. --Kipala (majadiliano) 05:01, 22 Mei 2010 (UTC)Reply
Naona sasa mambo mazuri! Mengineyo: unadhani ya kwamba kuna ulazima wa kile kipengele cha "Tazama pia": makala ya safari katika Wikipedia ya Kiingereza? Viungo vya interwiki vimetaja tayari - kwa hiyo sidhani kama kuna ulazima wa kuwepo kwa kiungo kile. Wasalaam,--MwanaharakatiLonga 07:01, 22 Mei 2010 (UTC)Reply
Nimeiweka kwa sababu viungo vya interwiki vinaelekeza kwenda "travel" n.k., siyo kwa "safari" ya Kiingereza. --Kipala (majadiliano) 12:43, 22 Mei 2010 (UTC)Reply
Kumbe mtu mzima dawa! Sijalijua hili hata kidogo. Hongera kwa ubunifu wako!--MwanaharakatiLonga 14:03, 22 Mei 2010 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Safari ".