Majadiliano ya Wikipedia:Wakabidhi/archive 1

Hapo nikumbukumbu ya majadiliano kwenye ukurasa Majadiliano ya Wikipedia:Wakabidhi ya miaka 2009-2010

Flowerparty

hariri

Amepotea tangu Septemba 2009. Naona tumfute katika orodha ya wakabidhi. Kipala (majadiliano) 09:08, 28 Septemba 2010 (UTC)Reply

Vilevile Marcos ambaye hakuchangia sehemu kubwa kwa makala yenyewe tangu Juni 2008. Hata hivyo lazima kukumbuka kwamba hatuwezi kuwaondolea haki za mkabidhi. Tulikuwa na majadiliano hayo tayari hapa. Pole sana! --Baba Tabita (majadiliano) 14:50, 28 Septemba 2010 (UTC)Reply
Tena anaonekana kakimbia kabisa kwenye miradi ya wiki. Tazama michangoi ya mawiki-mengimengi utaona kwamba hajachangia mtandao wowote tangu Septemba 2009. Hueanda akawa anachangia mara moja kwa mwaka.--MwanaharakatiLonga 07:08, 29 Septemba 2010 (UTC)Reply
Kumbe inaonekana mambo yamerahisishwa kidogo? Linganisha http://meta.wikimedia.org/wiki/Steward_requests/Permissions#Removal_of_access hapa wanaondoa wakabidhi mfululizo. Labda tunahitaji kwanza kura rasmi. Nani anapeleka? Kipala (majadiliano) 13:41, 29 Septemba 2010 (UTC)Reply

Kura ya kuondoa wakabidhi waliopotea

hariri

Naomba tuangalie na kuacha maoni. Wikipedia:Wakabidhi#Kuondoa_wakabidhi_ambao_hawakushiriki_tena_tangu_miezi_kumi_au_zaidi Kipala (majadiliano) 14:25, 29 Septemba 2010 (UTC)Reply

Mzee wangu, nimejaribu kutazama mahali pa kupigia kura sijapaona. Nilivyoelewa mimi, unawataka wale wenye madaraka yao waje kukubali kutolewa usimamizi, ama sivyo? Basi hata simwoni wa kuja kusema kama anataka aondolewe usimamizi! Kwanza inataka utazame global contributions kwa mmoja-mmoja. Ukiona ya kwamba hakuna michango yao kwa muda mrefu, basi tupige kura sisi tu na kina Meta watakubali kwa msukumo wetu. Nimeona yakitokea kwenye Wikipedia ya Kislovakia - kulikuwa na wakabidhi wengi, halafu wakaanza kupururushwa kama maembe mtini. Unaonaje?--MwanaharakatiLonga 15:03, 29 Septemba 2010 (UTC)Reply
Pole, ukigonga hapa Wikipedia:Wakabidhi#Kuondoa_wakabidhi_ambao_hawakushiriki_tena_tangu_miezi_kumi_au_zaidi unatakiwa kufika kwenye ukurasa wa wikipedia:wakabidhi halafu unaona orodha ya mapendekezo. Si wale wenyewe wanaotakiwa kusema hapa (wangeweza, lakini, kama wapo) lakini wanawikipedia kwa jumla wanaweza kupiga kura hapa kwa kuongeza sahihi kwa "nakubali" au "sikubali" kwa kila jina. Naona kama watu 3 wamekubali bila upinzani inatosha. Baadaye mmoja wetu anapeleka matokeo huko Meta na wale wanachukua hatua. Kipala (majadiliano) 16:05, 29 Septemba 2010 (UTC)Reply

Kuhusu wakabidhdhi wa kale

hariri

Nimeorodhesha majina ya hao wasioonekana kabisa tena tangu muda mrefu. Ninajua ya kwamba wengine kati yao bado ni marafiki wa wikipedia; kwa mfano Marcos alijibu nilipomwuliza mwaka uliopita kuhusu historia ya wikipedia yetu ingawa hajashiriki menginevyo kwa muda mrefu zaidi. Wengine bado wako katika wikipedia nyingine kama en:wiki. Lakini naona mkabidhi anahitaji kupatikana nisipokosei hawako tena.

Natazama pia mbele kama tunataka kumwongeza mtu kama mkabidhi kuna ugumu ya kwamba katika wikipedia yetu ndogo kuna orodha ya wakabidhi wengi kidogo tayari. Kwa hiyo sioni faida kuendelea na hao wote. Hata kama watu wamesaidia sana wakati uliopita tunahitaji kutazama hali halisi jinsi ilivyo na kutazama mbele. Wote wamearifiwa katika kurasa zao nimeona pia ya kwamba Baba Tabita aliwatembela kwenye kurasa zao huko en:wiki au meta na kuwaarifu tena .

Kama ni swali la kusubiri - kwa muda gani? Wikipedia nyingine nilivyoona wanasema tu "6 months of inactivity" halafu wanafuta. Binafsi naona tusubiri mwaka 1 lakini si zaidi. Kipala (majadiliano) 15:54, 2 Oktoba 2010 (UTC)Reply

Sijaelewa bado. Tusubiri mwaka baada ya kuwachague waondolewe haki zao au namna gani? Wengi hawajafanya michango ya haja tangu kuondoka kwao. Hatutazami marekebisho ya sentensi mbili - halafu unakaa tena miezi nane unakuja kuhariri sentensi tatu. Basi tabu mtindo mmoja. Kama kukaa miaka tayari wameshakaa, ila ukitaka kupendekeza miaka mingine, basi twende!--MwanaharakatiLonga 05:48, 4 Oktoba 2010 (UTC)Reply
Ninavyoona mimi hao wote wanaotajwa mbele wamekaa kimya muda mrefu naona tusafishe orodha. Lakini wengine wetu wameandika "tusubiri kidogo" na hapa nauliza Je kwa muda gani? Katika matokeo jinsi yalivyo sasa naona ni Matt na Neno wanaofutwa lakini watatu wengine kuna wenzetu wasiokubali. Kwa hiyo sitapeleka majina yao Meta kwa ufutaji. Lakini swali linabaki palepale: je tuwaangalie upya baada ya muda gani wakikaa kimya? Kipala (majadiliano) 08:38, 4 Oktoba 2010 (UTC)Reply
Haya tungoje majibu kutoka kwao, lakini jana sio leo! Wao wapo mahali kwingine siku hizi!--MwanaharakatiLonga 09:10, 4 Oktoba 2010 (UTC)Reply


Rudi kwenye ukurasa kuu Majadiliano ya Wikipedia:Wakabidhi

Rudi kwenye ukurasa wa mradi " Wakabidhi/archive 1 ".