Mipindopindo (mto)

(Elekezwa kutoka Meander)

Mipindopindo (kwa Kiingereza: meander) ni umbo la mto wenye vizingo vingi. Mipindipindo hutokea pale ambako mto unapita katika tambarare yenye ardhi laini bila mteremko mkubwa. Mipindopindo hubadilika baada ya muda kwa namna inayofanana na mwendo wa nyoka.

Mipindopindo ya Mto Clyde, Uskoti
Kutokea na kupotea kwa mipindopindo

Mipindopindo hutotokana na kizuizi fulani katika mwendo wa maji ya mto, kama vile mwamba au mti wenye ukingo. Hiki kinasababisha tofauti kati ya sehemu zenye mwendo wa haraka na mwendo wa polepole zaidi ndani ya maji.

Maji yenye mwendo mkubwa huwa na nguvu mzaidi. Hivyo yanaondoa ardhi kwenye upande wake wa ukingo na kuyabeba kama mashapo ndani yake. Kwa upande mwingine maji upande wa mwendo polepole unakosa nguvu kubeba mashapo yote ndani yake, kwa hiyo mashapo hushuka chini katika sehemu hii.

Tokeo lake ni katika kizingo:

  • upande wa nje ya kizingo maji huwa na mwendo wa haraka zaidi yakiendelea kuchimba ukingo. Mmomonyoko huo unapanua upande ule wa kizingo.
  • upande wa ndani ya kizingo maji huachana na mashapo na hivyo kupunguza urefu wake.
  • hivyo kizingo cha mto kinaanza kusogea upande wa nje.
  • mchakato huo unaweza kuendelea hadi vizingo viwili vinagusana na maji yanafuata njia mpya iliyo fupi. Kizingo kilichoachwa na mwendo wa mto kinabaki kama ziwa au bwawa.

Kujisomea

hariri
  • Hickin, Edward J. (2003). "Meandering Channels". In Middleton, Gerard V.. Encyclopedia of Sediments and Sedimentary Rocks. Kluwer Academic Encyclopedia of Earth Sciences. Dordrecht; Boston: Kluwer Academic Publishers. pp. 430–434. ISBN 1-4020-0872-4
      .
  • Leopold, Luna B.; Langbein, W.B. (Juni 1966). "River Meanders". Scientific American: 60.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Virtual Luna Leopold
  • Thonemann, P., The Maeander Valley: A historical geography from Antiquity to Byzantium (Cambridge, 2011) (Greek Culture in the Roman World Series).

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mipindopindo (mto) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.