Mkoa wa Savanes, Togo

Mkoa wa Savanes ni mojawapo ya mikoa mitano ya Togo. Iko kwenye kaskazini ya nchi hiyo. Jina la Savanes linamaanisha Savana yaani eneo pakavu penye manyasi na miti kiasi tu.

Wilaya za Savanes
Mkoa wa Savanes nchini Togo

Mkoa wa Savanes una eneo la kilomita za mraba 8,460. Idadi ya wakazi ilikadiriwa kufikia 1,017,100 kwenye mwaka 2020.[1]

Makao makuu ya mkoa yako mjini Dapaong. Mji mwingine katika mkoa huo ni Mango.

Savanes imegawanywa katika wilaya za Kpendjal, Oti, Tandjouare, na Tone.

Kusini mwa Savanes uko Mkoa wa Kara.

Mipaka mingine ya mkoa huo ni kwa nchi jirani za Ghana (magharibi), Burkina Faso (kaskazini) na Benin (mashariki).

Marejeo

hariri
  1. https://www.citypopulation.de/en/togo/cities/ Togo, Regions; tovuti ya citypopulation.de