Mashine
Mashine ni kifaa kilichobuniwa na binadamu kwa kurahisisha kazi yake.
Mashine vinatumia nguvu inayoelekezwa kwa kutekeleza kazi maalumu.
Kuna mashine zenye vipande vingi vya kuzunguka kama baiskeli au saa.
Kuna mashine vyenye vipande visivyozunguka kama kompyuta au simu.
Mashine sahiliEdit
Kuna vifaa sita vinavyojulikana tangu kale na kuitwa mashine sahili (pia: mashine rahisi). Vinaongeza nguvu ya kani au vinabadilisha mwelekeo wake na kupatikana ndani ya mashine tata yaani mashine zinazojumlisha vipande vingi.
Mashine sahili ni kama zifuatazo:
Mashine tataEdit
Mashine tata ni aina ya mashine inayohitaji kani moja au zaidi katika kufanya kazi. Mfano: Baiskeli, Cherehani n.k. kwahiyo mashine tata huundwa na mashine rahisi zaidi ya moja