Bahari Nyeusi
Bahari Nyeusi ni bahari ya pembeni ya Mediteranea inayozungukwa na nchi kavu pande zote iliyoko kati ya Ulaya ya Mashariki na Asia ya Magharibi. Imeunganishwa na Bahari ya Mediteranea kwa njia ya Bahari ya Marmara pamoja na milango ya bahari ya Bosporus na Dardaneli. Ina eneo la takriban 424,000 km² na kina hadi 2,244 m.
Nchi zinazopakana ni Uturuki, Bulgaria, Romania, Ukraine, Urusi na Georgia. Rasi ya Krim ni sehemu ya kujitawala ya Ukraine.
Miji muhimu mwambaoni ni: Istanbul, Burgas, Varna, Constanţa, Yalta, Odessa, Sevastopol, Kerch, Novorossiysk, Sochi, Sukhumi, Poti, Batumi, Trabzon, Samsun na Zonguldak.
Jina
haririKatika lugha zote za kisasa bahari inaitwa "bahari nyeusi": Kigiriki Μαύρη θάλασσα, Kibulgaria cherno more (Черно море), Kigeorgia shavi zghva (შავი ზღვა), Kiromania Marea Neagră, Kirusi chyornoye more (Чёрное море), Kituruki Karadeniz, Kiukraine chorne more (Чорне море). Jina hili limepatikana kwa hakika tangu karne ya 13 lakini asili yake haijulikani.
Wagiriki na Waroma wa Kale waliita Euxeinos Pontos (Εὔξεινος Πόντος) au "Bahari ya ukarimu".
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari Nyeusi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |