Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:52, 1 Novemba 2024 (UTC)Reply

ahsante sana Athunjenge (majadiliano) 12:53, 2 Novemba 2024 (UTC)Reply

Ushairi

hariri

7. NAMPENDA NISOMTAMANI.

Karatasi ya weusi , kalamu wino mweupe

Mezani mbao nyepesi , feni pembeni ni pepe

Mkono wandike kasi , niwe makini na kope

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Nilaumu wangu moyo , ambao wapenda penda

Au ndimi isemayo , maneno yenye kushinda

Au macho yaonayo , kutazama kusokonda

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Moyo umependa siye , yule nilomtamani

Ulimi utamkaye , kudhihirisha moyoni

Mikono imshakaye , nafsi ipo kinzanini

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Namtani mweusi , nimempenda mweupe

Awe mrefu kiasi , nimekwama kupekupe

Moyoni napata wasi , nabaki kupea kope

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Nilitamani nione , macho makubwa mazuri

Umbole linamba nane , na nguo zake hariri

Kiwe kiza nimuone , karibu kumkabiri

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Nimempenda kioja , bonge mwenye kilo zake

Umbo namba kumi moja , tani ndo chakula chake

Kubeba yataka haja , yafanya ufadhaike

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Mwembamba namtamani , vyovyote namweka mie

Kifo cha mende chumbani , dogi dogi nipo nae

Nimbebe ukutani , begani nimtumie

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Haya yote siyawezi , kwa huyu nilompenda

Kapasuka michirizi , mwili wote wa vidonda

Hamu yaja usingizi , kwake tendo linadunda

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Nilitamani mpole , mwenye sauti ya chini

Asininyoshe kidole , kosa seme samahani

Nikiguna awe mbele , niulizwe kulikoni

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Nimempenda chiriku , aongea pasi pimo

Asubuhi si usiku , michambo yake misemo

Nilete nyama ya kuku , kasoro itakuwemo

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Haiti mume silani , chakula jipakulie

Naitwa baba fulani , na nguo nijifulie

Housegirl. Chumbani , shuka anitandikie

Nampenda kwa yakini , yule nisomtamani.


Waweza penda yakini , kile usokitamani?

Maumivu ya moyoni , najiuluza kwanini ?

Simpendi yamkini , pendo nisolitamani

Nampenda kwa makini , yule nisomtamani.


Zainabu Njenge : mtunzi Athunjenge (majadiliano) 12:52, 2 Novemba 2024 (UTC)Reply

Ndugu, naona umejaribu kuboresha makala zetu, lakini bado hujajifunza vya kutosha. Kwanza angalia vizuri kazi za wenzako waliokutangulia. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:18, 7 Novemba 2024 (UTC)Reply