Guadeloupe

département ya Ufaransa

Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement) wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.

Guadeloupe,Ufaransa
Guadeloupe

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Ufaransa Ufaransa
Mji mkuu Basse-Terre
Eneo
 - Jumla 1,628 km²
Idadi ya wakazi (2016)
 - Wakazi kwa ujumla 394,110
Tovuti:  http://www.cr-guadeloupe.fr/
Maeneo mweupe ni sehemu za Guadeloupe

Makao makuu ni Basse-Terre, ingawa mji mkubwa ni Pointe-à-Pitre.

Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni kutoka Ulaya (1493).

Ilikuwa koloni la Ufaransa halafu la Uingereza halafu la Uswidi halafu la Ufaransa tena.

Eneo lake ni km² 1,628.

Watu hariri

Idadi ya wakazi ni 394,110. Asilimia 71 za wakazi ni wa asili ya Afrika au machotara. Wazee wao waliletwa huko kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa. 15% ni Wahindi, 9% Wazungu, 3% Wachina na 2% Waarabu.

Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wengi wanaongea pia Krioli.

Upande wa dini, 80% ni Wakatoliki na 5% Waprotestanti.

Tazama pia hariri

  • Martinique, eneo lingine la Ufaransa katika Bahari ya Karibi

Viungo vya nje hariri

Serikali hariri

Safari hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guadeloupe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.