Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (kwa Kiingereza: "Food and Agriculture Organzation of the United Nations"; kifupi: FAO) ni kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na tatizo la njaa duniani.

Nembo la FAO

Inalenga kuboresha uzalishaji na ugawaji wa mazao na vyakula duniani kwa shabaha ya kuboresha hali ya lishe ya watu duniani.

FAO iliundwa tarehe 16 Oktoba 1945 mjini Québec nchini Kanada. Tangu mwaka 1981 tarehe hiyo hukumbukwa kila mwaka kama "Siku ya Chakula Duniani".

Mwaka 1951 makao makuu yalihamishwa kwenda Roma, Italia.

Mwaka 2007 nchi 191 pamoja na Umoja wa Ulaya zilikuwa wanachama.

Shughuli za FAO ziko hasa za aina nne:

  1. FAO inawasilisha mawasiliano kati ya wataalamu kwenye uwanja wa lishe na chakula. Inaajiri wataalamu wa kilimo, biolojia, misitu, uvuvi na ufugaji. Inaendesha semina na warsha za kimataifa ambako watalaamu wanakutana na kubadilishana habari na mawazo. Tovuti ya FAO inakusanya habari husika na inatembelewa zaidi ya mara milioni kila mwezi.
  2. FAO inatuma washauri katika nchi nyingi wanaosaidia kupanga sera za kilimo.
  3. FAO inakutanisha serikali za nchi nyingi katika masuala ya lishe na kilimo.
  4. FAO inakusanya ujuzi kwa kazi ya kila siku, inaongoza au kushauri miradi elfu kadhaa ya kilimo kote duniani. Pamoja na Mradi wa Lishe Duniani inasaidia pia katika maeneo yenye njaa kwa kuleta msaada wa haraka kwa watu wasio na chakula.

Ofisi za kanda za FAO

hariri

Viungo vya nje

hariri