Centro Sur (Kihispania kwa "Kusini-Kati") ni mkoa wa Guinea ya Ikweta. Mji mkuu wake ni Evinayong.

Centro Sur
Mahali paCentro Sur
Mahali paCentro Sur
Nchi Equatorial Guinea
Makao makuu Evinayong
Eneo
 - Jumla 9,931 km²
Idadi ya wakazi (2015[1])
 - Wakazi kwa ujumla 141,903

Mkoa huu ni sehemu ya kanda la Rio Muni lililopo kwenye bara la Afrika.

Centro Sur inapakana na Mkoa wa Estuaire wa Gabon upande wa kusini-magharibi na Mkoa wa Woleu-Ntem upande wa kusini-mashariki, halafu Mkoa wa Kusini wa Kamerun upande wa kaskazini. Ndani ya nchi, inapakana na Kié-Ntem kwenye kaskazini-mashariki, Wele-Nzas kwenye kusini-mashariki, na Litoral upande wa magharibi.

Centro Sur ina miji mitatu kuu: Akurenam, Niefang na Evinayong.

Marejeo hariri

  1. "Censo de población 2015–República de Guinea Ecuatorial" (kwa Kihispania). INEGE. uk. 7. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 October 2017. Iliwekwa mnamo 8 October 2017.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)