Mzinga

(Elekezwa kutoka Mizinga)

Kwa maana nyingine tazama: Mzinga (Ilala) na Mzinga (Morogoro).

Mzinga wa kihistoria mwenye muundo wa gobori
Mzinga wa 150 mm wa Kijerumani wa zamani ya Vita Kuu ya Pili (1939-1945)
Mzinga wa 155 mm wa Kifaransa ulioungwa juu ya mwili wa kifaru

Mzinga ni silaha ya moto kubwa au aina ya bunduki kubwa. Kutokana na uzito wake hauwezi kubebwa hivyo inapatikana ikifungwa juu ya magurudumu au magari kama kifaru au pia kwenye manowari.

Mzinga hufanywa sawa na bunduki kwa kasiba na chemba cha ramia. Baruti ya ramia inalipushwa na kuchoma ikitoa gesi moto. Gesi hii inasukuma risasi kwa kufuata mifuo ndani ya kasiba. Risasi inatoka kwa mbio mkubwa mdomomi mwa kasiba na kuelekea lengo lake.

Mizinga ya kwanza zilifanana na gobori; baruti na risasi ziliingizwa mdomoni na baruti kuwashwa kwa kuingiza moto kwa njia ya shimo dogo kwenye tako la kasiba.

Siki hizi chemba cha ramia huwa na msumali inayorushwa mbele kwa nguvu na kusababisha mlipuko ikipiga upande wa ramia unaojaa baruti.

Mizinga hutofautishwa kutokana na unene wa kasiba inayotawala ukubwa wa risasi na nguvu yake.

Kiasi cha baruti kinatawala umbali unaoweza kufikiwa na risasi zake. Mizinga mikubwa zaidi yenye kipenyo cha kasiba cha 150 mm inafikia lengo lenye umbali hadi kilomita 30.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.