Misemo
maana za misemo
Misemo ni kauli fupifupi zinazotumiwa na jamii ili kusisitiza ukweli wa jambo fulani. Ni mafungu ya maneno ambayo hutumiwa na jamii fulani kwa lengo la kutoa msisitizo wa maadili fulani.
Misemo huunganisha dhana au mawazo mawili kuwa moja.
Mifano:
- Elimu ni ufunguo wa maisha
- Mtu ni afya
- Heshima ya mtu ni utu
- Mtu kwao
- Maji ni uhai'
- Hasara roho pesa makaratasi
- Kikubwa uhai
- Hujafa hujaumbika
- Masikini hana hoja
- Samaki anayefunga mdomo wake hashikwi na ndoano ya mvuvi
- Daima dawama
- udi na budi
Msemo unapokuwepo katika jamii kwa muda halafu ukatoweka basi unaitwa "msimu".
Tazama pia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Misemo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |