Meta-Wiki ni tovuti ya Wikimedia Foundation na mahali muhimu pa kuendeleza na kusimamia miradi yote ya shirika hii.

Nembo ya Meta-Wiki

Miradi kama Wikipedia, Wiktionary, Wikiquote, Wikisource, Wikinews, Wikibooks, Wikiversity au Wikimedia Commons hutumia programu ya pamoja inayozidi kuendelezwa.

Vile maswali ya kuanzisha miradi ya wiki kwa lugha mpya yanajadiliwa hapa. Kama jumuiya inayohariri wikipedia kwa lugha fulani imepatwa na fitina na inashindwa kupatana kati yao wasimamizi kwenye ngazi ya Meta-Wiki wanaweza kuingilia kati.

Vilevile wasimamizi wa Meta-Wiki wanaangalia kama haki za hatimiliki inaangaliwa katika matumizi ya picha. Ila mara nyingi wao hufanya kazi za kuratibu miradi yote ya Wiki, yaani, swala zima la kiufundi wao ndiyo wana uwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya miradi yote husika na Wikimedia.

Kiungo

hariri