Jumba la Makumbusho
(Elekezwa kutoka Makumbusho)
Kwa kata nchini Tanzania, tazama Makumbusho (Kinondoni).
Jumba la Makumbusho ni jengo au taasisi penye maonyesho ya vitu vya kale, kazi za sanaa, sampuli za malighafi au vifaa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya jamii.
Mkusanyiko wa aina hii hulenga kuonyesha mifano ya sanaa, utamaduni, teknolojia au mazingira asilia kwa manufaa ya kuwaelimisha watazamaji.
Kuna majumba ya makumbusho ya aina mbalimbali yanayokazia fani fulani za elimu kama vile makumbusho ya historia, ya sanaa, ya teknolojia ya sayansi na kadhalika.
Kati ya majumba ya makumbusho mashuhuri duniani ni
- Louvre mjini Paris
- makumbusho ya Britania mjini London
- Makumbusho ya Vatikani mjini Roma
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jumba la Makumbusho kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |