Rungwe (wilaya)

(Elekezwa kutoka Wilaya ya Rungwe)

Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania yenye Postikodi namba 53500. Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi. Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.

Mahali pa Rungwe (kijani) katika mkoa wa Mbeya.
Daraja la Mungu ni kati ya maajabu asilia ya wilaya hii.

Jina la wilaya limetokana na kituo cha misioni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban km 20 kutoka Tukuyu.

Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde".

Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270.[1]

Mnamo mwaka 2013 kata 11 zilitengwa na Rungwe na kuunda Wilaya ya Busekelo.

Barabara kuu kutoka Daressalaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya.

Rungwe inapokea mvua nyingi na iko kati ya maeneo yenye rutuba sana katika Tanzania.

Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai.

TanbihiEdit

  1. Tanzania.go.tz census/districts/rungwe. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-06-23. Iliwekwa mnamo 2004-06-23.

MarejeoEdit

  Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania  

Bagamoyo | Bujela | Bulyaga | Ibighi | Ikama | Ikuti | Ilima | Iponjola | Isongole | Itagata | Kawetele | Kikole | Kinyala | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Lupepo | Makandana | Malindo | Masebe | Masoko | Masukulu | Matwebe | Mpuguso | Msasani | Ndanto | Nkunga | Suma | Swaya


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rungwe (wilaya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.