Mtandao wa kompyuta

(Elekezwa kutoka Mitandao ya kompyuta)

Mtandao wa kompyuta ni kundi la kompyuta ambazo zimeunganishwa kwa madhumuni ya mawasiliano. Mitandao yaweza kupangwa kulingana na sifa mbalimbali Makala haya yanatoa maelezo ya ujumla ya baadhi ya aina na makundi ya mtandao. Pia inatoa msingi wa vipengele vya mtandao. Mtandao wa kompyuta unaojulikana zaidi ukiwa pia mkubwa kabisa ni intaneti lakini kuna mitandao Mingi.

uanishaji wa matandao ya kompyuta

Utangulizi

hariri

Mtandao wa kompyuta huruhusu mawasiliano kati ya kompyuta na kompyuta nyingine nyingi na kuwezesha ushirikiano wa rasilimali na habari baina ya kompyuta. "Advanced Research Projects Agency" (ARPA) ilifadhili mpango wa "Advanced Research Projects Agency Network" (ARPANET) inayotumiwa na Idara ya Ulinzi huko Marekani. Ulikuwa mtandao wa kompyuta wa kwanza kutumika duniani. Kuundwa kwa mtandao kulianza mwaka 1969, kwa kuzingatia miundo iliyoanzwa katika miaka ya 1960.

Uainishaji wa mitandao

hariri

Orodha ifuatayo yatoa makundi yanayotumika kwa uainishaji wa mitandao.

Mbinu ya uunganishaji

hariri

Mitandao ya kompyuta pia yaweza kuainishwa kulingana na vifaa vya programu kiteknolojia ambayo hutumiwa kwa kuunganisha vifaa katika mtandao, kama nyaya za optiki, Ethernet, LAN isiyotumia nyaya, HomePNA, Nyaya za nguvu ya mawasiliano au G.hn. Ethernet hutumia nyaya kuunganisha vifaa. Vifaa vinavyotumika mara kwa mara ni pamoja na mahabu, swichi, madaraja na / au ruta.

Teknolojia ya LAN inayotumia nyaya imeundwa kwa kuunganisha vifaa bila kuweka nyaya. Vifaa hivi hutumia mawimbi ya redio au miale ya Infraredkama njia ya kuwasilisha ujumbe.

Teknolojia ya ITU-T G.hn inatumia nyaya zilizowekwa nyumbani (Waya wa Koaxial , nyaya za simu na [[]]nyaya za nguvu za umeme kuunda mtandao wa kieneo wenye kasi (karibu 1 Gigabits/s).

Teknolojia ya Kutumia Nyaya

hariri

Waya jozi uliopindwa - Hii ndiyo njia inayotumika sana kwa mawasiliano. Waya jozi uliopidwa ni nyaya za kawaida za simu ambazo zinahusisha nyaya mbili za shaba zilizopindwa na ambazo zimewekwa kizuizi na hutumika kwa upeperushaji wa sauti na data pamoja. Matumizi ya nyaya mbili zilizopindwa pamoja husaidia kupunguza madhara yasiyofaa na uharibifu utokanao na nguvu za usumakumeme. Kasi ya upeperushi huwa kutoka biti milioni 2 kwa sekunde moja hadi biti milioni 100 kwa sekunde moja.

Waya wa Koaxial - Hizi ni nyaya zinazotumika sana kwa televisheni za mfumo wa waya, majengo ya ofisi, na makao mengine ya kazi ya mitandao ya kieneo. Nyaya hizi zimeundwa kwa shaba au alumini na kufungwa pamoja kwa tabaka la kifaa kinama na ambacho kina uwezo mkubwa wa kidielekitiki. Kizuizi cha tabaka husaidia kupunguza kuingiliwa na kuvurugwa.Kasi ya Upeperushi huwa kutoka milioni 200 na zaidi ya biti milioni 500 kwa sekunde moja.

Nyaya za Optiki - Nyaya hizi huundwa kwa uzi au nyuzi nyepesi sana za nyuzi za kioo ambazo zimefungwa katika tabaka la kinga. Hupeperusha mwangaza ambao unaweza kusafiri umbali mrefu na wa upana mkubwa. Nyuzi za optiki haziathiriwi na miale ya mnururisho wa usmakumeme. Kasi ya upeperushaji yaweza kwenda hadi biti zaidi ya trilioni kwa sekunde moja. Kasi ya nyuzi za optiki huwa mara mia zaidi kuliko nyaya za Koaxial na mara zaidi ya elfu kwa kasi, kuliko waya-jozi uliopindwa.

Teknolojia isiyotumia nyaya

hariri

Mawimbi madogo ya Nchi kavu - Mawimbi madogo ya nchi kavu hutumia vifaa vya upeperushaji na upokeaji vilivyo duniani. Vifaa hivi hufanana na sahani za satelaiti. Mawimbi madogo ya Nchi kavu hutumia vitengo vya gigahertz za chini ambazo hufupisha mawasiliano kuwa kwenye upeo wa macho. Njia za kati za vituo vya upeperushaji huwa zimeachana kwa maili 30 kati yake. Antena za mawimbi madogo kawaida huwekwa juu ya majengo, minara, vijilima, na vilele vya milima.

Mawasiliano ya Satelaiti - Satelaiti hutumia mawimbi madogo ya redio kama njia yake ya mawasiliano ambayo hayapindwi na anga ya dunia. Satelaiti huwekwa katika anga, karibu maili 22,000 juu ya ikweta. Mifumo hii inayozunguka-Dunia huwa na uwezo wa kupokea na kupeperusha sauti, data, na siginali za TV.

Mifumo ya Cellular na PCS - Hutumia teknolojia ya mawasiliano kadhaa ya redio. Mifumo hii imegawanyika kwa maeneo tofauti ya kijiografia. Kila eneo lina kipeperushi cha nguvu ya chini au mlingoti wa upokezi wa redio ambao hupokea na kupokeza simu kutoka kwa eneo moja hadi lingine.

LAN zisizotumia nyaya - mtandao wa kieneo usiotumia nyaya hutumia teknolojia ya redio yenye masafa ya juu ufananao na cellular ya digitali na teknolojia ya redio ya masafa ya chini. LAN zisizotumia nyaya hutumia teknolojia ya spectrum kuwezesha mawasiliano kati ya vifaa vingi katika eneo dogo. Mfano wa teknolojia ya wawimbi ya redio na isiyotumia nyaya na iliyo na uwazi wa wastani ni IEEE 802.11b.

Bluetooth - Hii ni teknologia ya umbali wa karibu. Hufanya kazi kwa karibu 1Mbps na kitengo cha mita 10-100. Bluetooth ni mtandao wa itifaki zilizowazi na zinazotumia waya, unaotumika kwa kubadilishana data kwenye umbali mfupi.

Wavuti isiyotumia nyaya - wavuti isiyotumia nyaya inahusu matumizi ya wavuti kupitia kwa vifaa kama simu za cellular, pagers, PDAs, na vifaa vingine vya mawasiliano vinavyobebwa. Huduma ya wavuti isiyotumia nyaya hutolewa na kuunganisha watu wakati wowote / mahali popote.

Kipimo

hariri

Mitandao mara nyingi huainishwa kama Mtandao wa Tarafa, (Local Area Network )(LAN), Wa Eneo Kubwa ,(Wide Area Network) (Wan),Eneo la Mjini, (Metropolitan Area Network) (MAN), Mtandao wa Eneo la Kibinafsi,( Personal Area Network )(PAN), Mtandao wa Kifaragha, (Virtual Private Network) (VPN), Mtandao wa Eneo la Chuo, (Campus Area Network) (CAN), Mtandao wa Eneo la kuhifadhi Bidhaa, (Storage Area Network )(SAN), nk. kutegemea na kiwango chake, upeo na kusudi. Matumizi, uaminifu na haki za upatikanaji mara nyingi hutofautiana kati ya aina hizi za mtandao - kwa mfano, LAN yaelekea huundwa kwa ajili ya matumizi ya ndani kwa ndani, wa mifumo ya ndani ya shirika na wafanyakazi katika maeneo ya makazi yao binafsi {kama vile jengo), wakati, WANs inaweza kuunganisha pamoja sehemu zilizo tofauti za shirika moja, na pengine pia kuunganisha vikundi vinginevyo vya tabaka la tatu.

Uhusiano wa utendaji (usanifu wa mtandao)

hariri

Mitandao ya kompyuta inaweza kuainishwa kulingana na uhusiano wa utendaji uliopo miongoni mwa vifaa vya mtandao, mfano, Shughuli za mtandao (Active Networking), huduma-kwa mtumiaji (Client-server) na usanifu wa rika kwa rika (Peer-to-peer) (kundi la utendaji kazi).

Topolojia ya Mtandao

hariri

Mitandao ya kompyuta inaweza kuainishwa kulingana na topolojia ya mtandaoambayo huwa msingi wa mtandao, kama mtandao wa bus, , mtandao wa Kinyota, mtandao wa pete, mtandao wa meshi, na mtandao wa kinyota-bus, mti au mtandao wa topolojia ya moja kwa moja. Aina ya Mtandao inaashiria njia ambayo vifaa katika mtandao hupata mantiki katika mpangilio wa uhusiano wa kimoja kwa kingine. Matumizi ya neno "mantiki" hapa ni muhimu. Kwamba aina ya mtandao haitegemei mpangilio halisi wa mtandao. Hata kama kompyuta zilizounganishwa kwa mtandao zimewekwa mkabala kwa safu, kama zimeunganishwa na kupitia habu, huo mtandao una aina ya Kinyota, badala ya aina ya basi. Kwa njia hii,sifa zinazoonekana na zile za kiutenda kazi za mtandao ni bainifu; aina ya mantiki ya mtandao si muhimu kwa namna moja katika mpangilio halisi. Mitandao inaweza kuainishwa kuzingatia utaratibu wa data unaotumiwa kuwasilisha data, hizi ni pamoja na mtandao wa Digitali na Analogi.

Aina za mitandao

hariri

Chini ni orodha ya aina ya mitandao ya kompyuta inayotumika sana iliyopangwa kulingana na ukumbwa.

Mtandao wa kieneo wa kibinafsi

hariri

A Mtandao wa kieneo wa kibinafsi (PAN) ni mtandao wa kompyuta unaotumiwa kwa mawasiliano kati ya vifaa vya kompyuta vilivyo karibu na mtu mmoja. Baadhi ya mifano ya vifaa ambavyo hutumika katika PAN ni kompyuta binafsi, machine ya kuchapisha, mashine ya faksi, simu, PDAs, skana, na hata michezo ya video. PAN kama hii yaweza kuhusisha unganisho la nyaya au lisilotumia nyaya kati ya vifaa. PAN ina upeo wa angalau futi 20-30 (karibu mita 6-9), lakini hii inatarajiwa kuongezeka kwa maboresho ya teknolojia.

Mtandao wa eneo la karibu

hariri

Mtandao wa eneo la karibu (LAN) ni mtandao wa kompyuta unaovusha katika eneo ndogo, kama vile nyumba, ofisi, au kikundi kidogo cha majengo, kama vile shule, au uwanja wa ndege. LAN zinazotumia nyaya kwa sasa huwa zimeundwa kwa teknolojia ya Ethernet, ingawa viwango mpya kama ITU-T G.hn pia hutoa njia ya kuunda LAN zinazotumia nyaya zikitumia nyaya zilizo nyumbani (nyaya za Koaxial , nyaya za simu na nyaya za umeme) [1]

Kwa mfano, maktaba yaweza kuwa na LAN inayotumia au isiyotumia nyaya kwa kuunganisha vifaa vilivyo karibu (kama, mitambo ya kupiga chapa na seva) na kuunganisha na mtandao.. Katika LAN itumiayo nyaya, KompyutaPC kwenye maktaba kawaida huunganishwa na kikundi cha jamii ya waya cha 5 (Cat5), ikitumia itifaki ya 802.3 IEEE katika mfumo wa vifaa vilvyounganishwa pamoja na hatimaye kuunganishwa kwenye mtandao. Nyaya za seva kawaida huwa kutoka kwa kikundi cha nyaya zilizoongezwa nguvu za 5e, ambazo hutumia IEEE 802.3 katika 1 Gbit / s. LAN isiyotumia nyaya yaweza kutumia itifaki tofauti ya IEEE i, 802.11b, 802.11g au pengine 802.11n. Kompyuta za wafanyikazi (angavu kwa kijani kibichi katika mchoro) zaweza kutumia mtambo wa kuchapisha (printa) kwa rangi tofauti, itazame rekodi, na mtandao wa kiakademia na wavuti. Kompyuta za watumiaji zaweza kupata wavuti na orodha ya kadi. Kila kundi la ufanyikazi laweza kufikia machine yao ya kuchapisha- printa ya eneo lao. Zingatia kuwa machine ya kuchapisha haiwezi kutumika na kikundi kilicho nje ya kundi lao la ufanyikazi wake.

