Makabelo Mosothoane
Makabelo Priscilla Mosothoane (amezaliwa Kanye, Botswana, 1952) ni mwanasiasa wa Lesotho ambaye alihudumu kama Waziri wa Elimu na Mafunzo kutoka mwaka 2012 hadi 2015, katika serikali ya Tom Thabane. Alikuwa muuguzi na mwalimu kabla ya kuingia katika siasa, na pia alikuwa raisi wa tawi la mitaa la Shirika la Msalaba Mwekundu.
Maisha
haririMosothoane alizaliwa katika familia ya Watswana. Lugha yake ya asili ilikuwa ni Kitswana. Mosothoane alihudhuria shule ya sekondari jijini Gaborone (mji mkuu wa Botswana), na baadaye alihitimu diploma ya uuguzi, akifanya mafunzo katika Hospitali ya Princess Marina ya Gaborone.
Alihamia Lesotho kusoma katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Lesotho, akimaliza masomo yake mwaka 1982 na kupata Shahada ya Sanaa katika Elimu. Akiendelea kukaa Lesotho baada ya kuhitimu, Mosothoane kwanza alifanya kazi kama mwalimu wa shule ya upili, akifundisha shule iliyopo Linare na Hlotse. Mwaka 1987, alianza kufanya kazi katika shule ya Kiingereza ya Wilaya ya Leribe, ambapo alikuwa mkuu wa shule mwaka 1991. Nje ya kazi yake katika elimu, Mosothoane alichaguliwa kuwa rais wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Lesotho mwaka 2003.[1]
Marejeo
hariri- ↑ Rosenberg, Scott; Weisfelder, Richard (2013). Historical Dictionary of Lesotho. Scarecrow Press. uk. 386. ISBN 978-0810879829.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Makabelo Mosothoane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |