Jamhuri ya Kamerun (Kiswahili)
Bendera ya Kamerun Nembo ya Kamerun
(Bendera ya Kamerun) (Nembo ya Kamerun)
Lugha rasmi Kifaransa, Kiingereza
Mji Mkuu Yaounde
Mji Mkubwa Douala
Serikali Jamhuri
Rais Paul Biya
Wazir Mkuu Joseph Dion Ngute
Eneo km² 475,442
Idadi ya wakazi 25,216,267 (2018)
Wakazi kwa km² 39.7
Uchumi nominal Bilioni $38.445
Uchumi kwa kipimo cha umma $1,544
Pesa CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati)
Kaulimbiu "Amani - Kazi - Taifa"
Wimbo wa Taifa Ewe Kamerun, Mwanzo wa mababu wetu
Kamerun katika Afrika
Saa za Eneo UTC +1
Mtandao .cm
Kodi ya Simu +237

Jamhuri ya Kamerun (pia: Cameroon) ni jamhuri ya muungano katika Afrika ya Magharibi.

Imepakana na Nigeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Guinea ya Ikweta na Ghuba ya Guinea.

Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kifaransa (kinachoongoza kwa zaidi ya asilimia 80) na Kiingereza.

Jiografia hariri

 
Mpare kwa mlima Kamerun

Mito hariri

Milima hariri

 
Mlima Kamerun kutoka Tiko, Mkoa wa Kusini-Magharibi

Maeneo kiutawala hariri

Kamerun imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58.

Mikoa ni:


Ona pia: Orodha ya miji ya Kamerun

Historia hariri

Historia ya awali hariri

Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

Wakati wa ukoloni hariri

Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa.

Tangu uhuru hadi leo hariri

Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru. Wananchi wa Kamerun ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kamerun. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kamerun[1]. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun.

Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.[2] Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kamerun (kwa Kifaransa République du Cameroun).

Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao[3]. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kamerun[4], lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha[5].

Siasa hariri

 
Rais wa Kamerun Paul Biya (kulia)
Makala kuu: Siasa za Kamerun

Uchumi hariri

 
Majani chai inayotoka Kamerun
Makala kuu: Uchumi wa Cameroon

Watu hariri

 
Yaoundé, mji mkuu wa Kamerun (2003)
 
Picha, kaskazini mwa Kamerun
 
Ikulu ya sultani wa Bamun kwa Foumban, Mkoa wa Magharibi

Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini.

Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi.

Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.

Utamaduni hariri

 
Nyumba ya Njem
 
Mwanamke wa Maka akienda shamba
 
Familia ya Tikar, Kaskazini magharibi

Elimu hariri

Makala kuu: Elimu Kamerun

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. 1961 British Cameroons Plebiscite, kwenye tovuti ya africanelections.tripod.com/referenda, iliangaliwa Januari 2019
  2. Anglophone crisis: Cameroon must return to federal system abolished under Ahidjo, Abdur Rahman Alfa Shaban kwenye tovuti ya africanews.com tar. 11/03/2018
  3. Ahead of peace talks, a who’s who of Cameroon’s separatist movements, tovuti ya The New Humanitarian tar. 8 July 2020
  4. Cameroon's separatist leader is willing to talk peace, but only with UN backing, Tovuti ya Deutsche Welle ya 23.03.2020
  5. Cameroon Events of 2020, tovuti ya Human Rights Watch, taarifa kuhusu Kamerun mwaka 2021

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Elimu

Uchambuzi

Makabila na koo

Miongozo

Utalii


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kamerun kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.