Julius Nyerere

Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Mwalimu Nyerere)

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, Mkoa wa Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo.

Mwalimu Julius Nyerere


Muda wa Utawala
26 Aprili 1964 – 5 Novemba 1985
Waziri Mkuu Rashidi Kawawa (1972–77)
Edward Sokoine (1977–80)
Cleopa Msuya (1980–83)
Edward Sokoine (1983–84)
Salim A. Salim (1984–85)
Makamu wa Rais Abeid Karume (1964–72)
Aboud Jumbe (1972–84)
Ali Hassan Mwinyi (1984–85)
aliyemfuata Ali Hassan Mwinyi

Rais wa Tanganyika
Muda wa Utawala
9 Desemba 1962 – 25 Aprili 1964
Waziri Mkuu Rashidi Kawawa

Waziri Mkuu wa Tanganyika
Muda wa Utawala
1 Mei 1961 – 22 Januari 1962
Monarch Elizabeth II
mtangulizi Ofisi iliundwa
aliyemfuata Rashidi Kawawa

Waziri Kiongozi wa Tanganyika
Muda wa Utawala
2 Septemba 1960 – 1 Mei 1961
Monarch Elizabeth II

tarehe ya kuzaliwa (1922-04-13)13 Aprili 1922
Butiama, Tanganyika
tarehe ya kufa 14 Oktoba 1999 (umri 77)
London, Uingereza
mahali pa kuzikiwa Butiama, Tanzania
utaifa Mtanzania
chama CCM
ndoa Maria Nyerere
watoto 7
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere
Chuo Kikuu cha Edinburgh
Fani yake Mwalimu
dini Ukristo (Katoliki)
tovuti juliusnyerere.info
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.

Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."

Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi.

Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma lilianza kushughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu". Baada ya hapo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limepokea jukumu la kuratibu mchakato huo pamoja na kesi kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na Nyerere kuishi muda mrefu jijini humo[1].

Maisha yake

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).

Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.

Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.

Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.

Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.

Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Alijiuzulu ualimu[2] na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

 
Julius Nyerere akiwa mzee mnamo mwaka 1977.

Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.

Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.

Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.

Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.

Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.

Mafanikio

 
Nyerere akichanganya udongo wa Zanzibar na Tanganyika wakati wa muungano mwaka 1964.

Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".

Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda.

Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).

Ukosoaji dhidi yake

 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi.

Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria.

Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.”

Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake.

Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.

Sifa zake

 
Nyerere akicheza bao kwake Butiama, akitazamwa na mwandamizi wake katika urais Ali Hassan Mwini, mke wake Mama Maria, na kaka yake, chifu Burito.

Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

 
Kaburi la Nyerere kijijini Butiama.

Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999.

Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.

Heshima na Tuzo

Nishani

Nishani Nchi Mwaka Ref
  Nishani ya José Marti   Cuba 1975 [3]
  Nishani ya Tai ya Kiazteki (Ukosi)   Mexiko 1975 [4]
  Nishani ya Amílcar Cabral   Guinea Bissau 1976 [4]
Nishani ya Eduardo Mondlane   Msumbiji 1983 [4]
  Nishani ya Agostinho Neto   Angola 1985 [4]
  Nishani ya Masahaba wa O. R. Tambo (Dhahabu)   Afrika Kusini 2004 [5]
Nishani ya Kifalme cha Munhumutapa   Zimbabwe 2005 [6][7]
  Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu)   Uganda 2005 [8]
  Nishani ya Katonga   Uganda 2005 [8]
  Medali ya Ukombozi wa Kitaifa   Rwanda 2009 [9]
  Medali ya Kampeni Dhidi ya Mauaji ya Kimbari   Rwanda 2009 [9]
  Nishani ya Kikale cha Welwitschia Mirabilis   Namibia 2010 [10]
  Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere   Tanzania 2011
  Nishani ya Kitaifa cha Burundi   Burundi 2012 [11]
  Nishani ya Jamaika   Jamaika [12]

Tuzo

Kisha kufa

Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere

  • Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967)
  • Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
    • Ndamo zimo: "The Arusha Declaration"; "Education for self-reliance"; "The varied paths to socialism"; "The purpose is man"; and "Socialism and development."
  • Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974)
    • Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru.
  • Ujamaa - Essays on Socialism' (1977)
  • Crusade for Liberation (1979)
  • Julius Kaisari, Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius Caesar
  • Mabepari wa Venisi, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare, The Merchant of Venice
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Mathayo
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Marko
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Luka
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Yohane
  • Utenzi wa Matendo ya Mitume, Tafsiri ya kishairi ya Matendo ya Mitume

Marejeo

  1. https://www.mwananchi.co.tz/habari/kitaifa/Maaskofu-Katoliki-Tanzania-kuratibu-mchakato-/1597296-5310510-i48y5n/index.html
  2. Barua ya kujiuzulu ualimu ya Julius Kambarage Nyerere
  3. Condecorado Julius K. Nyerere por el Gobierno Revolucionario con la Orden Nacional Jose Marti LANIC [LATIN AMERICAN NETWORK INFORMATION CENTER] (Granma) (Kihispania)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Awards / Prices Archived 23 Machi 2013 at the Wayback Machine. Juliusnyerere.info
  5. Government Gazette (PDF) (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). info.gov.za (11 June 2004). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 2013-05-19.
  6. Maura Mwingira (18 April 2005). Nyerere awarded Zimbabwe’s highest medal. Kafoi.com (Daily News (Harare)). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 17 June 2013.
  7. The Royal Order of Munhumutapa (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). SADC Today (4 October 2005). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-04-13. Iliwekwa mnamo 2013-05-19.
  8. 8.0 8.1 "Museveni honours Nyerere", 10 July 2007. Retrieved on 2013-05-19. (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013) Archived from the original on 2014-12-05. 
  9. 9.0 9.1 Daniel R. Kasule. "Museveni, Zenawi, Nyerere to receive national honours", The New Times, 3 July 2009. Retrieved on 2013-05-19. (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013) Archived from the original on 2013-09-28. 
  10. Tanganyika: Africa’s mecca for liberation movementsArchived from the original on 16 May 2013
  11. Museveni gets prestigious Burundi award (Kiingereza accessdate=26 Septemba 2013). New Vision (4 July 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 2013-05-19.
  12. Members of the Order of Jamaica (Deceased). Government of Jamaica. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-07-20. Iliwekwa mnamo 26 September 2013.
  13. List of the recipients of the Jawharlal Nehru Award. Indian Council for Cultural Relations. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-03-23. Iliwekwa mnamo 8 February 2013.
  14. Morales Named “World Hero of Mother Earth” by UN General Assembly. Latin American Herald Tribune. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 8 February 2013.
  15. Kikwete urges local experts to embrace integrity. Daily News (4 December 2011). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-05-16. Iliwekwa mnamo 9 February 2013.

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Julius Nyerere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.