Shirika la Msalaba Mwekundu


Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na lile la Hilali Nyekundu ni mashirika ya kibinadamu yenye wahudumu wa kujitolea takriban milioni 97 duniani kote [1] ambayo yalianzishwa ili kulinda masilahi ya afya ya binadamu, kuhakikisha heshima kwa hulka ya mwanadamu, na kuzuia na kupunguza mateso ya kibinadamu, bila ubaguzi wowote kwa misingi ya utaifa, rangi, jinsia, imani za kidini, daraja la kijamii au maoni ya kisiasa.

Muungano wa Kimataifa wa Mwalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu

The Red Cross and the Red Crescent emblems, the symbols from which the Movement derives its name.
Founded1863
LocationGeneva, Switzerland
Area servedWorldwide
FocusHumanitarian
MethodAid
Websitehttp://www.redcross.int/

Jina maarufu la Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu ni dhana tu, kwani hakuna shirika lolote lililosajiliwa rasmi kwa jina hilo. Katika hali halisi, shirika hili lina mashirika tofauti kadhaa ambayo kisheria hujitegemea mbali na lile lingine, lakini yameungana pamoja kupitia kanuni za kimsingi, madhumuni, ishara, masharti na vyombo vya serikali. Vipengee muhimu vya shirika hili ni:

  • Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) ilianzishwa mwaka wa 1919 na kwa sasa huratibu shughuli kati ya 186 za kitaifa za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu katika Shirikisho. Kimataifa, Shirikisho linaongoza na kupanga, kwa ushirikiano wa karibu wa Vyama vya wa kitaifa , misaada pamoja na kukabiliana na mahitaji ya dharura. Sekretarieti ya Shirikisho la Kimataifa ina makao yake mjini Geneva, Uswizi. Mwaka wa 1963, Shirikisho (likijulikana kama Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu) lilipatiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa pamoja na ICRC. [2]
  • Vyama vya kitaifa vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu zipo katika takriban kila nchi duniani. Kwa sasa, Vyama 186 vya kitaifa vinatambuliwa na ICRC na kujumuishwa kama wanachama kamili wa Shirikisho. Kila kipengee hufanya kazi katika nchi yake kwa mujibu wa kanuni za sheria ya kibinadamu ya kimataifa na amri ya Muungano wa kimataifa. Kwa mujibu wa hali na uwezo wake maalum, Vyama vya Kitaifa vinaweza kuchukua kazi za ziada za kibinadamu ambazo hazijatambulikana moja kwa moja katika sheria ya kibinadamu ya kimataifa au katika Mustakabali wa utenda kazi wa Muungano wa kimataifa. Katika nchi nyingi, zimejumuishwa kwa karibu sana na mfumo wa afya kwa kutoa Huduma ya utabibu kwa dharura.

Historia ya Muungano hariri

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu hariri

Solferino, Henry Dunant na kuanzilishwa kwa ICRC hariri

 
Henry Dunant, mwandishi wa "A Memory ya Solferino"
 
Original dokument Genève wa kwanza konventionen 1864

Hadi karne ya 19, kulikuwa hakuna mpangilio madhubuti wa mfumo wa uuguzi wa jeshi kwa majeruhi wala usalama au taasisi zilizolindwa kuwalazia na kutibu waliokuwa wamejeruhiwa katika vita. Mnamo Juni 1859, mfanyabiashara mswizi Henry Dunant alisafiri hadi Italia na kukutana na kaizari wa Ufaransa Napoleon wa III kwa nia ya kujadili matatizo katika kuendesha biashara nchini Algeria, ambayo kwa wakati huo inamilikiwa na Ufaransa. Alipowasili katika mji mdogo wa Solferino jioni ya 24 Juni, alishuhudia Vita vya Solferino, mojawapo ya mapigano katika ya Vita vya Austro-Sardinian. Kwa siku moja, takriban askari 40,000 pande zote mbili walikufa au kuachwa wamajeruhiwa uwanjani. Henry Dunant alishtushwa sana na matokeo ya baada ya vita, mateso ya askari waliojeruhiwa na uhaba wa matibabu na huduma za kimsingi. Alitupilia mbali madhumuni ya hapo awali ya safari yake na kwa siku kadhaa akajitola kusaidia katika matibabu na kuwauguza waliojeruhiwa. Alifanikiwa kupanga msaada wa dharura kwa kuwahamasisha wakaazi kutoa misaada bila ubaguzi. Aliporudi kwao mjini Geneva, aliamua kuandika kitabu kiitwacho A Memory of Solferino kilichochapishwa kwa pesa zake mwenyewe katika mwaka wa 1862. Alituma nakala za kitabu kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi kote Ulaya. Pamoja na kuandika maelezo barabara kuhusu tajriba yake ya Solferino ya mwaka wa 1859, alipendekeza kuanzishwa kwa mashirika ya kitaifa ya kutoa misaada kwa hiari ili kusaidia kuwauguza askari waliojeruhiwa katika vita. Aidha, alipendekeza kubuniwa kwa mikataba ya kimataifa kuhakikisha ulinzi wa madaktari wasioegemea upande wowote na hospitali katika maeneo ya vita kwa ajili ya askari waliojeruhiwa vitani.

Mnamo 9 Februari 1863 mjini Geneva, Henry Dunant alianzisha "Kamati ya Watano" (pamoja na wengine wanne kutoka familia zilizojulikana sana mjini Geneva) kama tume ya uchunguzi ya Geneva Society for Public Welfare. Lengo lao lilikuwa kuchunguza uwezekano mawazo ya Dunant na kupanga kongamanao la kimataifa kuhusu uwezekano wa utekelezaji wake. Wanachama wa kamati hii, mbali na Dunant mwenyewe, walikuwa Gustave Moynier, mwanasheria na mwenyekiti wa Geneva Society for Public Welfare; daktari Louis Appia, aliyekuwa na uzoefu wa kazi muhimu katika upasuaji;rafiki na mwenzi wake Appia Theodore Maunoir, kutoka Geneva Hygiene and Health Commission na Guillaume-Henri Dufour generali katika Jeshi la Uswizi aliyesifika sana. Siku nane baadaye, watu hao watano waliamua kubadili jina la kamati kuwa "Kamati ya Kimataifa ya Kutoa Misaada kwa waliojeruhiwa". Kutoka 26 Oktoba hadi 29 1863, kamati hiyo iliandaa kongamano la kimataifa mjini Geneva kupanga hatua za kuboresha huduma za matibabu wakati wa vita. Mkutano huo ulihudhuriwa na watu 36: wajumbe rasmi kumi na nane kutoka serikali za kitaifa, sita kutoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, wajumbe saba wa kigeni wasiokuwa rasmi , na wajumbe wale tano wa Kamati ya Kimataifa. Majimbo na Falme zilizowakilishwa na wajumbe rasmi zilikuwa:

Kati ya mapendekezo yaliyoandikwa katika maazimio ya mwisho wa mkutano, yaliyopitishwa tarehe 29 Oktoba 1863, yalikuwa:

  • Kuundwa kwa jamii za kitaifa kwa askari waliojeruhiwa;
  • Kutoegemea upande wowote Katika ulinzi wa askari waliojeruhiwa;
  • Utumizi wa misaada ya kujitolea katika vita;
  • Kupangwa kwa kongamano zaidi ili kutunga dhana hizi katika mikataba yenye uwezo wa kisheria za kimataifa
  • Kuanzishwa kwa ishara maalum kwa ulinzi wa matabibu, yaani ukanda mweupe mkono wenye msalaba mwekundu.
 
Memorial kukumbuka ya kwanza ya matumizi ya alama ya Msalaba Mwekundu katika migogoro ya silaha wakati wa vita ya Dybbøl (Danmark) mwaka 1864; pamoja kujengwa mwaka 1989 na Msalaba Mwekundu kitaifa jamii wa Denmark na Ujerumani.

Mwaka mmoja tu baadaye, serikali ya Uswizi ilizialika serikali za nchi zote za Ulaya, pamoja na zile za Marekani,Brazil, na Mexico, kuhudhuria kongamano rasmi la kidiplomasia. Nchi kumi na sita zilimtuma jumla ya wajumbe ishirini na sita kwenda Geneva. Mnamo 22 Agosti 1864, kongamano lilibuni Mkataba wa kwanza wa Geneva "ili kukidhi hali ya wanajeshi waliojeruhiwa katika vita". Wawakilishi wa majimbo na falme 12 walitia saini kanuni hiyo: Baden, Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Hesse, Italia, Uholanzi, Ureno, Prussia, Uswisi, Uhispania, na Württemberg. Mkataba huo ulijumuisha makala kumi, na kuanzisha kwa mara ya kwanza masharti yenye uzito wa kisheria kuhakikisha ulinzi kwa askari waliojeruhiwa, matabibu, na taasisi maalumu za kibinadamu bila kuegemea upande wowote wakati wa vita. Isitoshe, Mkataba huo ulibainisha masharti mawili maalum ambayo yangelitambulisha Shirika la Kitaifa la kutoa misaada kwa Kamati ya Kimataifa:

  • Shirika hilo la kitaifa lazima litambuliwe na serikali ya taifa kama shirika la kutoa misaada kulingana na Mkataba huo na
  • Serikali ya taifa hilo lazima iwe mwanachama wa Mkataba wa Geneva.

Punde tu baada ya kufanywa kwa Mkataba wa Geneva wa kwanza, Mashirika ya kitaifa yalianzishwa katika Ubelgiji, Denmark, Ufaransa, Oldenburg, Prussia, Uhispania, na Württemberg. Na pia mwaka wa 1864, Louis Appia na Charles van de Velde Kapteni katika Jeshi la Uholanzi, wakawa wajumbe wa kwanza wasioegemea upande wowote kufanaya kazi chini ya Msalaba Mwekundu katika vita. Miaka mitatu baadaye yaani 1867, Kongamano la Kimataifala Vyama vya Kitaifa vya Misaada vya Uuguzi kwa waliojeruhiwa vitani lilikutana kwa mara ya kwanza.

Mwaka huohuo, Henry Dunant alilazimishwa kujitangaza kuwa muflisi kutokana na kushindwa kwa biashara kunawiri nchini Algeria, hasa kwa sababu alikuwa amesahau kuangalia maslahi ya biashara yake wakati wa shughuli zake nyingi kwa manufaa ya Kamati ya Kimataifa. Utata ulioizunguka biashara ya Dunant na tetesi zilizofuata na kumharibia jina katika umma, pamoja na migogoro yake na Gustave Moynier, vilisababisha Dunant kutibuliwa kutoka nafasi yake kama mwanachama na katibu. Alishtakiwa kuwa Muflisi laghai na kibali cha kukamatwa kwake kikatolewa. Hivyo akalazimishwa kuondoka Geneva na kamwe hakuwahi karudi mji wake wa nyumbani. Katika miaka iliyofuata, Mashirika ya kitaifa yalianzishwa katika takriban kila nchi Ulaya. Mnamo 1876, kamati ilijipa jina la "Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu" (ICRC) ambalo ndilo jina lake rasmi hadi sasa. Miaka mitano baadaye, Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekanililianzishwa kwa juhudi za Clara Barton. Nchi zaidi zilitia saini Mkataba wa Geneva na kuanza kuuheshimu kwa uhalisi wakati wa vita. Katika muda mfupi tu, Shirika la Msalaba Mwekundu lilipata kasi kubwa kama Shirikisho la kuheshimika kimataifa, na Vyama vya kitaifa vikawa maarufu kupindukia kama namna ya kufanya kazi ya kujitolea.

Wakati Tuzo ya Amani ya Nobel ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1901, Kamati ya Nobel ya Norway iliamua kumtuza Henry Dunant pamoja na Frédéric Passy, mwanaharakati wa kimataifa. La umuhimu zaidi kuliko heshima ya tuzo yenyewe, pongezi rasmi kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilikarabati kuchelewa hadhi yake Henry Dunant na kutambua mchango wake muhimu katika uanzilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu. Dunant alikufa miaka tisa baadaye katika kituo kidogo cha kupumziia cha Heiden, Usizi. Miezi miwili tu awali, adui wake wa muda Gustave Moynier alikuwa pia amekufa, na kuacha alama katika historia ya Kamati kama rais aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi.

Mwaka wa 1906, Mkataba wa Geneva wa 1864 uliundwa upya kwa mara ya kwanza. Miaka moja baadaye, Mkataba wa Hague X, ulioratibishwa katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Amani mjini Hague, uliupanua Mkataba wa Geneva kujumuisha pia Vita vya majini. Muda mfupi kabla ya Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia kuanza mwaka wa 1914, na miaka 50 baada ya kuanzishwa kwa ICRC na kupitishwa kwa Mkataba wa Geneva, tayari kulikuwa na Vya vya kitaifa 45 duniani kote. Vuguvugu hili lilikuwa limeenea hadi nje ya Ulaya na Amerika ya Kaskazinihadi ya Amerika ya Kati na Kusini (Argentina, Brazil, Chile, Cuba, Mexico, Peru, El Salvador, Urugwai, Venezuela), Asia (Jamhuri ya China, Japan, Korea, Siam), na Afrika (Jamhuri ya Afrika Kusini).

ICRC wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia hariri

 
Kifaransa Postcard kuadhimisha jukumu la Msalaba Mwekundu manesi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, 1915

Vita vya kwanza vya Dunia vilipozuka, ICRC ilijipata imekabiliwa na changamoto kubwa hivi kwamba ingeweza kufaulu tu kama kwa ushirikiano wa karibu na Vyama vya kitaifa vya Msalaba Mwekundu. Wauguzi wa Msalaba Mwekundu kutoka duniani kote, ikiwemo Marekani na Japan, walikuja kusaidia kutoa huduma za matibabu kwa Jeshi za nchi za Ulaya zilizokuwa zikishiriki katika vita. Mnamo 15 Oktoba 1914, punde tu baada ya kuanza kwa vita, ICRC ilianzisha Uwakala wake wa Kimataifa kwa Wafungwa-wa-Vita (POW), ambao walikuwa 1,200 wengi wao wakiwa wafanyakazi wa kujitolea kabla ya mwisho wa 1914. Mwishoni mwa vita, Uwakala alikuwa umehamisha takriban barua na jumbe milioni 20, vifurushi milioni 1.9, na karibu faranga za Usizi milioni 18 katika michango ya fedha kwa Wafungwa-wa-Vita katikaa nchi zote husika. Aidha, kutokana na hatua za Uwakala huu, takriban wafungwa200,000 walibadilishanwa kati ya pande zilizokuwa zikizozana, kuachiliwa kutoka kifungoni na kurejea nyumbani kwao. Uwakala huo ulikusanya rekodi za Kadi za usajili karibu milioni 7 kati ya 1914 na 1923, kila kadi ikiwakilisha mfungwa binafsi au mtu aliyepotea. Usajili wa Kadi ulipelekea kutambulishwa kwa zaidi ya Wafungwa-wa-Vita milioni 2 na kuwawezesha kuwasiliana na familia zao. Daftari kamili imetolewa kwa mkopo kutoka kwa ICRC katika Makavazi ya Mashirika ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu mjini Geneva. Haki ya kupata Daftari hiyo bado inahifadhiwa madhubuti na ICRC.

Katika kipindi chote cha vita,ICRC ilifuatilia pande tanzu kuona kwamba vilifuata Mkataba wa Geneva wa 1907 na kutuma malalamishi kuhusu ukiukaji kwa nchi husika. Wakati silaha za kemikali zilitumika katika vita hii kwa mara ya kwanza katika historia, ICRC ilipinga vikali dhidi ya aina hii mpya ya mapambano. Hata bila kuwa na mamlaka kutoka Mikataba ya Geneva, ICRC ilijaribu kupunguza mateso ya raia wa kawaida. Katika maeneo ambayo yalikuwa yateuliwa rasmi kama "wilaya zilizomilikiwa",ICRC ingeweza kusaidia raia kwa msingi ya Mkataba wa Hague uitwao "Sheria na Kanuni za Vita vya Ardhi" ya 1907. Mkataba huu ulikuwa pia msingi wa kisheria kwa ICRC kufanya kazi za wafungwa wa vita. Mbali na kazi za Uwakala wa Kimataifa kwa Wafungwa-wa-Vita kama ilivyoelezwa hapo juu, hii ilijumuisha ukaguzi wa kambi za Wafungwa wa Vita. Jumla ya kambi 524 kote Ulaya zilitembelewa na wajumbe 41 kutoka ICRC mpaka mwisho wa vita.

Kati ya 1916 na 1918,ICRC ilichapisha Postkadi kadhaa zikionyesha mandhari kutoka kambi za Wafungwa wa Vita. Picha zilionyesha wafungwa katika shughuli za siku baada ya siku kama vile usambazaji wa barua kutoka nyumbani. Nia ya ICRC ilikuwa kuzipa familia za wafungwa hao matumaini na furaha pamoja na kupunguza wasiwasi wao kuhusu hatima ya wapendwa wao. Baada ya mwisho wa vita,ICRC ilipanga namna ya kurudi kwa takriban wafungwa 420,000 nchini kwao. Mnamo 1920, jukumu la upatanisho liliachiwa League of Nations lililoanzishwa na kumfanya mwanadiplomasia na mwanasayansi wa Norway Fridtjof Nansen kama "Balozi Mkuu kwa Upatanishi wa Wafungwa wa vita." Kazi yake ilipanuliwa baadaye ili kusaidia na kutunza wakimbizi wa vita wakati ofisi yake ikawa chini ya " Ubalozi mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi". Nansen, ambaye alivumbua Pasipoti ya Nansen kwa wakimbizi na kupewa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1922, aliwateua wajumbe wawili kutoka ICRC kama manaibu wake.