 
Maktaba ya kawaida ya mtandao, katika topolojia ya matawi na udhibiti wa kupata rasilimali

Vifaa vyote vilivyounganishwa lazima vielewe tabaka la mtandao (tabaka la 3), kwa sababu zinashughulikia vitanzu vingi (rangi tofauti). Wale walio ndani ya maktaba, iliyo na uunganisho la Ethernet la 10/100 Mbit / s tu na kuunganishwa na vifaa vya mtumiaji na uunganisho la Ethernet Gigabit kwa ruta kuu, wanaweza kuitwa " Swichi za safu ya 3" kwa sababu wana kusano la Ethernet tu na lazima ielewe IP. Itakuwa sahihi zaidi kuwaita ruta za uunganisho, ambapo ruta sasa ipo juu ya usambazaji wa wavuti na mitandao ya kielimu' ruta za kuunganisha wateja.

Sifa bainifu za LAN, tofauti zake WANs(Mitando ya maeno pana), ni pamoja na kupeleka data kwa kasi ya juu sana, eneo ndogo la kijiografia, na ukosefu wa haja ya mawasiliano ya nyaya zilizokodishwa. Kwa sasa Ethernet au LAN za teknolojia ya 802.3 IEEE hufanya kazi kwa kazi ya hadi 10 Gbit / s. Hiki ndicho kiwango cha kupeleka data. IEEE ina miradi ya uchunguzi ya kuweka kitengo cha 40 na 100 Gbit / s. [ [2]

Mtandao wa eneo la bewa

hariri

Mtandao wa eneo la bewa (CAN) ni mtandao wa kompyuta unaoundwa kwa kuunganisha mitandao ya maeneo ya karibu (LANs) kwenye eneo ndogo la kijiografia. Unaweza kuchukuliwa kama aina mojawapo ya mitandao ya eneo la mijini, hususani kwa mpangilio wa kitaaluma.

Katika mandhari ya chuo kikuu, mtandao wa bewa uliojikita katika mtandao wa eneo la bewa, unauwezekano wa kuunganisha majengo ya bewa yakiwemo; Idara za kitaaluma , maktaba ya chuo kikuu na nyumba za maakazi za wanafunzi. Mtandao wa eneo la bewa ni mkubwa kuliko mtandao wa eneo la karibu lakini ni mdogo kuliko mtandao wa eneo pana (WAN) (katika baadhi ya mandhari).

Lengo kuu la mtandao wa eneo la bewa ni kuwawezesha wanafunzi wa chuo kikuu kupata wavuti na rasilimali za chuo kikuu. Huu ni mtandao unaounganisha LAN mbili au zaidi pamoja lakini iliyo tu kwa eneo maalum la kijiografia kama bewa la chuo, ukumbi wa viwanda, jengo la ofisi, au kambi ya kijeshi. A CAN inaweza kuonekana kama aina ya MAN (mtandao wa eneo la mji mkuu), lakini kwa ujumla inahusisha eneo ndogo kuliko MAN. Neno hili mara nyingi hutumika kujadili utekelezaji wa mitandao kwa eneo la mpaka mmoja. Hili halipaswi kukanganywa na Mtandao wa Eneo la udhibiti. LAN huunganisha vifaa vya mtandao kwa umbali mfupi. Jengo la ofisi, shule, au nyumba zenye mtandao kwa kawaida huwa na LAN moja, ingawa wakati mwingine jengo laweza kuwa na LAN chache ndogo(labda moja kwa kila chumba), na mara kwa mara LAN itafuturi kwa kundi la majengo ya karibu.

