Anatolia (Kituruki: Anadolu) ni rasi kubwa katika Asia ya Magharibi kati ya Bahari ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Eneo lake ni sehemu kubwa ya Uturuki upande wa Asia.

Ramani ya Uturuki - Anatolia ni nchi kati ya bahari

Jina la Kale ni "Asia Minor" (kilat.) au " Asia Ndogo".

Katika historia mataifa mengi yaliishi Anatolia au kuingia humo na kujenga madola yao kama vile Wahitti, Wagiriki, Wajemi, Waarmenia, Waroma, Wagothi, Wabizanti na Waturuki.