Mramba
(Elekezwa kutoka Mbaramba)
Miramba, mibaramba au milamba ni ndege wa familia Dicruridae. Wanatokea Afrika, Asia na Australia katika maeneo yenye miti mingi. Miramba ni ndege weusi wenye domo kubwa na pana, miguu mifupi na mkia mrefu mwenye ncha iliyogawanyika sehemu mbili (isipokuwa mramba mkia-mraba). Wakitua ndege hawa husimama kabisa. Hawaogopi na hushambulia ndege wakubwa zaidi, hata ndege mbua, ili kulinda tago lao au makinda yao. Hula wadudu tu na hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika panda ya mti. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi za Afrika
hariri- Dicrurus adsimilis, Mramba Mkia-panda (Fork-tailed Drongo)
- Dicrurus aldabranus, Mramba wa Aldabra (Aldabra Drongo)
- Dicrurus atripennis, Mramba-misitu (Shining Drongo)
- Dicrurus forficatus, Mramba Kishungi (Crested Drongo)
- Dicrurus fuscipennis, Mramba wa Ngazija (Grand Comoro Drongo)
- Dicrurus ludwigii, Mramba Mkia-mraba au Mramba Sawiya (Square-tailed Drongo)
- Dicrurus modestus, Mramba Mahameli (Velvet-mantled Drongo)
- Dicrurus waldenii, Mramba wa Mayotte (Mayotte Drongo)
Spishi za mabara mengine
hariri- Chaetorhynchus papuensis (Pygmy Drongo)
- Dicrurus aeneus (Bronzed Drongo)
- Dicrurus andamanensis (Andaman Drongo)
- Dicrurus annectans (Crow-billed Drongo)
- Dicrurus balicassius (Balicassiao)
- Dicrurus bracteatus (Spangled Drongo)
- Dicrurus caerulescens (White-bellied Drongo)
- Dicrurus densus (Wallacean Drongo)
- Dicrurus hottentottus (Hair-crested Drongo)
- Dicrurus leucophaeus (Ashy Drongo)
- Dicrurus lophorinus (Sri Lanka Drongo)
- Dicrurus macrocercus (Black Drongo)
- Dicrurus megarhynchus (Paradise au Ribbon-tailed Drongo)
- Dicrurus menagei (Tablas Drongo)
- Dicrurus montanus (Sulawesi Drongo)
- Dicrurus paradiseus (Greater Racket-tailed Drongo)
- Dicrurus remifer (Lesser Racket-tailed Drongo)
- Dicrurus sumatranus (Sumatran Drongo)
Picha
hariri-
Mramba kishungi
-
Mramba mkia-mraba
-
Bronzed drongo
-
Andaman drongo
-
Spangled drongo
-
White-bellied drongo
-
Hair-crested drongo
-
Ashy drongo
-
Black drongo
-
Greated racket-tailed drongo