Makao Makuu ya FAO
Jengo la FAO ni makao makuu ya kimataifa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), yaliyopo katika eneo la San Saba, Roma, Italia. Awali, jengo hili lilijengwa katika miaka ya 1930 wakati wa utawala wa kifashisti wa Italia, likikusudiwa kuwa makao ya Wizara ya Afrika ya Italia (Ministero dell'Africa Italiana).
Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, jengo hili lilibadilishwa matumizi na kuwa makao makuu ya shirika jipya la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya kilimo, FAO.
Jengo hili liko katika moja ya sehemu zenye mandhari nzuri zaidi jijini Roma, kusini mashariki mwa kilima cha Aventine (Aventine Hill), likiwa na mtazamo wa mabaki ya Baths of Caracalla na Circus Maximus.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Nel palazzo del mondo che ha fame", La Stampa, 2 June 2008. Retrieved on 2024-12-24. (Italian) Archived from the original on 2014-05-19.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |