Mchopeko ni aina ya mchele ambao kabla ya kukobolewa mashineni huchemshwa na kisha huanikwa juani kwa ajili ya kukauka vizuri. Baadaye hupelekwa mashineni kwa ajili ya kukobolewa na kupelekwa nyumbani au madukani kwa ajili ya biashara.

Mchele wa aina hii sanasana hupatikana maeneo ya Mrimba, Malinyi, Mahenge, Ifakara.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mchopeko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.