Mtandao wa eneo la mji mkuu

hariri

Mtandao wa eneo la mji mkuu (MAN) ni mtandao unaounganisha mitandao miwili au zaidi ya eneo la karibu au mitandao ya eneo la kampasi pamoja lakini haina upana nje ya mipaka ya mji/jiji. Ruta, Swichi au habu huunganishwa ili kuunda mtandao wa eneo la mji mkuu.

Mtandao wa eneo pana

hariri

Mtandao wa eneo pana (Wan) ni mtandao wa kompyuta unaotanda kwa eneo pana (yaani mtandao wowote wa viungo vya mawasiliano vinavyopita jiji kuu, kikanda, au mipaka ya kitaifa [1]). Kwa njia isiyo rasmi WAN ni mtandao unaotumia ruta na viungo vya mawasiliano ya umma. Tofauti na mitandao wa kieneo ya kibinafsi (Pans),mitandao ya eneo la karibu (LANs),mitandao ya eneo la kampasi (CANs), au mitandao ya eneo la Jiji kuu (Mans), ambayo kwa kawaida ina ukadirifu wa chumba, jengo, kampasi au eneo maalum (mfano, mji) kwa mpangilio huo. Mfano wa WAN unaojulikana kwa wengi na kwa ukubwa ni wavuti. Wan ni mtandao wa mawasiliano wa data uliotanda kwa eneo pana la kijiografia (yaani mji mmoja hadi mwingine na nchi moja kwenda nchi nyingine) na ya kwamba mara nyingi hutumia vifaa vya upokezi vinavyotolewa na vifaa vya uchukuzi vya kawaida, kama kampuni za simu. Teknolojia ya Wan kwa ujumla hufanya kazi katika tabaka tatu za chini za Kielelezo cha kumbukumbu cha OSI: tabaka la mahali halisia, tabaka la kiungo cha data na tabaka la mtandao.

Mtandao wa eneo la kimataifa

hariri

Ainisho bainifu la mitandao ya ulimwengu (GAN) (angalia pia IEEE 802,20) lipo katika harakati za ujenzi na vikundi kadhaa, na hakuna ufasili wa aina moja. Kwa ujumla, hata hivyo, GAN ni muundo wa kusaidia mawasiliano ya sabili katika LAN zisizotumia nyaya, maeneo yaliyogubikwa na satelaiti, nk.Changamoto muhimu katika mawasiliano ya sabili ni "kupokeza" mawasiliano ya mtumiaji kutoka eneo moja hadi lifuatalo. Katika Mradi wa IEEE 802, hii inahusisha mfululizo wa mitandao ya maeneo ya karibu isiyotumia nyaya (WLAN) ya nchi kavu .[3]

Mtandao dhahania wa kibinafsi

hariri

Mtandao dhahania wa kibinafsi (VPN) ni mtandao wa kompyuta ambao baadhi ya viungo katikati mwa vitengo hubebwa kwa unganisho lililowazi au mzungusho wa dhahania katika baadhi ya mitandao mikubwa (kwa mfano, wavuti) badala ya nyaya halisi. Itifaki za tabaka la kiungo cha data cha mtandao dhahania zinasemekana kupitishwa kwa mtandao mkubwa zikiwa katika mandhari haya. Mojawapo ya utendaji ni mawasiliano yaliyo salama kupitia kwa mtandao wa umma, lakini hamna haja VPN kuwa na vipengele vya usalama , kama vile uthibitishaji au usimbaji fiche wa maudhui. VPN, kwa mfano, inaweza kutumika kutofautisha mfuatano wa watumiaji wa jamii tofauti juu ya msingi wa mtandao na vipengele vya usalama.

VPN yaweza kuwa na utendaji wa juhudi-bora, au yaweza kuwa na kiwango maalumu cha huduma cha mkataba wa (SLA) kati ya mteja wa VPN na mtoa huduma wa VPN. Kwa jumla, VPN ina topolojia kubwa zaidi kuliko ncha-kwa-ncha.

VPN inaruhusu watumiaji wa kompyuta kuonekana kuhakiki kutoka kwa eneo la anwani ya IP mbali na ile halisi waliounganishwa nayo kwa mtandao.