Mwaka mmoja kabla mwisho vita, ICRC ilipokea Tuzo ya Amani ya 1917 kazi yake maridhawa wakati wa vita. Ilikuwa tuzo ya kipekee ya Amani ya Nobel iliyopeanwa katika kipindi cha 1914-1918. Mwaka wa 1923, Kamati ilifanya mabadiliko katika sera yake kuhusu uteuzi wa wanachama wapya. Hadi wakati huo, wananchi kutoka mji wa Geneva tu ndio walioweza kujiunga na Kamati. Kizuizi hiki kililegezwa na kujumuisha raia wa Uswizi. Kama matokeo ya moja kwa moja ya Vita vya kwanza vya Dunia, itifaki moja ilionngezwa katika Mkataba wa Geneva na kupitishwa mwaka wa 1925 ambayo ilipiga marufuku matumizi ya gesi zenye sumu na silaha za baiolojia kama silaha. Miaka minne baadaye, Mkataba wa awali ulihaririwa upya na Mkataba wa pili wa Geneva "uliohusiana na ule wa Namna ya kuwashughulikia Wafungwa wa Vita" ilianzishwa. Matukio ya Vita vya kwanza vya Dunia pamoja na shughuli za ICRC vilichangia pakubwa kuongezeka kwa sifa na mamlaka ya Kamati katika jumuiya kimataifa na kupelekea kuongezeka kwa uhodari wake.

Mapema kama mwaka wa 1934, rasimu ya pendekezo la kuongezwa kwa mkataba mwingine kwa ajili ya ulinzi wa raia wakati wa vita ulipitishwa na Kongamano la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Kwa bahati mbaya, serikali nyingi hazikuwa makini kutekeleza Mkataba huo na hivyo basi kutoidhinishwa kabla ya mwanzo wa Vita vya pili vya Dunia.

ICRC na Vita vya Pili vya Dunia hariri

 
Red Msalaba Budskapet Łódź Polen 1940.

Misingi ya kisheria ya ICRC kufanaya kazi wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia ilikuwa ni Mikataba ya Geneva iliyohaririwa mwaka wa 1929. Shughuli za Kamati zilikuwa sawa na zile za wakati wa Vita Kuu vya kwanza: kuwatembelea na ufuatiliaji wa kambi za Wafungwa-wa-Vita, kuandaa misaada kwa raia, na ubadilishanaji wa habari kuhusu wafungwa na watu waliopotea. Mwishoni mwa vita, wajumbe 179 walipata kuwatembelea Wafugwa wa vita 12,750 kambini katika nchi 41. Uwakala wa Wafungwa-wa-Vita (Zentralauskunftsstelle für Kriegsgefangene) ulikuwa na wafanyakazi 3,000, na daftari ya kadi ya kufuatilia wafungwa ikiwa na rekodi milioni 45, na jumbe milioni 120 ziliweza kubadilishanwa kwa Uwakala huo. Mojawapo ya pingamizi kuu ilikuwa kwamba Shirika la Kijerumani la Msalaba Mwekundu, liloendeshwa na Nazi lilikataa kushirikiana na masharti ya Geneva pamoja na ukiukaji hadharani kama vile kufurushwa kwa Wayahudi kutoka Ujerumani na Kambi za mauaji ya halaiki yaliyoendeshwa na serikali ya Ujerumani. Aidha, washiriki wengine wawili katika mgogoro huo, Umoja wa Kisovyeti na Japan, walikuwa si wanachama wa Mikataba ya Geneva ya 1929 na haikuwa lazima kwa wao kufuata sheria za mikataba.

Wakati wa vita, ICRC alishindwa kupata kufanya mkataba na serikali ya Ujerumani kuhusu namna wafungwa walivyotunzwa katika kambi walimowekwa, na hatimaye kutelekezwa kutumia shinikizo ili kuepukana na kutofanyia kazi kwa Wafungwa wa vita. ICRC pia ilishindwa kuendeleza mwitikio wa habari za kuaminika kuhusu kambi za ukatili na mauaji ya Wayahudi wa Ulaya. Jambo hili ndilo linachukuliwa kama mwanguko mkubwa zaidi katika historia ya ICRC.[onesha uthibitisho] Baada ya Novemba 1943,ICRC ilipata ruhusa ya kutuma vifurushi kwa wafungwa waliojulikana kwa majina na mahali walimokuwa kambini. Kwa sababu sahihi za kupokelewa kwa vifurushi hivi mara nyingi zilifanywa na wafungwa wengine, ICRC iliweza kutambua na kusajili zaidi ya wafungwa 105,000 kambini na kupeleka takriban vifurushi milioni 1.1, hususan kambi za Dachau, Buchenwald, Ravensbrück, na Sachsenhausen.

Inajulikana kuwa wakati wa Vita vya pili vya Dunia, afisa wa Jeshi la Uswizi Maurice Rossel alitumwa Berlin kama mjumbe wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, hivyo basi alitembelea Auschwitz mwaka wa 1943 na Theresienstadt wa 1944. Claude Lanzmann alimhoji kuhusu aliyoyashuhudia mwaka wa 1979, na kutoa makala ya Visitor from the living. [3]

 
Marcel Junod, mjumbe wa ICRC, kuwatembelea POWs katika Ujerumani. (© Benoit Junod, Uswisi)

Mnamo 12 Machi 1945, rais wa ICRC Jacob Burckhardt alipokea ujumbe kutoka kwa Sajenti Mkuu Generali Ernst Kaltenbrunner kukubali matakwa ya ICRC's ya kuruhusu wajumbe wake kutembelea kambi za Wafungwa. Mkataba huu ulikuwa na sharti ya kwamba wajumbe hawa wangekaa katika kambi mpaka mwisho wa vita. Wajumbe kumi, wakiwemo Louis Haefliger (Camp Mauthausen) Paul Dunant (Camp Theresienstadt) na Victor Maurer (Camp Dachau) walikubali kazi hii na kutembelea kambi hizo. Louis Haefliger alizuia kutibuliwa kwa nguvu au kulipuliwa kwa kambi ya Mauthausen-Gusen kwa kuwaarifu askari wa Marekani, na hivyo kuokoa maisha ya karibu Wafungwa 60,000. Matendo yake yalikaripiwa na ICRC kwa sababu waliona kwamba alipita mipaka ya mamlaka yake mwenyewe na kuhatarisha msimamo wa ICRC wa kutoegemea upande wowote. Ni mwaka wa 1990 tu ambapo hadhi yake nzuri ilirejeshwa na rais wa ICRC Cornelio Sommaruga.

Mfano mwingine wa utu ulidhihirishwa na Friedrich Born (1903-1963), mjumbe wa ICRC huko Budapest ambaye aliyaokoa maisha ya pata Wayahudi 11,000 hadi 15,000 huko Hungaria. Marcel Junod (1904-1961), daktari kutoka Geneva, alikuwa mjumbe mwingine maarufu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Taarifa kuhusu aliyoyashuhudia, aliyekuwa mmoja wa wageni wa kwanza kutembelea Hiroshima baada ya bomu ya atomiki kurushwa, inaweza kupatikana katika kitabu Warrior Without Weapons.

Mwaka wa 1944, ICRC ilipokea Tuzo yake ya pili ya Amani ya Nobel. Kama ilivyokuwa katika Vita vya Kwanza vya Dunia, ni ICRC tu ndiyo ilipokea tuzo ya Amani ya Nobel wakati wa kipindi hicho cha vita, kati ya 1939 na 1945. Mwishoni mwa vita, ICRC ilifanya kazi na Shirika la Msalaba Mwekundu kuandaa misaada kwa nchi zilizoathirika zaidi. Mwaka wa 1948, Kamati ya ICRC ilichapisha ripoti marekebisho ikieleza shughuli zake wakati wa vita kuanzia 1 Septemba 1939 hadi 30 Juni 1947. Tangu Januari 1996, ICRC nyaraka za kipindi hiki zimekuwa wazi kwa umma na kwa kufanyiwa utafiti wa kitaaluma.

ICRC baada ya Vita vya Pili vya Dunia hariri

 
Makao Makuu ya ICRC Geneva

Mnamo 12 Agosti 1949, uhariri zaidi ulifanywa kwa Mikataba miwili ya Geneva na kuratibiwa. Mkataba mwingine "kwa Manufaa ya hali ya Wanajeshi wanamaji waliojeruhiwa, kuwa wagonjwa au Waliopata dhoruba Baharini", inayojulikana kwa sasa kama Mkataba wa Pili wa Geneva, uliletwa chini ya mwamvuli wa Mkataba wa Geneva kama mwandamizi wa Mkataba wa Hauge X wa 1907. Mkataba wa 1929 wa Geneva "uliohusiana na Namna ya kuwatunza Wafungwa wa Vita" waweza kuwa Mkataba wa Geneva wa pili kutoka mtizamo wa kihistoria (kwa sababu uliandaliwa Geneva), lakini baada ya 1949 ulipata kuitwa Mkataba wa tatu kwa sababu ulikuja baada ya ule wa Hague. Kama jibu kwa masuala yaliyojiri baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Mkataba wa Nne wa Geneva mkataba mpya "kwa Ulinzi wa Raia wakati wa Vita", ulianzishwa. Pia, itifaki za ziada za 8 Juni 1977 zilinuiwa kufanya mikataba kutumika katika migogoro ya ndani kama vile vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hii leo, mikataba hiyo minne na itifaki zilizongezwa zina makala zaidi ya 600, upanuzi wa ajabu wakati ikilinganishwa na makala 10 tu katika mkataba wa kwanza wa 1864.

