Wikimedia Foundation

Wikimedia Foundation ni shirika lisilo la kiserikali lililopo Marekani linaloendesha mradi wa Wikipedia pamoja na miradi mingine.

Nembo la Wikimedia Foundation
Wikimedia Foundation, San Francisco

Shabaha yake ni usambazaji wa elimu huria inayopatikana bure kwa watu wote kwa njia ya mtandao. Lilianzishwa na Jimmy Wales mwaka 2001. Shirika linaendeleza maendeleo ya programu huria za wikiwiki zinazomruhusu msomaji si kusoma tu bali kuandika na kuhariri vilevile.

Kwa ujumla karibia miradi yote ya Wikimedia Foundation si ya kibiashara na maudhui yote yaliyomo katika miradi hiyo hutungwa na wachangiaji wengi wanaojitolea bila malipo kutoka karibia pande zote za Dunia.

Mapato ya shirika hutokana na michango ya watu binafsi. Pia makampuni mbalimbali na taasisi za elimu hujitolea pia kwa kutoa kompyuta na nafasi ya kutunza data kwenye server zao.

Miradi mingine ya Wikimedia Foundation ukiacha ule wa Wikipedia ni pamoja na Wikamusi (Wiktionary), Wikiquote, Wikisource, Wikinews, Wikibooks, Wikiversity, Wikimedia Commons na Meta-Wiki.

Shirika hili haliangalii yaliyomo kama makala ya Wikipedia ambayo hutungwa na jumuiya za watumiaji katika lugha zinazofikia karibu 200.

Viungo vya NjeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikimedia Foundation kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.