Muungano wa Mitandao

hariri

Muungano wa mitandao ni unganisho la mitandao miwili ya kompuyta au zaidi tofauti au sehemu za mtandao kwa kutumia teknolojia ya kawaida ya uelekezaji (kwa kutumia ruta). Matokeo yanaitwa muungano wa mitandao (mara nyingi hujulikana kama mtandao). Mitandao miwili au zaidi au sehemu za mtandao huunganishwa kwa kutumia vifaa vinavyo fanya kazi katika tabaka ya 3 (tabaka la 'mtandao' ) ambayo ni kielelezo cha kumbukumbu cha OSI , kama vile ruta. Unganisho lolote kati au baina ya umma, kibinafsi, biashara, viwandani, au mitandao ya kiserikali pia inaweza kuelezewa kama muungano wa mitandao.

Katika mazoezi ya kisasa, mitandao iliyounganishwa hutumia Itifaki za Wavuti. Kuna angalau aina tatu tofauti za muungano wa mitandao,kulingana na wanaoisimamia na ambao wanashiriki katika mitandao hii:

  • wavuti wa ndani
  • wavuti wa nje
  • mtandao

Wavuti za ndani na wavuti za nje zinaweza au zisiweze kuwa na uhusiano na Mtandao. Ikiwa zimeunganishwa na mtandao, wavuti za ndani na wavuti za nje kwa kawaida hupewa ulinzi dhidi ya kutumiwa kutoka kwa wavuti bila ruhusa ifaayo. Mtandao hauchukuliwi kuwa sehemu ya wavuti wa ndani na wavuti wa nje, ingawa inaweza kutumika kama vipengele vya kutumia sehemu za wavuti za nje.

Wavuti wa ndani

hariri

wavuti wa ndani ni kundi la mitandao,inayotumia Itifaki za wavuti na zana za msingi za IP kama vile vivinjari na proglamu za uhamisho wa faili, amabazo zimo chini ya udhibiti wa utawala mmoja. Uti huu wa kiutawala hufunga wavuti wa ndani kwa wote isipokuwa tu kwa, watumiaji maalumu. Kwa kawaida,wavuti wa ndani ni mtandao wa ndani wa shirika. wavuti wa ndani kubwa kawaida angalau utakuwa na seva ya wavuti ili kutoa taarifa za shirika kwa watumiaji.

Wavuti wa nje

hariri

Wavuti wa nje ni mtandao au muugano wa mitandao ambao una upeo mdogo wa shirika moja au kitengo fulani lakini ambao pia una uhusiano mdogo na mtandao moja au mingine, lakini siyo lazima, ya mashirika yanayoaminika au kitengo fulani (mfano, wateja wa kampuni wanaweza kuwa wamepewa uwezo wa kupata baadhi ya wavuti wa ndani ya kampuni hii hivyo kwa njia hii kuunda wavuti wa nje, lakini wakati uo huo wateja wanaweza kutochukuliwa kama 'wanaoaminika' kutoka kwa upande wa usalama). Kitaalam, wavuti wa nje unaweza pia kujumuishwa kama CAN, MAN, WAN, au aina nyingine ya mtandao, ingawa, kwa ufafanuzi, wavuti wa nje hauwezi kuwa na LAN moja; ni lazima angalau uwe na uunganisho na mtandao wa nje.

Wavuti

hariri

Wavuti unahusu unganisho la ulimwengu la mitandao ya kiserikali, kitaaluma, umma, na kibinafsi juu ya teknolojia ya Mkusanyo wa Itifaki za Mtandao. Ni mwandamizi wa Advanced Research Projects Agency Network (ARPANET) iliyotengenezwa na DARPA wa Idara ya Ulinzi ya Marekani. Mtandao pia ni uti wa mgongo wa mawasiliano ya World Wide Web (WWW). 'Internet' kwa kawaida huaandikwa na kutajwa kwa herufi kubwa 'I' kama nomino sahihi, kwa sababu za kihistoria na kuitofautisha na muungano wa mitandao ya aina nyingine.

