Masoko ni kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Iko kilomita 14 upande wa Kusini-Mashariki ya Tukuyu kando ya ziwa la volkeno.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 5,473 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,136 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 53511.

Kwenye kitovu cha Masoko kuna majengo ya boma ya kihistoria ya zamani ya ukoloni wa Kijerumani. Masoko ilikuwa makao makuu ya kikosi cha tano cha jeshi la Schutztruppe la koloni.

Wajerumani walipoondoka Masoko mnamo mwaka 1917 wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza walitupa vitu ziwani na watoto wamechukua mara kwa mara sarafu kutoka ziwani na kuziuza, hasa sarafu za heller.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Rungwe DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-13.
  Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania  

Bagamoyo | Bujela | Bulyaga | Ibighi | Ikuti | Ilima | Iponjola | Isongole | Itagata | Kawetele | Kinyala | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Lupepo | Makandana | Malindo | Masebe | Masoko | Masukulu | Matwebe | Mpuguso | Msasani | Ndanto | Nkunga | Suma | Swaya


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Masoko (Rungwe) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.