Katika maadhimisho ya miaka mia moja mwaka wa 1963, ICRC, pamoja na Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu, ilipokea Tuzo yake ya tatu ya Amani ya Nobel. Tangu 1993, raia wasio wa Uswizi wameruhusiwa kuwa wajumbe wa Kamati ya ugenini, jambo ambalo hapo awali lilikuwa hifadhi ya raia wa Uswizi. Hakika, tangu wakati huo, mgawo wa wafanyakazi wasio na uraia wa Uswizi umeongezeka kwa karibu asilimia 35.

Mnamo 16 Oktoba 1990, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kuiteu ICRC kama Mwangalizi wa vikao vya mikutano yake na mikutano ya kamati ndogo, mara yake ya kwanza kuwahi kulifanya shirika la kibinafsi kuwa Mwangalizi. Azimio hilo lilipendekezwa na nchi wanachama 138 na lililetwa mbele ya mkutano na balozi wa Kiitaliano, Vieri Traxler, kama kumbukumbu la asili ya shirika hilo katika Mapigano ya Solferino. Mkataba na serikali ya Uswizi uliotiwa saini 19 Machi 1993, aliimarisha sera ya muda ya uhuru kamili wa Kamati kutokana na kuingiliwa kwa vyovyote na Uswizi. Mkataba huo hulinda kikamilifu ICRC pamoja na mali yake yote pamoja na makao yake makuu nchini Uswizi, Hifadhi ya Nyaraka zake, kuwapa wanachama na wafanyakazi kinga kisheria, kuikinga ICRC kutotozwa ushuru na ada, kutoa dhamana ya ulinzi na kutotozwa ushuru kwa bidhaa, huduma, na fedha wakati wa usafirishaji, kuiwezesha ICRC kupata mawasiliano salama kwa kiwango sawa kama ubalozi za kigeni, na Kurahishisha kusafiri kwa Kamati ndani na nje ya Uswizi.

Wakati wa mwisho wa Vita Baridi, kazi ya ICRC ilikuwa hatari zaidi. Katika miaka ya tisini, wajumbe zaidi walipoteza maisha yao kuliko wakati mwingine wowote katika historia yake, hasa wakati wa kufanya kazi katika vita na migogoro ya ndani. Visa hivi mara nyingi vilidhihirisha kutoheshimiwa kwa kanuni na ishara za ulinzi za Mikataba ya Geneva. Miongoni mwa wajumbe waliouawa walikuwa:

  • Frédéric Maurice. Alikufa 19 Mei 1992 akiwa na umri wa miaka 39 siku moja tu baada ya gari la Msalaba Mwekundu alilokuwa akiandamana nalo liliposhambuliwa katika mji wa Sarayevo huko Bosnia .
  • Fernanda Calado (Uhispania) Ingeborg Foss (Norway) Nancy Malloy (Kanada) Gunnhild Myklebust (Norway) Sheryl Thyer na Hans Elkerbout (Uholanzi). Waliuawa kwa kupigwa risasi kwa karibu wakiwa wamelala asubuhi na mapema mnamo 17 Desemba 1996 katika hospitali ya ICRC katika mji wa Nowije Atagi nchini Chechnya karibu na Grozny. Wauaji wao hawajawahi kushikwa na kulikuwa hakuna sababu dhahiri ya kufanya mauaji hayo.
  • Rita Fox (Uswisi) Véronique saro (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zamani Zaire) Julio Delgado (Kolombia) Unen Ufoirworth (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) Aduwe Boboli (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) na Jean Molokabonge (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo). Mnamo 26 Aprili 2001, wakiwa na magari mawili kwenye misheni ya kupeleka misaada kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walishambuliwa kwa kufyatuliwa risasi kutoka kwa watu wasiojulikana.
  • Ricardo Munguia (El Salvador). Alikuwa anafanya kazi kama mhandisi maji nchini Afghanistan na kusafiri na wenzake tarehe 27 Machi 2003 wakati gari zao zilisimamishwa na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha. Aliuawa kinyama kwa kupigwa risasi kwa karibu lakini wenzake waliruhusiwa kutoroka. Alifariki akiwa na umri wa miaka 39.
  • Vatche Arslanian (Kanada). Tangu mwaka wa 2001, alifanya kazi kama mratibu wa vifaa kwa ajili ya utume wa ICRC nchini Iraq. Alikufa wakati alipokuwa akisafiri kupitia Baghdad pamoja na wanachama wa Shirika la Hilali Nyekundu la Iraq. Mnamo 8 Aprili 2003 gari lao lilijipata katikati ya mapigano makali mjini.
  • Nadisha Yasassri Ranmuthu (Sri Lanka). Aliuawa na washambuliaji wasiojulikana tarehe 22 Julai 2003 wakati gari lake lilipofyatuliwa risasi karibu na mji wa Hilla kusini mwa Baghdad.

Shirikisho la Vyama vya Kimataifa vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu hariri

Historia hariri

 
Henry Davison, Founding baba wa Ligi ya Msalaba Mwekundu jamii. (Picha kutoka: www.redcross.int)

Mwaka wa 1919, wawakilishi kutoka Vyama vya Kitaifa vya Msalaba Mwekundu za Uingereza, Ufaransa, Italia, Japan, na Marekani walikutana mjini Paris kuanzilisha "Shirikisho la Vyama vya Msalaba Mwekundu". Dhana ya awali ilikuwa ya Henry Davison, aliyekuwa rais wa Shirika la Marekani la Msalaba Mwekundu. Hatua hii, ikiongozwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani, ilipanua shughuli za kimataifa za Msalaba Mwekundu zaidi ya kazi halisi ya ICRC na kujumuisha utoaji wa misaada ya dharura kukabiliana na hali ambazo hazikuwa zimeesababishwa na vita (kama vile majanga yaliyosababishwa na wanadamu pamoja na yale ya kikawaida). Shirika hilo tayari lilikuwa na tajriba kubwa katiaka kutoa misaada wakati wa majanga tangu kuundwa kwake.

Kuanzishwa kwa Shirikisho, kama nyongeza ya shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu sambamba na ICRC, hakukuwa bila ya utata kwa sababu kadhaa. ICRC ilikuwa kwa kiasi fulani na wasiwasi juu ya uwezekano wa kuelekezana kati ya mashirika hayo mawili. Kuanzilishwa kwa Shirikisho hilo kulionekana kama jaribio la kudhoofisha nafasi ya uongozi wa ICRC vuguvugu zima na hatimaye kuhamisha nyingi ya majukumu yake wa kazi kwa taasisi ya kimataifa. Isitoshe, wanachama wote waanzilishi wa Shirikisho hilo walikuwa kutoka Vyama vya kitaifa vya nchi za Entente au kutoka washirika wa Entente. Masharti ya awali ya Shirikisho kuanzia Mei 1919 yalikuwa na kanuni zaidi ambazo zilivipa Vyama tano anzilishi hadhi ya kipekee na, kutokana na juhudi za Henry P. Davison, haki ya kudumu ya kuvizuia Vyama vya Msalaba Mwekundu vya kitaifa kutoka nchi zenye Mamlaka ya Juu, yaani Ujerumani, Austria, Hungary, Bulgaria na Uturuki , na pia Chama cha Kitaifa cha Msalaba Mwekundu cha Urusi. Sheria hizi zilikuwa ni kinyume na kanuni za Msalaba Mwekundu za ulimwengu na usawa kati ya Vyama vyote vya kitaifa, hali ambayo ilizidisha matatizo ya ICRC.

Msaada wa kwanza kuwahi kupangwa na Shirika hilo ulikuwa ni kutoa misaada kwa waathirika wa njaa na baadaye mkurupuko wa ugonjwa wa typhus nchini Poland. Miaka mitano tu baada yake kuundwa, Shirika hili tayari lilikuwa limetoa maombi 47 ya michango kwa ajili ya misioni katika mataifa 34, jambo lililo ashiria haja ya kuwa na aina hii ya kazi ya Msalaba Mwekundu. Jumla ya pesa zililotolewa kutokana na maombi haya zilifika faranga million 685 za Uswizi, ambazo zilitumika kuleta vifaa vya dharura kwa waathiriwa wa njaa nchini Urusi, Ujerumani, na [[Albania; mitetemeko ya ardhi nchini Chile, Uajemi, Japan, Colombia, Ecuador, Costa Rica, na Uturuki ; na ongezeko la wakimbizi kuingia Ugiriki|Albania; mitetemeko ya ardhi nchini Chile, Uajemi, Japan, Colombia, Ecuador, Costa Rica, na Uturuki; na ongezeko la wakimbizi kuingia Ugiriki na Uturuki. Misioni yake ya kwanza kushughulikia janga kuu kwa Shirika hili ilikuwa baada ya tetemeko la ardhi nchini Japan la 1923 ambalo liliwaua takriban watu 200,000 na kuwaacha wangi wakiwa na majeraha au bila makao. Kutokana na uratibu wa Shirika hili, Chama cha Msalaba Mwekundu chaa Ujapani kilipokea bidhaa kutoka vyama vingine na kufikia jumla ya thamani ya dola milioni 100. Jambo lingine muhimu lililoanzishwa na Shirika hili ilikuwa uumbaji wa mashirika ya vijana ya Msalaba Mwekundu ndani ya Vyama vya kitaifa.

 
A stempu kutoka Uturuki Mwekundu kusaidia Crescent, 1928.

Ujumbe wa pamoja kati ya ICRC na Shirika hili katika Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Urusi kati ya 1917 na 1922 ilikuwa mara ya kwanza kwa wanaharakati hao kuhusika katika migogoro ya ndani, ingawa bado bila ya idhini mwafaka kutoka kwa Mikataba ya Geneva. Shirika hili, pamoja na msaada kutoka zaidi ya Vyama 25 vya kitaifa, lilipangw misioni ya msaada na usambazaji wa chakula na bidhaa nyingine za misaada kwa raia walioathirika na njaa na maradhi. ICRC ilifanya kazi pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu la Urusi na baadaye na Chama cha Umoja wa Kisovyeti, daima ikitilia mkazo msimamo wake wa kutoegemea upande wowote. Mwaka wa 1928, ya "Halmashauri ya Kimataifa" ilianzishwa kuratibu ushirikiano kati ya ICRC na Shirikisho la Vyama vya Msalama Mwekundu, kazi ambayo baadaye ilichukuliwa na "Tume Simamizi". Mwaka uo huo, sheria moja kwa harakati iliwekwa kwa mara ya kwanza, na kufafanua majukumu husika ya ICRC na Shirika hilo katika muungano.

Wakati wa Vita vya Abyssiniankati ya Ethiopia na Italia kutoka 1935 hadi 1936, Shirika hilo lilitoa mchango wa vifaa vya msaada wa thamani karibu faranga milioni 1.7 za Uswizi. Kutokana na kukataa kwa serikali ya Kiitaliano chini ya Benito Mussolini kushirikiana kwa vyovyote na Msalaba Mwekundu, bidhaa hizi zilifikishwa tu Ethiopia. Wakati wa vita hivi, takriban watu 29 walipoteza maisha yao huku akiwa chini ya ulinzi wa wazi wa Msalaba Mwekundu, wengi wao kutokana na mashambulizi ya Jeshi la Kiitaliano. Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uhispania kati ya 1936 na 1939, mara tena Shirika hilo lilijiunga na ICRC kutoa misaada kwa usaidizi wa Vyama 41 vya kitaifa. Mwaka wa 1939 kabla ya Vita vya Pili vya Dunia kuanza, Shirika hilo lilihamisha makao yake makuu kutoka Paris hadi Geneva ili kufaidika na sera ya Uswisi ya kutoegemea upande wowote.

 
Sherehe ya amani ya Nobel mwaka 1963; Kutoka kushoto kwenda kulia: King Olav ya Norway, ICRC Rais Leopold Boissier, Ligi Mwenyekiti John A. MacAulay. (Picture kutoka: www.redcross.int)

Mwaka wa 1952, amri ya pamoja ya 1928 ilihaririwa upya kwa mara ya kwanza. Pia, kipindi cha Ukombozi kutoka Ukoloni katika miaka ya 1960-1970 kilionyesha ongezeko kubwa katika idadi ya Vyama vya kitaifa vya Msalaba na Hilali Nyekundu. Kufikia mwishoni wa miaka ya sitini, kulikuwapo na Vyama zaidi ya 100 duniani kote. Mnamo 10 Desemba 1963, Shirikisho hili pamoja na ICRC zilipokea Tuzo ya Amani ya Nobel. Mwaka wa 1983, Shirikisho lilibadili jina na kuitwa "Ligi ya Vyama vya Msalaba na Hilali Nyekundu" kuonyesha kuongezeka kwa idadi ya Vyama vya kitaifa chini ya Chama cha Hilali Nyekundu. Miaka mitatu baadaye, kanuni saba za msingi za muungano kama zilivyobuniwa mwaka wa 1965 ziliingizwa kwenye kanuni zake. Jina la Ligi lilibadilishwa tena mwaka wa 1991 na kuwa lake la sasa rasmi la "Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Vyama vya Hilali Nyekundu". Mwaka wa 1997, ICRC na Shirikisho zilitia saini Mkatabawa Seville ambao uliaini majukumu ya mashirika haya mawili ndani ya muungano. Mwakani 2004, Shirikisho lilianza Tume yake kubwa zaidi hadi wa leo baada ya ya tsunami katika Asia ya Kusini. Zaidi ya Vyama 40 vya Kitaifa vimefanya kazi na zaidi na wafanyikazi wa kujitolea 22,000 kuleta misaada kwa waathiriwa wengi walioachwa bila chakula na malazi na kuhatarishwa na magonjwa baada ya mikurupuko.

Marais wa Shirikisho hariri

Kufikia Novemba 2009, rais wa IFRC ni Tadateru Konoe (Shirika la Msalaba Mwekundu la Kijapani). Makamu wa rais ni Paul Bierch (Kenya), Jaslin Uriah Salmon (Jamaika), Mohamed El Maadid (Qatar) na Bengt Westerberg (Uswidi).

Marais wa zamani (hadi mwaka 1977 wenye jina "Mwenyekiti") walikuwa:

Shughuli hariri

Muundo wa Muungano hariri

 
Entry ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Red Crescent Museum mjini Geneva.

Kwa jumla, kuna watu milioni 97 duniani kote ambao hutumikia ICRC, Shirikisho la Kimataifa na Vyama vya Kitaifa. Na kuna jumla ya wafanyakazi wa kudumu takriban 12,000.

Kongamano la Kimataifa la 1965 huko Vienna liliratibisha kanuni saba za msingi ambazo zilifaa kutumiwa na pande zote za Muungano, na ziliongeza kwa masharti rasmi ya Muungano mwaka wa 1986.

  • Ubinadamu
  • Kutopendelea
  • Kutoegemea Upande wowote
  • Uhuru
  • Kazi ya Kujitolea
  • Umoja
  • Ujumuiya

Kongamano la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, ambalo hufanyika mara moja kila miaka minne, ndio taasisi ya juu zaidi katika Muungano huu. Huwaleta pamoja wajumbe kutoka Vyama vyote vya kitaifa na vilevile kutoka ICRC, Shirikisho na majimbo wanachama wa Mikataba ya Geneva. Katika kati ya mikutano, Tume Simamizi huwa na jukumu la kusimami utekelezaji wa maazimio ya kongamano hizo. Isitoshe, Tume Simamizi huratibu ushirikiano kati ya ICRC na Shirikisho. Inajumuisha wawakilishi wawili kutoka ICRC (akiwemo rais wake), wawili kutoka Shirikisho (akiwemo rais wake), na watu watano ambao huchaguliwa na Kongamano la Kimataifa. Tume Simamizi hukutana kila miezi sita hivi. Aidha, mkutano wa Baraza la Wajumbe wa Muungano hufanyika kila miaka miwili katika mfululizo wa mikutano ya Kikao Kikuu cha Shirikisho. Baraza la Wajumbe hupanga na kuratibu shughuli za pamoja za Muungano.

Shughuli na Muundo wa ICRC hariri

Tume ya ICRC na majukumu yake Katika Muungano hariri

 
Nembo ya ICRC

ICRC, kama Shirika lisiloegemea upande wowote, na ni shirika linalojitegemea ina jukumu la kuchukua msimamo wa kulinda maisha na hadhi ya waathirika wa migogoro ya kimataifa na ya ndani. Kulingana na Mkataba wa Seville wa mwaka wa 1997 , ndio "Uwakala wa mbele" wa Muungano wakati wa migogoro. Kazi za umuhimu zaidi za Kamati, ambazo zinazotokana na masharti ya Mikataba ya Geneva ni kama ifuatavyo:

  • kufuatilia kuwa pande zinazozozana zinafuata Mikataba ya Geneva
  • kupanga huduma za uuguzi na usaidizi kwa waliojeruhiwa katika vita
  • kusimamia matibabu kwa Wafungwa wa vita
  • kusaidia kutafuta watu waliopotea vitani (Huduma ya Usakaji)
  • kuandaa ulinzi na huduma kwa raia wa kawaida
  • kuwa mpatanishi kati ya pande zinazo zozana katika vita

Hadhi na Muundo wa Kisheria hariri

ICRC ina makao yake makuu katika mji wa Geneva Uswisi na ina ofisi za nje katika nchi zipatazo 80. Ina wafanyakazi karibu 12,000 duniani kote, 800 kati yao wakifanya kazi katika makao makuu yake mjini Geneva, wataalamu 1200, nusu yao wakiwa wajumbe wake kusimamia misioni zake za kimataifa na nusu nyingine wakiwa wataalamu kama madaktari, wanasayansi wa biashara ya kilimo, Wahandisi au wakalimani, na takriban wanachama 10,000 wa Vyama vya kitaifa binafsi wakifanya kazi kwenye maeneo yenye mahitaji. Kinyume na inavyofikiriwa, ICRC si Shirika lisilo la kiserikali katika hali halisiya jina hilo, wala si shirika la kimataifa. Kwa kuweka kikwazo kwa uanachama wake kwa raia wa Uswizi tu(mfumo unaoitwa 'cooptation'), haina sera ya wazi ya uanachama usio na vikwazo kwa watu binafsi kama Mashirika mengine yasiyo ya Kiserikali. Neno "Kimataifa" katika jina lake halimaanishi uaanachama wake bali upana wa shughuli zake duniani kote kama ilivyo katika Mikataba ya Geneva. ICRC ina stahiki maalum na kulindwa kisheria katika nchi nyingi, kwa kuzingatia misingi ya sheria za kitaifa katika nchi hizi au kupitia mikataba kati ya Kamati husika ya kitaifa na serikali. Kulingana sheria za Kiswizi, ICRC inatambulika kama muungano wa kibinafsi. Kulingana na kanuni zake ni ina wanachama 15-25 raia wa Uswizi , ambao hujumuishwa kwa kipindi cha miaka minne. Hakuna idadi ya juu ambayo mtu wanaweza kuwa mwanachama ingawa zaidi ya wingi wa kura robo tatu za wanachama wote zinahitajika ili mwanachama kuchaguliwa baada ya kuitumikia mara tatu mtawalio.

Vyombo vya uongozi katika ICRC ni Kurugenzi na Bunge. Kurugenzi ndio Chombo Tendaji cha Kamati. Inajumuisha Mkurugenzi Mkuu na wakurugenzi watano katika maeneo ya "Utenda Kazi", "Rasilmali ya Kibinadamu", "Rasilimali na Usaidizi kwa Utenda Kazi", "Mawasiliano", na "Sheria na Ushirikiano wa Kimataifa ndani ya Muungano". Wanachama wa Kurugenzi wanateuliwa na Bunge na kuitumikia kwa miaka minne. Bunge, likijumuisha wanachama wote wa Kamati, hukutana mara kwa mara na linawajibika kuweka malengo, miongozo, na mikakati na kwa ajili ya kusimamia masuala ya kifedha ya Kamati. Rais wa Bunge pia ni rais wa Kamati kwa ujumla. Isitoshe, Bunge huchagua Baraza la wabunge watano ambalo lina mamlaka ya kuamua kwa niaba ya Bunge kamili katika baadhi ya mambo. Baraza pia ina wajibu wa kuandaa mikutano ya Bunge na kuwezesha mawasiliano baina ya Bunge na Kurugenzi.

Kwa kuwa Geneva iko katika sehemu ya Uswisi inayozungumza Kifaransa, ICRC kwa kawaida hufanya kazi zake kwa kutumia jina lake la Kifaransa Comité kimataifa de la Croix-Rouge (CICR). Ishara rasmi ya ICRC ni Msalaba Mwekundu juu ya kinyume cheupe na maneno "Comité KIMATAIFA GENEVE" yakiuzunguka msalaba.

Ufadhili na masuala ya fedha hariri

Bajeti ya 2005 ya ICRC ilifikia kiasi cha karibu faranga million 970 za Uswizi. Nyingi ya pesa hizi hutoka Uswizi ikiwa nchi shikilizi ya hazina ya Mikataba ya Geneva, kutoka kwa Vyama vya kitaifa vya Msalaba Mwekundu, majimbo yaliyotia saini Mikataba ya Geneva, na kutoka mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Ulaya. Malipo yote kwa ICRC ni kwa hiari na ni hupokelewa kama michango kwa msingi wa aina mbili ya maombi ambayo hutolewa na Kamati: Ombi la kila mwaka la Makao Makuu ili kufidia gharama zake za ndani na Maombi ya Dharura kwa misheni zake binafsi. Bajeti nzima ya mwaka 2005 inajumuisha takriban faranga million 819.7 za Uswizi (asilimia 85 ya kiasi chote) kwa ajili ya kazi zake na faranga million 152.1 za Uswizi (asilimia 15) kwa gharama za ndani. Mwaka wa 2005, bajeti kwa ya kushughulikia kazi zake iliongezeka kwa asilimia 8.6 na ile ya ndani kwa asilimia 1.5 ikilinganishwa na mwaka wa 2004, hasa kutokana na ongezeko la idadi na wigo wa misheni yake barani Afrika.[onesha uthibitisho]

Shughuli na Muundo wa Shirikisho hariri

Misheni ya Shirikisho na majukumu yake ndani ya Muungano hariri

 
Emblem ya Shirikisho

Shirikisho huaratibu ushirikiano kati ya Vyama vya kitaifa vya Msalaba na Hilali Nyekundu duniani kote na husaidia kuanzishwa kwa vyama vipya vya kitaifa katika nchi ambako hakuna vyama hivyo. Kimataifa, Shirikisho hupanga usaidizi katika kutoa misaada baada ya hali za dharura kama majanga, shida zilizosababishwa na wandadamu, mikurupuko ya magonjwa, wakimbizi wanapohama, na dharura nyinginezo. Kulingana na Mkataba wa Seville wa 1997, Shirikisho hili ndilo Uwakala uliopewa kipa mbele katika Muungano katika hali za dharura zozoto zinazotokea bila ya kuletwa na vita. Shirikisho hushirikiana na vyama vya kitaifa katika nchi husika - kila moja ikiitwa Operating National Society (ONS) - pamoja na Vyama vingine vya kitaifa vilivyo tayari kutoa msaada - ambavyo huitwa Participating National Societies (PNS). Kati ya vyama 187 vya kitaifa vyenye kikao katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho kama wanachama kamili au waangalizi, ya pata 25-30 zao hufanya kazi kama PNS mara kwa mara katika nchi nyingine. Zenye bidii zaidi kati yao ni Mashirika ya Msalaba Mwekundu ya Marekani, Uingereza,Ujerumani, na Vyama vya Msalaba Mwekundu vya Uswidi na Norway. Kazi nyingine muhimu ya Shirikisho ambayo imepata kipaumbele katika miaka ya hivi karibuni ni kujitoa kwake mhanga ili kupelekea kupigwa marufuku duniani matumizi ya bomu za kutegwa ardhini na kuleta matibabu, na msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa watu waliojeruhiwa na nchi zenye mabomu hayo.

Majukumu ya Shirikisho hiyo yanaweza kuelezwa kwa muhtasari kama ifuatavyo:

  • kueneza kanuni na maadili ya kibinadamu
  • kutoa misaada katika hali za dharura kwa kipimo kikubwa
  • kusaidia Vyama vya kitaifa katika kujitayarisha ili kukabiliana na majanga kupitia elimu kwa wanachama wake wa kujitolea na utoaji wa vifaa na vifaa vya kutoa msaada
  • kusaidia miradi ya afya kwa mitaa
  • kusaidia vyama vya kitaifa katika shughuli zinazohusu vijana

Hadhi na Muundo wa Kisheria hariri

Kama ICRC, Shirikisho hili lina makao yake makuu mjini Geneva. Pia inaendesha ofisi za kudumu 14 za mikoa na ina karibu wajumbe 350 katika zaidi ya Jumbe 60 duniani kote. Msingi wa kisheria wa kazi ya Shirikisho ni katiba yake. Mtendaji wa Shirikisho ni sekretarieti, ikiongozwa na Katibu Mkuu. Sekretarieti huungwa mkono na vitengo vinne hususan "Support Services", "National Society and Field Support", "Policy and Relations" na "Movement Cooperation". Kitengo cha Movement Cooperation hupanga mwingiliano na ushirikiano na ICRC. Ofisi kuu zaidi ya Shirikisho ni Baraza Kuu ambalo hukutana kila baada ya miaka miwili pamoja na wajumbe kutoka Vyama vyote vya kitaifa. Miongoni mwa kazi nyingine, Baraza kuu huchagua Katibu Mkuu. Kati ya mikutano Baraza Kuu, Bodi ya Uongozi ndiyo huongoza shughuli za Shirikisho. Ina mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba ya Shirikisho katika maeneo kadhaa. Bodi ya Uongozi inajumuisha rais na makamu wa rais wa Shirikisho, Mwenyekiti wa Tume ya Fedha, na wawakilishi ishirini kutoka kwa Vyama vya kitaifa. Husaidiwa na tume ya ziada nne: "Disaster Relief", "Youth", "Health & Community Services", na "Development".

Ishara ya Shirikisho ni mchanganyiko wa Mwekundu (kushoto) na Hilali Nyekundu (kulia) kwenye kinyume cheupe (zikizungukwa na mraba mwekundu ) bila maandishi mengine yoyote.

Ufadhili na masuala ya fedha hariri

Sehemu muhimu zaidi za bajeti ya Shirikisho hufadhiliwa na michango kutoka Vyama vya kitaifa ambavyo ni wanachama wa Shirikisho na pia kupitia mapato kutokana na uwekezaji. Kiasi hasa cha michango kutoka kila mwanachama huwekwa na Tume ya Fedha na kuidhinishwa na Baraza Kuu. Fedha za ziada zozote, hasa za kushughulikia gharama za ghafla wakati wa kutoa misaada hutolewa kwa kupitia maombi ambayo huchapishwa na Shirikisho na hutokana na michango ya hiari ya Vyama vya kitaifa, serikali, mashirika mengine, makampuni na watu binafsi.

Vyama vya Kitaifa ndani ya Muungano hariri

Kutambulika rasmi kwa Chama cha kitaifa hariri

 
Ambulensi inayomilikiwa na Mexican Red Cross

Vyama vya Kitaifa vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu vipo katika karibu kila nchi duniani. Nchini mwao, vyama hivi huchukua kazi na majukumu kama Chama cha kitaifa kama ilivyoandikika katika Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu. Ndani ya Muungano, ICRC inawajibika kisheria kutambua rasmi Chama cha kitaifa kama Chama cha Msalaba Mwekundu au Chama cha Hilali Nyekundu. Kanuni za kutambulikana zimewekwa katika masharti ya Muungano. Ibara ya 4 ya masharti haya ni "Masharti kwa kutambuliwa kwa Vyama vya Kitaifa":

Ili kutambuliwa, kulingana na Ibara ya 5, aya ya 2b) kama Chama cha Kitaifa, Chama hicho lazima kitimize masharti yafuatayo:
  1. Kiwe kimeundwa ndani ya jimbo la nchi huru ambapo Mkataba wa Geneva kwa Kushughulikia hali ya waliojeruhiwa na wagonjwa katika vita umeidhinishwa.
  2. Kiwe ndicho Chama cha pekee cha Kitaifa cha Msalaba Mwekundu au Hilali Nyekundu katika Jimbo hilo na kuelekezwa kutoka Mamlaka moja ambayo itakuwa peke yake yenye uwezo wa kuiwakilisha katika shughuli zake na vipengele vingine vya Muungano.
  3. Kutambuliwa kisheria na serikali ya nchi yake kwa misingi ya Mikataba ya Geneva na sheria ya taifa kama shirika la kutoa misaada ya hiari, kusaidia mashirika ya umma katika uwanja wa kazi za kibinadamu.
  4. Kiwe na uhuru wa kuendesha shughuli zake kulingana na Kanuni za Msingi za Muungano.
  5. Kutumia jina na ishara ya Msalaba Mwekundu au Hilali Nyekundu kulingana na Mikataba ya Geneva.
  6. Kuwa kimeundwa kuweza kutimiza majukumu yake kama yalivyo katika masharti yake, pamoja na kujiandaa wakati wa amani kazi za kukabiliana na vita.
  7. Kufikisha shughuli zake kwa jimbo au nchi mzima.
  8. Kuwasajili wanachama na wafanyakazi bila Kuangalia rangi, jinsia, daraja, dini au mtazamo wa kisiasa.
  9. Ambatana na Maagizo ya sasa, shiriki katika umoja ambao unaunganisha vipengele muhimu vya Muungano na kushirikiana navyo.
  10. Heshimu kanuni za msingi za Muungano na kuelekezwa katika kazi zake na kanuni za Sheria ya kibinadamu ya kimataifa.

Baada ya kutambulika na ICRC, Chama cha kitaifa hukubaliwa kama mwanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu.

Shughuli za Vyama vya kitaifa katika taifa na kimataifa hariri

Licha ya uhuru rasmi na muundo wa kazi yake, kila chama cha kitaifa bado kiko chini ya sheria za nchi yake ya nyumbani. Katika mataifa mengi, Vyama vya kitaifa vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu hufurahia stahiki ya kipekee kutokana na mikataba na serikali zao maalum au "Sheria za Msalaba Mwekundu" na kupewa uhuru kamili kama inavyotakiwa na Muungano wa Kimataifa. Kazi na majukumu ya Chama cha kitaifa kama ilivyowekwa na sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu na Kanuni za Muungano ni pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu katika vita na migogoro na hali za dharura kama majanga. Kutegemea uwezo wake wa kibinadamu, kiufundi, kifedha, na rasilimali, vyama vingi vya kitaifa kuchukua kazi ya ziada ya kibinadamu ndani ya nchi zao kama Huduma ya Kutoa Damu au kufanya kazi kama watoaji wa huduma ya Utabibu wa Dharura (Emergency Medical Service - EMS). ICRC na Shirikisho la Kimataifa hushirikiana na Vyama vya kitaifa katika misheni za kimataifa, hasa kwa kutoa usaidizi wa kibinadamu, nyenzo, fedha na kupanga mikakati katika maeneo ya kazi.

Historia ya nembo hariri

Nembo zinazotumiwa hariri

Msalaba Mwekundu hariri

 
 
Bendera ya Uswisi, ambayo awali ya Msalaba Mwekundu ni akamwambia wamekuwa derived

Nembo ya Msalaba Mwekundu iliidhinishwa rasmi mwaka wa 1863 huko Geneva. [4]

Bendera ya Msalaba Mwekundu haihusiani na Msalaba wa St George ambayo ni bendera ya Uingereza, Barcelona, Freiburg, na maeneo mengine kadhaa. Ili kuepuka mkanganyiko, ishara hii inajulikana katika hifadhi nyingine kama "Msalaba Mwekundu wa Kigiriki"; jina hili pia kutumika katika sheria ya Marekani kuelezea Shirika la Msalaba Mwekundu. Msalaba mwekundu wa St George unafikia makali ya bendera, ilhali msalaba mwekundu katika bendera ya Msalaba Mwekundu haifikii.

Bendera ya Msalaba Mwekundu mara nyingi pia huchanganyikiwa na Bendera ya Uswisi ambayo ni kinyume chake. Mwaka wa 1906, ili kusitisha ubishi kutokaa Uturuki kuwa bendera hii ina mizizi yake kutoka Ukristo, iliamuliwa kuwa kuendelezwe dhana ya kwamba bendera ya Msalaba Mwekundu ilitokana na kugeuzwa kwa rangi rasmi za Uswisi, ingawa hakuna ushahidi wa wazi kwamba asili hii iliwahi kupatikana [5]

Hilali Nyekundu hariri

 

Nembo ya Hilali Nyekundu ilitumiwa kwa mara ya kwanza na wafanyikazi wa kujitolea wa ICRC wakati wa vita kati ya Urusi na Uturuki (1877-1878). Ishara ilichukuliwa rasmi mwaka wa 1929, na hadi sasa imetambuliwa na nchi 33 za Kiislamu.

Bilauri Nyekundu hariri

 

Mnamo 8 Desemba 2005, kwa kukabiliana na shinikizo za kumkubalia Magen David Adom kama mwanachama kamili wa shirika la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu,[onesha uthibitisho] nembo mpya rasmi nembo rasmi ya tatu katika itifaki, ikijulikana kama Bilauri nyekundu) ilichukuliwa baada ya kuhaririwa kwa Mikataba ya Geneva inayojulikana kama Itifaki ya III.

Nembo zinazotambulika na kutumika hariri

Simba Mwekundu na Jua hariri

 

Chama cha Simba Mwekundu na Jua cha Iran kilianzishwa mwaka wa 1922 na kutiwa katika Muungano wa Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu mnamo 1923. [6] Hata hivyo, baadhi ya ripoti zinasema kwamba ishara hii ililetwa Geneva mwaka wa 1864[onesha uthibitisho] [7] kama jawabu kwa Hilali na msalaba zilizotumiwa na Himaya mbili wapinzani wa Iran, ya Ottoman na ya Urusi. Ingawa dai hilo haliambatani na historia ya Hilali Nyekundu, historia hiyo inapendekeza kwamba Simba Mwekundu na Juo, kama Hilali Nyekundu, zawezakuwa ziliundwa wakati wa vita vya 1877-1878 kati ya Urusi na Uturuki.

