Mfalme Dongmyeong wa Goguryeo
Mfalme Dongmyeong wa Goguryeo (58 - 19 KK, au 37 – 19 KK), "Dongmyeongseongwang" (東明聖王) pia anafahamika kwa jina lake la kuzaliwa kama Jumong, alikuwa kiongozi mwanzilishi wa taifa la Goguryeo, huko mbali kabisa kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Falme Tatu za Korea. Wakati wa Gwanggaeto Stele, alimwita Chumo-wang (Mfalme Chumo). Wakati wa Samguk Sagi na Samguk Yusa, alirekodiwa akimwita kama Jumong, na jina lake la ukoo la Go. Wale wakina Samguk Sagi walielezea kwamba pia alikuwa akijulikana kama Chumo au Sanghae (상해, 象解). Jina hili pia kuelezewa kwa rekodi nyingine kama Chumong (추몽, 鄒蒙), Jungmo (중모, 中牟 au 仲牟), au Domo (도모, 都牟).[1]
Ufalme wa Korea Goguryeo |
---|
|
Kwenye tamaduni maarufu
haririMnamo 2006-2007, mtandao wa televisheni wa Korea Kusini (Munhwa Broadcasting Corporation, kifupi 'MBC) umerusha hewani mfululizo wa kipindi cha maarufu chenye vipengele 81, Jumong.
Kifo na Urithi
haririJumong alikufa mnamo 19 KK akiwa na umri wa miaka 40.[2] Mtoto wa (Yuri) kamzika baba yake ndani ya kaburi la pyramid, na kumpa jina la Chumo-seongwang.
Familia
hariri- Mke wa 1: Bi. Ye So Ya
- Yuri (Mfalme Yuri),
- Mke wa 2: So Seo-no
- Biryu
- Onjo (Mfalme Onjo)
Marejeo
hariri- ↑ Digital Korean Studies http://www.koreandb.net/KPeople/KPShow.asp?ID=0003672&Type=L
- ↑ 秋九月 王升遐 時年四十歲 葬龍山 號東明聖王, 《Samguksagi》 Goguryeo, volume 13.