Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (Dar es Salaam)

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Dar es Salaam International Trade Fair, kifupi: DITF), yanayojulikana pia kama Saba Saba, hufanyika kila mwaka mwezi Juni au Julai katika viwanja vya maonyesho vilivyopewa jina la mwanasiasa na mwanafalsafa wa siasa wa Tanzania, Mwalimu Nyerere. Maonyesho haya yanapatikana kando ya Barabara ya Kilwa, kilomita nane kusini mashariki mwa Dar es Salaam nchini Tanzania.

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni tukio kubwa la kila mwaka la matangazo linaloandaliwa na Bodi ya Biashara za Nje. Bodi hii ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria Nambari 5 ya mwaka wa 1978 ili kuongoza juhudi za Tanzania za mauzo ya nje. [1]

Historia

hariri

Viwanja vya maonyesho, vinavyojulikana pia kama Viwanja vya Maonyesho vya Mwl. J.K. Nyerere, vilifunguliwa rasmi mwaka wa 1962, mwaka mmoja baada ya Tanzania kupata uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Maonyesho haya awali yalikuwa chini ya Wizara ya Biashara na Mashirika na yalijulikana kama Maonyesho ya Kitaifa ya Kilimo na Biashara, kwa kingereza, National Agricultural and Trade Fair (NATF).

Maonyesho ya kwanza ya biashara yalifanyika mwaka wa 1963. Yaliandaliwa na mtaalam wa Uingereza kutoka Wizara ya Biashara na Mashirika, kwa msaada wa Bwana Mashamba, afisa wa wizara hiyo.

Baraza la Biashara za Nje - Board of External Trade (BET) la Tanzania limejitolea kuanzisha ushirikiano wa kibiashara duniani kwa kuandaa na kusimamia maonyesho ya biashara ya kimataifa na yaliyo maalum, maonyesho ya bidhaa za kibinafsi, utafiti wa bidhaa na masoko, ukuzaji wa uwezo, safari za kibiashara, mikutano ya wanunuzi na wauzaji, na mipango ya ushirikiano kati ya wauzaji. BET inatoa taarifa za kibiashara za mara kwa mara na huduma za ushauri kwa wazalishaji, wauzaji nje, na waagizaji ili kuwawezesha kushiriki kwa ufanisi katika soko la kimataifa. [2]

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya kisasa

hariri

Maonyesho ya Dar es Salaam yamekuwa jukwaa la kuonyesha bidhaa kutoka Tanzania, pamoja na kutoka maeneo ya Afrika Mashariki, Kati, na Kusini. Kwa msaada wa bandari ya Dar es Salaam inayotumiwa na eneo zima, maonyesho haya yanahudumu kama kitovu cha kuunganisha nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DR Congo, Zambia, Malawi, Zimbabwe, na Botswana. Maonyesho haya pia yanapata msaada kutoka kwa jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania, ambao wanayatumia kama jukwaa la kubadilishana biashara. [3]

Ushiriki wa makampuni umekuwa ukiongezeka. Kuanzia kampuni 100 tu mwishoni mwa miaka ya 1980, zaidi ya kampuni 1,041 zilishiriki mwaka wa 1999. Kufikia mwaka 2006, maonyesho yalikuwa na waonyeshaji 1,526 kutoka zaidi ya nchi 18 za kigeni. [4]

Leo, maonyesho haya yanapata msaada kutoka kwa serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara, na Masoko. Pia yanasaidiwa na Baraza la Biashara, Viwanda, na Kilimo la Tanzania yaani, Tanzania Chamber of Commerce, Industry, and Agriculture (TCCIA) na Muungano wa Viwanda vya Tanzania yaani Confederation of Tanzanian Industries (CTI), pamoja na taasisi nyingine nchini, kama vile Meridian.[5] Saba Saba sasa ni maonyesho makubwa zaidi barani Afrika, yakileta pamoja zaidi ya kampuni 3,500 za ndani, karibu kampuni 200 za kigeni, na nchi 26 zilishiriki kwenye maonyesho mwaka 2023. [6]

Wasifu wa maonyesho

hariri

Aina za waonyeshaji tunaoweza kuona kwenye maonyesho haya ni kama ifuatavyo:

  • Bidhaa za kilimo - chakula na vinywaji
  • Nguo na uzi
  • Bidhaa zinazotengenezwa
  • Teknolojia ya habari na mawasiliano
  • Vifaa vya ujenzi
  • Magari
  • Watoa huduma za usafirishaji wa bidhaa
  • Watoa huduma za usafiri wa abiria
  • Bidhaa na vifaa vya umeme
  • Bidhaa na vifaa vya kilimo
  • Vifaa vya kilimo
  • Kemikali na vipodozi
  • Mbao na samani
  • Huduma za biashara
  • Bidhaa za uhandisi
  • Mashine
  • Programu kwa ajili ya kompyuta
  • Zawadi na ufundi

Marufuku

hariri
  • Silaha na risasi
  • Madawa
  • Maudhui ya kisiasa na ya kidini

Profaili za wageni

hariri
  • Watumiaji na wafanyabiashara
  • Waagizaji
  • Wauzaji wa jumla
  • Mawakala
  • Watendaji wa biashara
  • Umma
  • VIP

Marejeo

hariri
  1. "SAMS | About DITF". tradefair.tantrade.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-05-31.
  2. "SAMS | About DITF". tradefair.tantrade.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-05-31.
  3. "THE 48th DAR ES SALAAM INTERNATIONAL TRADE FAIR (SABASABA) - TANZANIA WELCOMES ALL FOREIGN EXHIBITORS TO PARTICIPATE IN THE FAIR, FROM 28 JUNE TO 13 JULY 2024, IN DAR ES SAALAM | Embassy of Tanzania in Tokyo, Japan". www.jp.tzembassy.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-05-31.
  4. "47th Dar es Salaam International Trade Fair (Saba Saba)". Iran Trade Center Tanzania- Africa (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-31.
  5. https://ir.meridianbet.com/wp-content/uploads/2024/07/Meridianbet-Global-Half-Year-CSR-Report-2024.pdf
  6. Osman, Muhammad Nooh (20230707T1901+0200). "Exploring Opportunities: 179 Foreign Firms Join Tanzania's 2023 Saba Saba Trade Fair". Sputnik Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-31. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)