Meena Ally

Mtayarishaji na mtangazaji wa vipindi vya redio

Meena Ally (alizaliwa Tanzania, 13 Mei 1993) ni mtayarishaji na mtangazaji wa vipindi vya redio na televisheni , mwigizaji [1] [2]

Meena Ally
AmezaliwaKauthar Ali Rashid
13 Mei 1993
UtaifaTanzania
Majina mengineMuhaymeena/Kauthar
ElimuDar es salaam School of Journalism
Kazi yakeMedia Personality
MwenzaAnderson Mollel

Alianza kujihusisha na kazi za utangazaji wa vipindi kadhaa vya TV katika kituo cha Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) jijini Dar es Salaam kutoka 2011 hadi 2014.

Alitangaza kipindi kiitwacho Uswazi katika Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV), kipindi hicho huonesha maisha halisi ya uswahilini huku kikiongelea mada mbalimbali za kuelimisha jamii kwa ujumla.

Pia alikuwa ni mshereheshaji katika mikutano mbalimbali kwa mfano Mkutano wa Watangazaji na Wasambazaji (BDF 2018), uliofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, kwa lengo la kuunda Jukwaa la waundaji wa bidhaa ili kukutana na walinda lango wa tasnia hiyo. Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe. Huko Kenya, alialikwa na Start-Up Africa ili azungumze jinsi ya kufanya ndoto ya mtu iweze kutimia maishani na aliongea juu ya maendeleo ya vijana katika Chuo Kikuu cha The Columbia University of Nairobi.

Aliwahi kushiriki katika mkutano wa Ignite ulioandaliwa na BBC Media Action uliofanyika London ambapo wanaharakati vijana walishiriki kuzungumza juu ya uzoefu wao na changamoto zinazoikabili jamii ya vijana ulimwenguni. Amefanya kazi na BBC Media Action kuelezea changamoto mbalimbali zinazosumbua vijana kupitia kipindi kiitwacho Niambie.

Meena alishiriki katika mradi wa ujasiriamali wa kitanzania wa kuwezesha wanawake uitwao Malkia wa Nguvu unaoelezea upambanaji wa wanawake katika kujiajiri na kutetea haki zao.[3] Aliwahi kutangaza kipindi cha jioni cha burudani na habari akiwa pembeni ya mtangazaji Millard Ayo. Hivi sasa ni mtangazaji wa kipindi cha burudani kwa vijana kinachosikika kila siku mchana kupitia Clouds Fm “XXL” kupitia kipindi hiki amepata nafasi ya kufanya mahojiano na wasanii mbali mbali wa nyumbani na nje ya nchi wakiwemo : Darassa, Mwana F.A, Rema, Joe Boy, Patoranking, John Amos wa coming to America, Sauti sol na wengine wengi. Mwaka 2020, Meena amejishindia tuzo ya Tanzania consumer Choice Awards kama mtangazaji wa kike anaekubalika zaidi nchini Tanzania.

Kazi za Utangazaji

hariri

Hii ni orodha ya vituo mbalimbali alivyowahi kufanya kazi kama mtangazaji.

Mwaka Kitengo Kampuni
2011 - 2014 MTANGAZAJI WA REDIO - VOICE OVER ARTIST/RADIO PRESENTER - EATV EATV
2014-2019 MTANGAZAJI WA REDIO - BBC MEDIA ACTION (NIAMBIE) BBC MEDIA ACTION
2015 - Present MTANGAZAJI WA REDIO NA RUNINGA - CLOUDS MEDIA GROUP CLOUDS MEDIA GROUP
2007-2011 MSHEREHESHAJI Community

Shughuli za hivi karibuni

hariri

Meena Ally alianzisha chapa yake mwenyewe ya matangazo ya Promosheni, mfano ni matangazo ya Tigo fiesta 2018 ambayo yameshinda maelfu ya wafuasi wake kwa mtindo wake wa ucheshi na uvumbuzi mkubwa. Matangazo huwa kawaida mafupi lakini yana ujumbe wa kuvutia ambayo huacha hisia kwa wasikilizaji na kutumia misemo mifupi yenye ucheshi kama hatuli kwa kushiba tunakula kumaliza n.k. Meena ameonekana kama mtangazaji wa kike jasiri na wa kuvutia katika onyesho la Bongo Star Search (BSS), ambalo ni shindano la kusaka vipaji vya muziki wa Afrika Mashariki kwa talanta za vijana. Amefanya kazi katika vyombo vya habari na katika maonyesho makubwa ya jukwaani, hata baada ya masomo yake katika Shule ya Uandishi wa Habari, Meena Ally alifanya kazi ya utangazaji wa programu mbalimbali za televisheni katika EATV tangu mwaka 2011 mpaka 2014.

Marejeo

hariri

Mengineyo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meena Ally kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.