Karibu Bichuu katika Wikipedia ya Kiswahili! Tunafurahia kila mmoja akiingia na kuchangia kwake. Labda tu nianze na safu ya kuzungumzia Chakula mashuhuri chipsi kuku, hapa umeandika habari nzuri, lakini ulitakiwa utoe sifa na maelezo yahusianayo na chakula hicho kwa wakazi wa Tanzania ama Afrika ya Mashariki - na sio kuponda ama kuzungumzia kama upo gazetine la. Hii ni kamusi elezo, narudi tena, hii ni kamusi elezo! Maana halisi ni kwamba hapa tunaelezea jambo kwa undani, ikiwa twazungumzia chakula cha "Chips kuku" basi tutaelezea namna kilivyo na madhara yake na sio kuandika kama kero binafsi. Hivyo waombwa uirekebishe makala hiyo kisha uache ujumbe katika ukurasa wa majadiliano wa chips kuku, halafu mkabidhi atabadilisha mwundo wa jina hili la Chakula mshuhuri chips kwenda kwa "Chips kuku", unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 09:58, 28 Machi 2008 (UTC)Reply