Maryse Condé (née Boucolon; 11 Februari 1937 - 2 Aprili 2024) alikuwa mwandishi wa riwaya na wa maigizo, pia mkosoaji wa Ufaransa, kutoka Eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa wa Guadeloupe.

Maryse Condé mnamo 2008
Maryse Condé mnamo 2008.

Condé anafahamika zaidi kwa riwaya yake ya Ségou (1984–85). [1]

Riwaya zake zinachunguza diaspora ya Waafrika iliyotokana na utumwa na ukoloni huko Karibi. Riwaya zake, zilizoandikwa kwa lugha ya Kifaransa, zimetafsiriwa kwa Kiingereza, Kijerumani, Kiholanzi, Kiitalia, Kihispania, Kireno na Kijapani. [2]

Ameshinda tuzo mbalimbali, kama vile Grand Prix Littéraire de la Femme (1986), Prix de l'Académie française (1988), Prix Carbet de la Carraibe (1997) [3] na New Academy Tuzo katika Fasihi (2018) kwa kazi zake.

Marejeo

hariri
  1. Condé, Maryse, and Richard Philcox. Tales from the Heart: True Stories from My Childhood. New York: Soho, 2001.
  2. "Maryse Condé | Columbia | French". french.columbia.edu. Iliwekwa mnamo 2019-03-16.
  3. "Author Profile: Maryse Condé". World Literature Today (September–December 2004), 78 (3/4), p. 27.
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maryse Condé kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.