Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar ni bunge la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania inayojitawala katika mambo mengi ya ndani.[1]
Historia
haririBaraza lilianzishwa mwaka 1980. Kabla ya mwaka huo, Baraza la Mapinduzi lilikuwa na shughuli za serikali na pia bunge kwa muda wa miaka 16 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.[2]
Wabunge wa baraza
haririTangu uchaguzi wa mwaka 2020 baraza lina wabunge wafuatao:[3]
Aina ya Wajumbe tangu 2020 | CCM | ACT-W | TADEA | Jumla |
---|---|---|---|---|
Wajumbe wa kuchaguliwa majimboni | 46 | 4 | 0 | 50 |
Wajumbe wa Kuteuliwa na Rais | 4 | 2 | 1 | 7 |
Wajumbe Wanawake wa Viti Maalum | 18 | 0 | 0 | 18 |
Spika | 1 | - | - | 1 |
Mwanasheria Mkuu | - | - | - | - |
Jumla | 69 | 6 | 1 | 76 |
Ilhali chama cha ACT-Wazalendo kilishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 19 za kura, kiliingia katika serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na katiba ya Zanzibar.
Matokeo ya chaguzi za awali
haririTangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kulikuwa na matokeo yafuatayo:[4]
Chama | Mwaka wa uchaguzi | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1995 | 2000 | 2005 | 2010 | 2015* | 2016 | |||
Chama Cha Mapinduzi (CCM) | 26 | 34 | 30 | 48 | - | 84 | ||
Civic United Front (CUF) | 24 | 16 | 19 | 33 | - | |||
Wengine | - | - | - | - | - | 3 | ||
Jumla | 50 | 50 | 50 | 82 | - | 88 |
Uchaguzi wa mwaka 2015 ulibatilishwa na mwenyekiti wa Tume la Uchaguzi la Zanzibar. Katika marudio ya mwaka 2016 chama cha CUF hakikukushiriki. "Wengine" katika bunge la 2016 walikuwa wajumbe walioteuliwa na rais, pamoja na mwanasheria mkuu aliyeingia kutokana na cheo chake.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "The Parliament of Zanzibar, Tanzania". Commonwealth Parliamentary Association. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-28. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "History of the ZHoR". Zanzibar House of Representatives. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-29. Iliwekwa mnamo 15 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Baraza la kumi(2020-2025), uchambuzi wa kitakwimu wa aina za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ilihifadhiwa 24 Aprili 2021 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliangaliwa Aprili 2021
- ↑ "Elections in Zanzibar". Iliwekwa mnamo 15 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti rasmi ya Baraza la Wawakilishi Ilihifadhiwa 3 Mei 2017 kwenye Wayback Machine.