Majadiliano:Uingereza (maana)

Latest comment: miaka 15 iliyopita by Lloffiwr in topic Istilahi

Istilahi

hariri

Nimeongeza pendekezo lingine kwenye makala, linalotoka BAKITA. Labda Uingereza liwe jina la Ufalme wa Muungano, ambalo ni jina la kawaida linaloeleweka kirahisi. Halafu 'Inglandi' litumike kwa ajili ya sehemu ya 'England'.

Naona kwamba si mbaya kisiwa kiwe Kisiwa cha Briteni au Kisiwa cha Britania, badala ya Uingereza tena. Uzuri wa Wikipedia ni kwamba tunaweza kuingiza ramani au picha inayoeleza maana ya istilahi - tofauti na redio ambapo ni lazima kutumia neno lililoeleweka moja kwa moja. Je, tungeweza kutumia 'Briteni' kama ilivyo kwenye TUKI pamoja na BAKITA (tazameni Kamusi Project)? Halafu Britania ingeweza kuwa 'Brittany', sehemu ya Ufaransa? Je, mnajua kwamba jina la 'Brittany' ('Breizh' kwenye lugha ya kwao) kinafanana na jina la 'Britain' kwa sababu watu wa 'Brittany' ni wakimbizi waliowakimbilia 'Waingereza' (kabla hawajawa Waingereza!), Waingereza walipoingia 'Britain' na kuunda 'England', miaka mingi iliyopita? Maneno yana siasa nyingi!

'Visiwa vya Britania' ni istilahi yenye siasi kali tena. Watu wa Eire wanakasirika wanapoisikia istilahi hii. Kwenye Kiwelisi tunasema kitu kinachotafsiriwa 'Britania na Eire' (Kiwelisi - 'Prydain ac Iwerddon'. Tungeweza kuongeza 'Visiwa vya' mbele yake. Kwetu inaeleweka kwamba visiwa vyote vya karibu vinahusika ndani ya istilahi hii. Mnaonaje? Lloffiwr (majadiliano) 18:11, 7 Novemba 2009 (UTC)Reply

Kuhusu 'Brittany'. Tukitaka kuwaridhisha wenyeji wa pale wanaozungumza lugha yao ya asili (na pia kuwaridhisha wenyeji wa Uskoti, Welisi, Kernow, Ellan Vannin na Eire) tuuite 'Breizh', ila kitamsho chake hakieleweki kirahisi kwa sababu 'zh' hakuna kwenye Kiswahili. Nimeomba faili la sauti ya matamsho ya 'Breizh' iwekwe Wikimedia Commons. Lakini Wafaransa labda watakasirishwa kwa sababu za kihistoria na kisiasa. Kila kitu ni siasa tena! Lloffiwr (majadiliano) 18:47, 7 Novemba 2009 (UTC)Reply


Sikubali sehemu lakini tuwasikie wengine.
a) Inglandi (kwa nini si "ingilandi"??) ni neno lisoloeleweka.
b) "Ufalme wa Maungano" haueleweki kirahisi kwa lugha mbalimbali kwa mfano Kijerumani changu. Ila tu watu wakilisoma wanatafakari na kuielewa. Tena wanajifunza kitu juu ya nchi ambayo kwa kweli ni ufalme wa maungano. Sijui ukiandika juu ya katiba yake unataka kweli kuandika "Uingereza ni maungano wa Inglandi, Uskoti na...."
c) Briteni: sina neno kama wengine wanaona inafaa. Naona ni vema kuwa na neno inayosaidia kisiasa, kijiografia na pia kihistoria (Wabriteni wa kale walishindwa na Waroma ?)
d) Hakika Britania haifai kwa Bretagne. Heri tutumie Kifaransa chake kuliko "Britania" maana Waswahili wengi wanaotumia intaneti wamejifunza kiwango cha Kiingereza wanachukua "Britania" kama "Britain". Kwangu Breizh ni kielekezo.
e) Visiwa vya Britania - Kwa nini tusifuate makala ya en:British Isles ? Maana jina ni kimataifa (angalia interwiki yake!!) lakini kuna upinzani fulani unaostahili kutajwa.
Hoja! Tuombe wenyeji wengi wa Uswahilini kutafsiri sentensi zifuatazo:
1) The United Kingdom is a country in the British Isles comprising of England, Scotland, Wales and Northern Ieland.
2) It covers all of Great Britain and the northern part of Ireland.
--Kipala (majadiliano) 22:34, 7 Novemba 2009 (UTC)Reply
Mimi ningejaribu kutafsiri (lakini kwa shaka):

1) Ufalme wa Muungano ni nchi iliyopo katika visiwa vya Britania ikihusisha Uingereza, Uskoti, Wales na Eire ya Kaskazini. 2) Unaenea katika kisiwa chote cha Britania Kubwa na sehemu ya kaskazini ya Eire. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:31, 8 Novemba 2009 (UTC)Reply

Riccardo Riccioni: Umegonga Ikulu. Yaani, sawasawa kabisa. Haya, naona kizaizai kimeisha! Mimi binafsi naunga mkono maelezo ya Riccardo. Je, wengine?--  MwanaharakatiLonga 05:42, 9 Novemba 2009 (UTC)Reply
Nimetoa mawazo hapa kwa sababu Kipala ameomba nitoe mawazo yangu, kama Mwelisi. Lakini mimi si Mswahili, na ni dhahiri kwamba ni matumizi ya istilahi ya Waswahili yanayomiliki. Nilipofika Tanzania tofauti ya 'United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland' na 'England' haikueleweka. Yote yalikuwa 'Uingereza' tu. Kwa hiyo nimefurahi kwamba si mimi niliyependekeza kwamba 'Uingereza' ipate kushushwa cheo, isiwe 'United Kingdom' tena, bali iwe sehemu kadogo ya 'England' tu! :-)
Kuhusu 'Wales' naona kwamba 'the Kamusi project' inalitafsiri jina liwe Welisi. Nilipokuwa Tanzania 'Wales' haikueleweka. Lakini hiyo ni zamani. Kama 'Wales' inaeleweka sasa na linatumika, basi iwe 'Wales'. Lakini ikiwa bado jina la 'Wales' halieleweki vizuri hapo Afrika kuna ubaya gani wa kuacha jina la 'Welisi' hapo Wikipedia, hadi matumizi ya kisasa yatabadilika tena? Lloffiwr (majadiliano) 12:20, 21 Novemba 2009 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Uingereza (maana) ".