Mnamo 1980, kwa sababu ya kuhusishwa kwa nembo na Shah Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilibadilisha Simba Mwekundu na Juo na badala yake kuweka Hilali Nyekundu, sawia na mataifa mengine ya Kiislamu. Ingawa Simba Mwekundu na Jua haitumiki sasa, Iran imehifadhi haki ya kuichukua tena wakati wowote; Mikataba ya Geneva bado inaitambua kama nembo rasmi, na ilithibitishwa na Itifaki III wakati wa kupitisha Bilauri Nyekundu.[onesha uthibitisho]

Nembo zisizotambuliwa hariri

Nyota Nyekundu ya Daudi (Magen David Adom) hariri

 

Kwa kipindi cha miaka 50, Israeli iliomba kujumuishwa kwa Nyota Nyekundu ya Daudi, ikisema kuwa kwa vile nembo za Wakristo na Waislamu zilitambuliwa, nembo ya Wayahudi yafaa itambuliwe vilevile. Nembo hii imetumika tangu 1935 na Magen David Adom (MDA) Chama cha kitaifa cha msaada wa kwanza cha Israeli, lakini bado hakijatambuliwa na Mikataba ya Geneva kama ishara iliyolindwa. [8]

Shirika la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu lilikataa ombi la Israeli kwa miaka kadhaa, na kusema kuwa nembo ya Msalaba Mwekundu haikuwa iwakilishe Ukristo bali ilikuwa ni kugeuzwa kwa bendera ya Uswisi, na pia kwamba kama Wayahudi (au kundi jingine) wangepewa nembo nyingine, kungekuwa hakuna mwisho wa idadi ya makundi ya kidini au mengine yakidai nembo yao wenyewe. Walisema kwamba ongezeko kupindukia kwa alama nyekundu kungewaondoa kutoka nia asili ya nembo ya Msalaba Mwekundu, ambayo ilikuwa iwe nembo moja ya kutambulisha magari na majengo yaliyopewa ulinzi kwa misingi ya kibinadamu.

Baadhi ya mataifa ya Kiarabu, kama vile Syria, pia walipinga kuingia kwa MDA katika Shirika la Msalaba Mwekundu, na kufanya makubaliano kutowezekana kwa muda. Hata hivyo, kuanzia 2000 hadi 2006 Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekanililishikilia mchango wake (jumla ya dola milioni 42) kwa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Vyama vya Hilali Nyekundu (IFRC) kwa sababu ya IFRC kukataa kukubali MDA; hii ilipelekea kuundwa kwa nembo ya Bilauri Nyekundu na uandikishaji wa MDA tarehe 22 Juni 2006.

Nyota Nyekundu ya Daudi haitambuliwi kama ishara iliyolindwa nje ya Israeli; badala yake, MDA hutumia nembo ya Bilauri Nyekundu wakati wa oparesheni zake za kimataifa ili kuhakikisha ulinzi. Kutegemeana hali ilivyo, inaweza kuweka Nyota Nyekundu ya Daudi ndani ya Bilauri Nyekundu, au kutumia Bilauri Nyekundu peke yake.

Ukosoaji hariri

Stesheni ya Australian TV network, ABC, na kundi la haki za wazawa asili, Friends of Peoples Close to Nature, ilitoa makala yaitwayo Damu Msalababani yaliyozua madai ya kuhusika kwa Shirika la Msalaba Mwekundu na Jeshi la Uingereza kufanya mauaji katika eneo la milima kusini mwa Papua ya Magharibi. Mark Davis amefanya uchunguzi wa madai kuhusu mchango wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu Na Jeshi la Uingereza katika hali ya mateka wa WWF ya Mei 1996. [9] [10] Kufuatia kupeperushwa kwa makala haya hewani, Shirika la Msalaba Mwekundu lilitangaza hadharani kwamba lingemteua mtu binafsi nje ya shirika hilo kuchunguza madai yaliyotolewa katika filamu na wajibu wowote kwa upande wake. Ripoti inadai kwamba si dhahiri kabisa kinwango ambacho Shirika la Msalaba Mwekundu kilihusika, baadhi ya ukosoaji ukiwa kuhusu jinsi ambayo shirika lilikushughulikia mgogoro huo. [11]

ICRC haitakiwi kutoa ushahidi katika kesi za kivita kuhusu mambo iliyoyashuhudia wakati wa kutekeleza majukumu yake. Kwa sababu hii baadhi ya wakosoaji [30] wanadai kuwa wakati mwingine ICRC huwanyima haki waathiriwa wa kivita na hivyo basi kuwezesha kutojali kwa upande wa wahalifu wa kivita.

Madai ya uongozi duni na wasiwasi kuhusu uwajibikaji na uwazi yamesababisha kujiuzulu kwa maafisa wa ngazi za juu. [12] [13]

Tazama pia hariri

Vitabu hariri

  • David P. Forsythe: Humanitarian Politics: The International Committee of the Red Cross. Johns Hopkins University Press, Baltimore 1978, ISBN 0-8018-1983-0
  • Henry Dunant: A Memory of Solferino. ICRC, Geneva 1986, ISBN 2-88145-006-7
  • Hans Haug: Humanity for all: the International Red Cross and Red Crescent Movement. Henry Dunant Institute, Geneva in association with Paul Haupt Publishers, Bern 1993, ISBN 3-258-04719-7
  • Georges Willemin, Roger Heacock: International Organization and the Evolution of World Society. Volume 2: The International Committee of the Red Cross. Martinus Nijhoff Publishers, Boston 1984, ISBN 90-247-3064-3
  • Pierre Boissier: History of the International Committee of the Red Cross. Volume I: From Solferino to Tsushima. Henry Dunant Institute, Geneva 1985, ISBN 2-88044-012-2
  • André Durand: History of the International Committee of the Red Cross. Volume II: From Sarajevo to Hiroshima. Henry Dunant Institute, Geneva 1984, ISBN 2-88044-009-2
  • International Committee of the Red Cross: Handbook of the International Red Cross and Red Crescent Movement. 13th edition, ICRC, Geneva 1994, ISBN 2-88145-074-1
  • John F. Hutchinson: Champions of Charity: War and the Rise of the Red Cross. Westview Press, Boulder 1997, ISBN 0-8133-3367-9
  • Caroline Moorehead: Dunant's dream: War, Switzerland and the history of the Red Cross. HarperCollins, London 1998, ISBN 0-00-255141-1 (Hardcover edition); HarperCollins, London 1999, ISBN 0-00-638883-3 (Paperback edition)
  • François Bugnion: The International Committee of the Red Cross and the protection of war victims. ICRC & Macmillan (ref. 0503), Geneva 2003, ISBN 0-333-74771-2
  • Angela Bennett: The Geneva Convention: The Hidden Origins of the Red Cross. Sutton Publishing, Gloucestershire 2005, ISBN 0-7509-4147-2
  • David P. Forsythe: The Humanitarians. The International Committee of the Red Cross. Cambridge University Press, Cambridge 2005, ISBN 0-521-61281-0

Makala hariri

  • François Bugnion: The emblem of the Red Cross: a brief history. ICRC (ref. 0316), Geneva 1977
  • Jean-Philippe Lavoyer, Louis Maresca: The Role of the ICRC in the Development of International Humanitarian Law. In: International Negotiation. 4(3)/1999. Brill Academic Publishers, p. 503–527, ISSN 1382-340X
  • Neville Wylie: The Sound of Silence: The History of the International Committee of the Red Cross as Past and Present. In: Diplomacy and Statecraft. 13(4)/2002. Routledge/ Taylor & Francis, p. 186–204, ISSN 0959-2296
  • David P. Forsythe: "The International Committee of the Red Cross and International Humanitarian Law." In: Humanitäres Völkerrecht - Informationsschriften. The Journal of International Law of Peace and Armed Conflict. 2/2003, German Red Cross and Institute for International Law of Peace and Armed Conflict, p. 64–77, ISSN 0937-5414
  • François Bugnion: Towards a comprehensive Solution to the Question of the Emblem. Revised 4th edition. ICRC (ref. 0778), Geneva 2006

Marejeo hariri

  1. American Red Cross: Understanding of the Movement. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-06-26. Iliwekwa mnamo 2021-01-17.
  2. 2.0 2.1 Nobel Laureates Facts - Organizations. Nobel Foundation. Iliwekwa mnamo 2009-10-13.
  3. VIVANT QUI PASSE. AUSCHWITZ 1943 - THERESIENSTADT 1944. R: Lanzmann [FR, 1997]. Cine-holocaust.de. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-04-28. Iliwekwa mnamo 2009-04-14.
  4. International Kamati Mwekundu Msalaba (ICRC)
  5. "Kutoka Solferino kwa Tsushima", Pierre Boissier
  6. Historia ya Iranian Red Crescent Society (IRCS) (IRCS website, kwa Kiingereza). Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2021-01-20.
  7. IRCS tovuti, katika Kiajemi. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-04-04. Iliwekwa mnamo 2021-01-17.
  8. American Friends of Magen David Adom - ARMDI. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-01. Iliwekwa mnamo 2009-12-14.
  9. fPcN medierna Kushiriki videos - Damu ya Msalaba
  10. Leith, Denise (2002). The politics of power: Freeport in Suharto's Indonesia. University of Hawaii Press. ISBN 0824825667. 
  11. MUHTASARI NA SLUTSATSER YA uchunguzi matukio ya Mei 9, 1996 IN WESTERN PAPUA, alimkabidhi BY THE ICRC TO AN nje Consultant
  12. http://www.rte.ie/news/2009/1117/andrewsd.html
  13. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-12-03. Iliwekwa mnamo 2009-12-14.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons

Coordinates: 46°13′40″N 6°8′14″E / 46.22778°N 6.13722°E / 46.22778; 6.13722