Kai salaam na karibu sana kwenye wikipedia yetu!!! Naona utapata baadaye ukaribisho rasmi kwa sasa napenda kusema ni vema kuwa na Mswahili mwenyewe hapa kwetu (nategemea hutamwaga kwetu google-tanslate isiyonyoshwa!!). Naongeza ombi maalumu: pamoja na yote uliyopanga Je unaonaje ukitazama makala fupi ya mahali unapotoka na kutia chumvi kidogo afadhali hata mboga!) ? Unaweza kuingia katika Jamii:Mbegu za jiografia ya Tanzania uchague mkoa, wilaya halafu kata unapotoka halafu hariri kata ya nyumbani! --Kipala (majadiliano) 10:58, 29 Novemba 2009 (UTC)Reply