Mkongo ni kata ya Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61604.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,543 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,619 [2] walioishi humo.

Wanakijiji wake ni wa kabila la Wandengereko. Koo zipatikanazo ni Mbonde, Mkumba, Rwambo, Msumi, Masimike, Mkukula, Malinda n.k. Pia hujishughuLisha sana na kulima mpunga na mahindi pamoja na uvuvi wa samaki. Lakini pia mtu wa kwanza kuugua UKIMWI katika wilaya ya Rufiji alitokea Mkongo.

Historia

hariri

Kijiji cha Mkongo kilianzishwa mwaka 1961. Kabla ya hapo wanakijiji hao waliishi katika eneo la Lusende kwa sasa hufanywa mashamba ya watu wa Mkongo. Lusende ipo km 4 kutoka Mkongo mjini pia km 4 kutoka Mto Rufiji.

Asili ya jina ni hivi: baada ya uhuru kulianzishwa vijiji vya ujamaa; ndipo watu walitoka Lusende na kuhamia Mkongo ambapo kulikuwa na miti mingi aina ya mikongo, pia kulikuwa na Mkongo mkubwa sana ambao ndio uliobeba jina la kijiji na mpaka sasa huo mti upo katika Barabara ya kuelekea Lusende (mashambani) na hiyo barabara inaitwa Mkongo road.

Hapo mwanzo Mkongo ndio kulikuwa na mji mkubwa katika Wilaya ya Rufiji hata Mwalimu JK Nyerere alifika hapo; alifikia kwa mzee Ally Mamba aliyekuwa mtu wa kwanza kujiunga na Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Rufiji mwaka 1977. Nyerere aliwezesha kujenga Bunge Dogo, Benki, Mahakama ya wilaya, pia kulikuwa na karakana ambayo iliuliwa na kufanywa Shule ya Sekondari iitwayo Mkongo mnamo mwaka 1996. Kuna shule za msingi mbili ambazo ni Mkongo iliyojengwa mwaka 1961 na Kaunda 1976. Mkongo ndipo yalipo makao makuu ya RUBADA (Rufiji Basin Development Authority).

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Pwani - Rufiji DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-18.
  Kata za Wilaya ya Rufiji - Mkoa wa Pwani - Tanzania  

Chemchem | Chumbi | Ikwiriri | Kipugira | Mbwara | Mgomba | Mkongo | Mohoro | Mwaseni | Ngarambe | Ngorongo | Umwe | Utete


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkongo (Rufiji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.