Nyasi
Nyasi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyasi
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 12 |
Nyasi ni kundi la mimea inayofunika udongo; nyasi zilizo nyingi si kubwa sana lakini aina kama mianzi hufikia urefu wa miti. Kibiolojia hujumlishwa katika familia ya Poaceae au Gramineae.
Nyasi nyingi huwa na mizizi mirefu inayoshika ganda la juu la ardhi hivyo kuzuia au kupunguza mmomonyoko wa udongo. Kiekolojia aina za nyasi zimezoea mazingira tofauti kabisa kati ya kanda za joto hadi kanda za baridi sana. Wakati wa baridi au ukame majani juu ya ardhi hukauka hata kupotea kabisa lakini mizizi ina uwezo wa kulala muda mrefu na kusubiri mvua au halijoto ya juu zaidi.
Lishe ya wanyama
haririWatu wametumia nyasi kwa shughuli mbalimbali. Nyasi ni muhimu kama lishe ya wanyama kama ng'ombe au kondoo. Wanyamapori wengi wanakula nyasi vilevile. Wakulima wanaweza kuteua aina za nyasi zinazofaa kama lishe ya mifugo na kuzipanda. Kumekuwa sababu mbalimbali toka kwa wanasayansi kuelezea kwa nini binadamu hali nyasi.[1]
Nafaka, viungo na dawa
haririAina kadhaa za nyasi hutoa mbegu zinazoliwa na watu kama nafaka; nyasi hizo za nafaka kama vile mahindi, mpunga au ngano ni kati ya vyakula vya msingi vya binadamu duniani kote. Asilimia 70 ya mimea yote inayopandwa ni nyasi.[2]. Aina nyingine za nyasi hutumika pia kama dawa za aina mbalimbali kwa binadamu na viungo vya chakula au vinywaji kama chai.
Mimea kwa burudani
haririKatika mazingira ya mjini nyasi za pekee hutumiwa kufunika ardhi hasa katika maeneo ya bustani yanayokanyagwa na watu wengi wanapenda kukalia kwenye nyasi na kupumzika; aina hizi zinatumiwa pia kwenye viwanja vya michezo. Katika bustani nyasi hukatwa kwa mitambo maalum kuwa fupi ili kupendezesha bustani, tofauti na nyasi za mashambani au sehemu za kulishia wanyama.[3] Nyasi hutumika pia kufunika ardhi nje ya nyumba ili kuipendezesha.
Ujenzi
haririNyasi hutumika pia kwa ujenzi wa nyumba, mara nyingi maeneo ya vijijini, hasa katika nchi zinazoendelea.
Majina ya aina za nyasi katika Afrika ya Mashariki
hariri- fefe (kuezeka paa, Hyparrhenia rufa - en: thatching grass, Jaragua grass)
- gombakanzu au majani ya Pemba (Stenotaphrum dimidiatum - en: Pemba grass)
- inde (Megathyrsus maximus - en: Guinea grass)
- kichoma-mguu, kichoma-nguo au kishona-nguo (Heteropogon contortus - en: Black Spear Grass)
- kifungambuzi (Eleusine indica - en: Indian goosegrass, Wiregrass)
- kimbugimbugi (Dactyloctenium aegyptium - en: Egyptian crowfood grass)
- lugowi (Cynodon spp. - en: Bermuda grass, African starr grass)
- mabingobingo (Pennisetum purpureum - en: Napier grass, elephant grass)
- malamata (Setaria verticillata - en: Bristly foxtail, love grass)
- mbaya (Rottboellia cochinchinensis - en: Guinea-fowl grass, itch grass)
- mchaichai (Cymbopogon spp. - en: Lemon grass na ingine)
- mkekundu (Chloris gayana - en: Rhodes grass)
- mtimbi au msufi wa bara (Imperata cylindrica - en: Speargrass, swordgrass, lalang grass)
- mwanzi (nusufamilia Bambusoideae - en: Bamboo)
- mzumai (Chrysopogon zizanioides - en: Vetiver, Khuskhus grass)
- sangari (Digitaria abyssinica - en: African couch grass)
- tete (Phragmites australis - en: Common reed)
Nyasi-bahari zinafanana na nyasi za kweli za oda Poales lakini zinaainishwa katika oda Alismatales. Pwani ya Afrika ya Mashariki ina spishi 12 katika jenasi 8.
Marejeo
hariri- ↑ "Kwa nini binadamu hakuli nyasi?
- ↑ George Constable, mhr. (1985). Grasslands and Tundra. Planet Earth. Time Life Books. uk. 19. ISBN 0-8094-4520-4.
- ↑ "mitambo ya kukata majani
Viungo vya nje
hariri- Tasfiri ya nyasi
- Uainishaji wa nyasi
- Nyasi za Pakistani Archived 3 Desemba 2011 at the Wayback Machine.
- Nyasi za Zimbabwe
- Nyasi za Australia Magharibi Archived 1 Aprili 2012 at the Wayback Machine.