Mkataba wa Haki za Kisiasa kwa Wanawake

Mkataba wa Haki za Kisiasa kwa wanawake ulipitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa kikao chake cha 409, tarehe 20 Disemba 1952, na kuidhinishwa rasmi tarehe 31 Machi 1953.

Mkataba wa Haki za Kisiasa kwa wanawake ulipitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa kikao chake cha 409, tarehe 20 Disemba 1952, na kuidhinishwa rasmi tarehe 31 Machi 1953.

Mkataba huo unalenga kuhakikisha haki za msingi za kisiasa za wanawake kimataifa.[1]

Utangulizi

hariri

Baada ya Vita vikuu vya pili, nchi nyingi hazikuwa zinatoa uhuru kamili kwa wanawake kushiriki katika siasa. Mnamo mwaka 1952, mwaka mmoja kabla mkataba huu haujapitishwa, haki ya wanawake ya kupiga kura ilikuwa imetolewa na nchi zisizozidi 100 duniani kote.[1]

Msukumo mkuu wa sheria hii na zaidi rasimu yake ulitoka kwa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia masuala ya wanawake. Tume ilipeleka dodoso juu ya haki za wanawake kisiasa kwa nchi wanachama; ambapo majibu yake yalisadia kuonesha mahali pa kuanzia kwa mkataba huu.

Mkataba huu uliodhinishwa tarehe 31 Machi 1953.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 Cherif, Feryal M. (2015), Myths About Women's Rights: How, Where, and Why Rights Advance, Oxford: Oxford University Press, uk. 271, ISBN 9780190211172
  2. Convention on the Political Rights of Women (PDF), New York: United Nations, 1953
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkataba wa Haki za Kisiasa kwa Wanawake kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.