Washiriki katika mitandao hutumia mbinu mbalimbali za safu ya kumbukumbu za mamia kadhaa, na mara nyingi,itifaki maalum zilizo sambamba na Mkusanyo wa Itifaki wa Mtandao (Internet Protocol Suit) na mfumo wa kutambulisha ( Anwani za IP ) unasimamiwa na Internet Assigned Numbers Authority na regista za anwani. Watoa huduma na mashirika makubwa hubadilishana habari kuhusu upatikanaji wa nafasi ya anwani zao kupitia kwaBorder Gateway Protocol (BGP), na kutengeneza matandao wa njia za upokezi.

Sehemu msingi za tijara ngumu

hariri

Mitandao yote inaundwa kwa msingi matofali ya ujenzi ili kuunganisha kwa vipengelevya mtandao kama vile Kadi za kuunganisha na mtandao (NICs), Madaraja, Habu, Swichi, na Ruta. Aidha, mbinu ya kusaidia kuunganisha vipengele hivi inahitajika, kawaida katika mfumo wa waya wa galvani (kwa kawaida waya wa kundi la 5 ). Njia zisizotumika sana ni pamoja na viungo vya wawimbi madogo (kama katika IEEE 802,12) au waya wa optiki( " nyuzinyuzi za optiki"). Kadi ya Ethernet yaweza pia kuhitajika.

Kadi za kuunganisha mtandao

hariri

Kadi ya mtandao , kibadili mtandao , au NIC (kadi ya kuunganisha mtandao) ni kipande cha tijara ngumu ya kompyuta iliyoundwa ili kuruhusu kompyuta kuwasiliana kwenye mtandao wa kompyuta. Hutoa utumizi halisia wa kiungo cha kati cha mitandao na mara nyingi hutoa ngazi ya chini ya mfumo wa utambulishi kwa kutumia anwani za MAC.

Vipaazi

hariri

Kipaazi ni kifaa cha eletroniki kinachopokea wawimbi na kuyapokeza na nguvu ya ngazi ya juu, au kwa upande mwingine wa kizuizi, ili wawimbi yaweze kufunika umbali mrefu bila ya uharibifu. Katika mipangilio mingi ya Ethernet ya nyaya jozi zilizopindwa, vipaazi vinahitajika kwa waya ambao unatamba zaidi ya mita 100.

Habu ya mtandao ina mashimo mengi. Wakati pakiti inafika kwenye shimo moja,huwa inaigwa kwa mashimo yote bila kubadilishwa kwa ajili ya kupokezwa. Anwani ya inakoenda katika fremu huwa haibadilishwi hadi kuwa anwani ya kutangaza. [4]

Madaraja

hariri

Daraja la mtandaohuunganisha Vijisehemu vya mitandaomingi katika tabaka la kiungo data (tabaka la 2) cha kielelezo cha OSI . Madaraja huwa hayaigi kiholela trafiki yote kwa mashimo yote, kama habu zinavyofanya, lakini husoma ni anwani ipi ya MAcambayo inaweza kufikiwa kwa shimo fulani. Mara baada ya daraja kuhusisha shimo na anwani fulani, litakuwa likituma trafiki kwa anwani hiyo tu kwa hilo shimo. Madaraja huwa yanatuma habari za utangazaji kwa mashimo yote isipokuwa tu kwa shimo ambamo habari zilipokelewa.

Madaraja hujifunza uhusiano wa mashimo na anwani kwa kuchunguza anwani ya mwanzo ya fremu ambazo inaona kwa mashimo mbalimbali. Mara fremu zinapofika kwa kupitia shimo, anwani ya ilipotoka inahifadhiwa na daraja inadhania kwamba anwani hii ya MAC inahusishwa na shimo hili. Mara ya kwanza ambapo anwani shabaha ambayo haikuwa ikijulikana hapo awali inaonekana, daraja litawasilisha fremu hii kwa mashimo yote isipokuwa lile ambalo fremu iliwasili.

