Bwawa ni mkusanyiko wa maji mengi. Ni dogo kuliko ziwa na mara nyingi huwa limetengenezwa na binadamu. Kwa kawaida, maji huzuiwa kutumia lambo katika bonde la mto au katika ardhi iliyochimbwa, ili kuhifadhi maji. Ingawa kuna mabwawa yaliyo na neno 'ziwa' katika jina, tofauti kuu ni kuwa bwawa hutengenezwa na binadamu[1].

Bwawa la Ndakaini, Thika.
Maji ya Ndakaini hutumiwa na wakazi wa Jiji la Nairobi.
Bwawa la Haweswater linalosambaza maji Manchester, Uingereza.
Bwawa la kuzalisha umeme.

Aina hariri

Mabwawa katika mabonde hariri

 
Bwawa la Haweswater linalosambaza maji Manchester, Uingereza.

Lambo lililojengwa katika bonde hutegemea topografia asilia kwa kutoa bonde la bwawa. Malambo kwa kawaida huwekwa katika sehemu nyembamba ya bonde asilia la mto. Pande za bonde hutenda kama kuta asilia, bwawa likiwa katika sehemu nyembamba zaidi inayoweza kujengwa ili kupatia lambo nguvu na kudidimisha gharama ya ujenzi. Katika miradi ya ujenzi wa mabwawa, watu na vitu vilivyobuniwa kale huhamishwa. Kwa mfano, Mahekalu ya Abu Simbel[2] (ambavyo vilihamishwa kabla ya ujenzi wa Lambo la Aswan na kutengeneza Ziwa Nasser kutoka NiliMisri), kuhamishwa kwa kijiji cha Capel Celyn wakati wa ujenzi wa Llyn Celyn.[3]

Ujenzi wa bwawa katika bonde kwa kawaida huhitaji mto kuchepuliwa wakati wa ujenzi, mara nyingi kwa upenyo wa muda ardhini au mlizamu.[4]

Bwawa kando ya mto hariri

Wakati maji yanapovutwa kwa pampu kutoka mto kwa kiwango kikubwa, mabwawa ya kando ya mto yanaweza kujengwa kuhifadhi maji. Mabwawa hayo, yanaweza kuchimbiwa nafasi au kuzingirwa kwa kuta.[5] Kuta na sakafu za bwawa lazima ziwe hazipenyeki. Kwa mfano, mfumo wa usambazaji maji wa London hutumia mabwawa ya kando ya mto: maji hutolewa Mto Thames na Mto Lea na kuhifadhiwa katika mabwawa, k. v. Bwawa la Malkia Mary.


Matumizi hariri

Usambazaji wa moja kwa moja hariri

Mabwawa mengi yaliyojengwa kutumia lambo na yaliyo kando ya mto hupelekwa kwenye vituo vya usafishaji maji kisha kusambazwa kwa mfereji. 

 
Maji ya Ndakaini hutumiwa na wakazi wa Jiji la Nairobi

Umememaji hariri

 
Bwawa la kuzalisha umeme

Bwawa la uzalishaji umememaji huwa na tabo zikiwa zimening'inia kwenye maji. Vifaa vya uzalishaji umeme vinaweza kuwa katika sehemu ya chini ya lambo au mbali kidogo. Kwa mto ulio katika mahali tambarare, bwawa linafaa kuwa kina cha kutosha ili kutengeneza nafasi ya maji kupitia tabo; na kama kuna vipindi vya ukame bwawa linafaaa kushikilia maji ya kutosha ili kutosheleza mto. 

Baadhi ya mabwawa ya kuzalisha umememaji hurejesha maji ndani ya bwawa wakati mahitaji ya umeme yako chini, na kutumia maji yaliyohifadhiwa kuzalisha umeme wakati mahitaji yatapanda. [6]

Kudhibiti maji hariri

Bwawa linaweza kutumika kudhibiti jinsi maji yanavyotiririka:

Usambazaji wa maji – maji yanaweza kutolewa kutoka hifadhi ya maji iliyo juu na kutumiwa kama maji ya kunywa.
Umwagiliaji - maji katika bwawa la umwagiliaji linaweza kusambazwa kwa mifereji ya maji kwa ajili ya matumizi katika mashamba au mifumo ya upili ya maji.[7]
 
Ziwa Nasser hutumika katika umwagiliaji.[8]
Kudhibiti mafuriko – mabwawa ya kudhibiti mafuriko hukusanya maji katika nyakati za mvua kubwa kupita kiasi, kisha kutolewa polepole wakati baada ya wiki au miezi.
Mifereji ya maji – Ambapo mkondo wa maji hauwezi kubadilishwa, bwawa linaweza kujengwa ili kuhakikisha kiwango kizuri cha maji katika mfereji: kwa mfano, ambapo mfereji unapanda kupitia malango milimani.[9]
 
Bwawa la mapumziko tu karibu na  AachenUjerumani.
Burudani – maji yanaweza kufunguliwa kutoka bwawa ili kutengeneza hali nzuri ya kuwezesha michezo ya majini.[10] 

Burudani hariri

Kuna mabwawa ambayo huruhusu burudani k.v. uvuvi na uendeshaji mashua. Kwa mfano, Bwawa la Masinga huwa na eneo la utalii kando na uzalishaji umeme.

Athari kwa mazingira hariri

Biolojia hariri

Malambo yanaweza kuwa kizuizi cha samaki ambao huhama kulingana na msimu. Wanaeza kuwa chakula cha nyuni wa majini. Wanaweza pia kuwa wengi sana katika mfumo wa ikolojia na kusababisha kutoweka kwa spishi.

Athari kwa binadamu hariri

Mabwawa yanaweza kupunguza sana kiasi cha maji ya kinachofikia nchi zilizo chini mwa mkondo wa mto, na kusababisha uhaba wa maji, kwa mfano Sudan na Misri katika Mto Nili.

Marejeo hariri

  1. Susanna Scott. How Lakes Differ - Lake Scientist. Iliwekwa mnamo 2018-04-17.
  2. UNESCO World Heritage Centre. Nubian Monuments from Abu Simbel to Philae. Iliwekwa mnamo 20 September 2015.
  3. Capel Celyn, Ten Years of Destruction: 1955–1965, Thomas E., Cyhoeddiadau Barddas & Gwynedd Council, 2007, ISBN 978-1-900437-92-9
  4. Construction of Hoover Dam: a historic account prepared in cooperation with the Department of the Interior. KC Publications. 1976. ISBN 0-916122-51-4.
  5. Bryn Philpott-Yinka Oyeyemi-John Sawyer. ICE Virtual Library: Queen Mary and King George V emergency draw down schemes. Iliwekwa mnamo 20 September 2015.
  6. First Hydro Company Pumped Storage. Jalada kutoka ya awali juu ya 29 July 2010.
  7. Irrigation UK. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 20 September 2015.
  8. Lake Nasser. Iliwekwa mnamo 2018-04-17.
  9. Huddersfield Narrow Canal Reservoirs. Jalada kutoka ya awali juu ya 23 December 2001. Iliwekwa mnamo 20 September 2015.
  10. Canoe Wales – National White Water Rafting Centre. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-28. Iliwekwa mnamo 20 September 2015.
  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.