Mariano Soler (San Carlos, 25 Machi 1846 - Gibraltar, 26 Septemba 1908) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Uruguay na askofu mkuu wa kwanza wa Montevideo, Uruguay.

Mariano Soler

Akiwa mwanafunzi katika Chuo cha Amerika Kusini mjini Roma, alipata shahada yake ya uzamivu katika Sheria za Kanisa (Canon Law).

Soler alikuwa msomi mashuhuri katika masuala ya utamaduni wa kisayansi na kifalsafa nchini Uruguay na mtetezi mkubwa wa taasisi za kikanisa (yaani, haki za Kanisa Katoliki). Alijulikana pia kwa kupinga vikali nadharia ya uteuzi wa kiasili ya Charles Darwin na Darwinism kwa ujumla..[1]

Aliandika idadi kubwa ya makala za kidini na alihudumu kama mhadhiri wa falsafa. Aidha, alichaguliwa kuwa mbunge wa Idara ya Canelones.

Marejeo

hariri
  1. Puig-Samper, Miguel Angel; Ruiz, R; Glick, T. F. (2001). The Reception of Darwinism in the Iberian World Spain, Spanish America and Brazil. Kluwer Academic Publishers. p. 44-45. ISBN 1-4020-0082-0
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.