Madaraja huwa katika aina tatu:

  1. Madaraja ya kienyeji: Huuunganisha mitandao ya eneo la karibu (LANs) moja kwa moja
  2. Madaraja ya mbali: Hutumiwa kujenga kiungo cha mtandao wa eneo pana (WAN) kati ya LAN nyingi. Madaraja ya mbali, ambapo viungo vya kuunganisha vina kasi ndogo kuliko mitandao ya mwisho, kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakibadilishwa kwa ruta.
  3. Madaraja yasiyotumia nyaya: Hutumika kuunganisha LAN au kuunganisha vituo vya mbali kwenye LAN

Swichi

hariri

Swichi ya mtandao ni kifaa ambacho hupokeza na kuchunga datagramu za tabaka la 2 la OSI (vijisehemu vya mawasiliano ya data) kati ya mashimo (nyaya zilizounganishwa) yenye msingi wa anwani za MAC kwenye pakiti. [5] Hii inaitofautisha kutoka kwa habu kwa vile hupokeza pakiti kwa mashimo yale tu yanayohusika katika mawasiliano kuliko mashimo yote yaliyounganishwa. Kwa kihalisia, swichi haina uwezo wa kuendesha trafiki kwa kutumia misingi ya anwani za IP(tabaka la 3 la OSI )ambalo ni muhimu kwa mawasiliano kati ya vijisehemu vya mtandao au ndani ya LAN kubwa. Baadhi ya swichi zina uwezo wa kuendesha kwa misingi ya anwani za IP lakini bado zinaitwa Swichi kama jina la kisoko. Swichi kwa kawaida huwa na mashimo mengi, kwa nia kuwa mitandao mingi au yote imeunganishwa moja kwa moja kwenye swichi, au kwa swichi ambayo kisha inaunganishwa kwa swichi nyingine. [6]

Swichi ni jina la kisoko ambalo linahusisha ruta na madaraja, na vile vile vifaa vyovyote ambavyo vinaweza kusambaza trafiki inapohitahika au kama maudhui ya mifumo (mfano, kitambulisho cha URL ya wavuti). Swichi zinazaweza kufanya kazi katika tabaka moja au zaidi kwenye kielelezo cha OSI, likiwemo tabaka la kmahali halisia,kiungo data, mtandao, au usari (yaani mwisho-kwa-mwisho). Kifaa kinachofanya kazi wakati huo huo kwenye tabaka zaidi ya moja huitwa swichi la tabaka nyingi.

Kutilia maanani sana kwa ufafanuzi usiofaa wa neno "swichi" mara nyingi hupelekea kuchanganyikiwa wakati wa kwanza wa kujaribu kuelewa mitandao iliyoungaishwa. Wengi wa waundaji wa mitandao wenye uzoefu mkubwa na waendeshi hupendekeza kuanza kwa umantiki wa vifaa vinavyoshughulika na itifaki za ngazi moja tu, si zote ambazo zipo kwenye OSI. Kifaa cha tabaka tofauti ni mada ya juu ambayo inaweza kupelekea uchaguzi wa matumizi fulani, lakini dhana ya swichi za tabaka nyingi tofauti si muundo unaowezekana ulimwenguni.

Ruta ni kifaa cha mtandao ambacho hupokeza pakiti kati ya mitandao kwa kutumia habari iliyopo kwenye vichwa vya itifaki na katika jendwali la upokezi kuamua ruta ifuatayo ya kila pakiti. Ruta hufanya kazi katika Tabaka la Mtandao la kielelezo cha OSina Tabaka la Mtandao la Tabaka la Mtandao la TCP / IP.

Angalia pia

hariri
 
WikiMedia Commons

Marejeo

hariri
  1. Usanifu mpya wa kimataifa wa mtandao wa nyumbani ulio kamilifu, Archived 21 Februari 2009 at the Wayback Machine.Toleo la kitengo cha habari cha ITU-T
  2. [5] ^ Kundi la ufanya kazi wa Ethernet ya IEEE P802.3ba 40Gb / s na 100Gb / s
  3. [6] ^ Unganisho la Mobie Broadband Wireless (Mbwa)
  4. Pountain, Dick (2001), The New Penguin Dictionary of Computing, New York: Penguin Books, ISBN 0-14-051437-6 {{citation}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  5. "Define switch". www.webopedia.com. Iliwekwa mnamo 2008-04-08.
  6. "Basic Components of a Local Area Network (LAN)". NetworkBits.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-12. Iliwekwa mnamo 2008-04-08.

Viungo vya nje

hariri