Miranda Naiman
Miranda Naiman ni mjasiriamali Mtanzania, mmiliki na mwanzilishi wa kampuni iitwayo Empower na mmoja wa waanzilishi wa mgahawa ujulikanao kama Inspire cafe[1][2].
Miranda Naiman | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | Mjasirilamali |
Aliwahi kutajwa kama mmoja kati ya wanawake 20 wenye nguvu na waliofanikiwa nchini Tanzania na pia aliwahi kutajwa na gazeti maarufu la Marekani (Forbes) linaloangazia mambo ya biashara kuwa ni mtaalamu wa kukuza vipaji vya watu[3].
Mbali ya hayo, kuanzia Julai 2019 mpaka sasa Miranda Naiman ni rais katika umoja wa Wajasiriamali unaojulikana kama Enterprenuership Organization (EO)[4][5].
Elimu
haririMiranda ni mmoja wa wahitimu katika shule ya International School of Tanganyika (IST) mwaka 2000. Baada ya hapo Miranda alijiunga na chuo cha Central school of speech and Drama cha jijini London akichukua masomo ya shahada ya BA (HONS) Drama, applied Theatre and education. Baada ya hapo aliunganisha masomo ya shahada ya uzamili chuo cha Leeds katika masomo ya Theatre and development studies. Aliendelea kusoma huku akifanya kazi mbalimbali nchini humo. [6]
Kazi yake
haririMiranda Naiman mbali na kuwa mjasiriamali pia ni mama wa mtoto mmoja wa kiume. Mwaka 2019, Miranda alichaguliwa kuwa mmoja kati ya wanawake mia nchini chini ya mtandao unaojulikana kama Sheroes, ikiwa ni wanawake wenye michango chanya kwenye jamii.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.istafrica.com/b/~board/blog-posts/post/international-school-of-tanganyika-alumna-miranda-naiman-the-accidental-entrepreneur
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/business/american-chamber-bank-m-train-over-1000-youth-entrepreneurs
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/news/Top-20-Superwomen/1840340-5033398-gg8oj0z/index.html
- ↑ 2.https://blog.eonetwork.org/tag/miranda-naiman/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-27. Iliwekwa mnamo 2020-04-03.
- ↑ https://www.istafrica.com/b/~board/blog-posts/post/international-school-of-tanganyika-alumna-miranda-naiman-the-accidental-entrepreneur
Viungo vya Nje
hariri- https://www.cnbcafrica.com/videos/2019/10/25/miranda-naiman-assesses-how-africa-list-is-reshaping-continent-by-reskilling-its-workforce/ Ilihifadhiwa 12 Desemba 2019 kwenye Wayback Machine.
- https://www.thecitizen.co.tz/magazine/Stay-humble--never-give-up-in-business/1840564-4636490-prifyyz/index.html
- http://www.bbc.co.uk/worldservice/specials/1433_City_Secrets/page5.shtml
- https://africanbusinessmagazine.com/press/youth-entrepreneurship-empowered-via-daraja-la-mafanikio-bridge-success-seminar/ Ilihifadhiwa 16 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine.
- https://www.empower.co.tz/team
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Miranda Naiman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |