Asia Ndogo
(Elekezwa kutoka Mkoa wa Asia)
Asia Ndogo ni namna ya kutaja eneo la Anatolia ambalo ni sehemu ya Kiasia ya Uturuki. Ni hasa eneo la rasi kati ya Bahari Nyeusi na Mediteranea.
Asia Ndogo (Kilatini: Asia Minor) ni jina la kihistoria la eneo hili. Wakati mwingine kisiwa cha Kipro kilihesabiwa kama sehemu ya Asia Ndogo.
Jina la Asia lina asili yake hapa. Asia ilikuwa jina la jimbo la Kiroma katika maeneo ya magharibi tu yaliyotazama Ugiriki. Kutoka hapa jina la Asia lilitumiwa pia kwa bara lote lililokaa nyuma yake mahoni pa Waroma wa Kale.
"Asia Ndogo" likawa jina baada ya matumizi ya jina "Asia" kwa bara kubwa kuwa kawaida.