Martin Weinek (amezaliwa 1964) ni mwigizaji, mtengenezaji mvinyo, kabaila na mburudishaji kutoka nchi Austria. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza katika tamhiliya ya Inspector Rex (akiwa kama Inspector Fritz Kunz). Pia anatengeneza pombe nchini Austria.

Martin Weinek (kulia) akiwa na Denise Zich na Kaspar Capparoni

Weinek alisomea masuala ya maigizo kuanzia 1983 hadi 1986.

Kuanzia 1986, aliapta kucheza katika moja ya sehemu ya Group 80 katika maonyesho yaliyofanyika mjini Vienna na pia alipata kucheza katika sehemu ndogo ya filamu ya Nachsaison (Baada ya msimu a), ambamo alicheza kama mhusika wa katika lifti.

Katika mwaka wa 1987, alicheza katika tamasha la Recklinghausen akiwa chini ya uongozi wake Bw. Georg Mittendrein katika seti ya The Lechner Edi looks into Paradise na pia kacheza kama mfagiaji wa mtaa katika filamu ya Müllomania ikiwa chini ya uongozi wake Dieter Berner.

Alipata kuigiza katika maonyesho ya Jura Soyfertheater Vienna kuanzia 1988 hadi 1989, vilevile katika baadhi ya maonyesho mengine ya jukwaani. Pia alishawahi kufanya kazi kama mwongozaji, kushiriki katika maigizo na utayarishaji, ambavyo vilifutiwa na kuwa kiongozi wa wasanii wa Hernalser City Theater kuanzaia 1990 hadi 1991.

Katika hali ya kuwa mwigizaji, Weinek akaja kuwa mwigizaji zaidi wa katika televisheni, na alipata kucheza katika tamthilia moja ya mwaka wa 1989 iliyojulikana kwa jina la Calafati Joe.

Mbali na uigizaji, Weinek pia ni mkuzzaji wa mvinyo, akiwa anasaidiana sambamba kabisa na mke wake, Bi. Eva. Eva awali alikuwa akifanya kazi ya uigizaji baada ya kusomea masuala ya maigizo. Wawili hao waliianza kazi ya ukuzaji wa mvinyo ikiwa kama upenzi kunako mwaka wa 1993. Wana shamba kubwa la mizabibu lenye hekta kadhaa karibu kidogo na Heiligenbrunn.

Filamu alizocheza

hariri
  • 1989: Calafati Joe (mfululizo wa tv)
  • 1999-2004, 2008- : Inspector Rex (mfululizo wa tv)
  • 2004: Silentium
  • 2005: Grenzverkehr
  • 2006: Unter weißen Segeln (Sehemu ya Träume am Horizont)
  • 2007: Die Rosenheim-Cops (Sehemu ya Liebe bis zum Ende)

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: