Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 61000.

Barabara ya Pwani
Mkoa wa Pwani katika Tanzania

Mkoa umepakana upande wa Kaskazini na Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro.

Makao makuu ya mkoa yako Kibaha.

Eneo na wakazi

Mkoa huu unalo eneo la km² 32,407, ukiwa na idadi ya wakazi wapatao 2,024,947 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1] kutoka 1,098,668 (2012).

Mkoa huu wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wakwere, Wazaramo, Wandengereko, Wadoe, Wazigua na Wanyagatwa.

Wilaya ya Rufiji imegawanyika sehemu mbili, visiwani na bara: wenyeji wa visiwani ni wa kabila la Wanyagatwa na walio bara ndio Wandengereko. Wenyeji wa visiwani wanajishughulisha sana na uvuvi, kilimo cha mnazi na kupika chumvi, Wandengereko wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi n.k.

Wilaya

 
Wilaya za Mkoa wa Pwani

Mkoa wa Pwani una wilaya nane (katika mabano idadi ya wakazi wakati wa sensa ya mwaka 2022 [2]):

Mkoa huu una jumla ya majimbo ya uchaguzi yanayofikia (9) ambayo yanajumuisha Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kibaha Vijijini, Kibiti, Kisarawe, Mafia, Mkuranga na Rufiji [3]

Utalii

Mkoa huu ni maarufu sana kwa shughuli za kiutalii hususani katika mji wa Bagamoyo.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

Tanbihi

  1. https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. Kuhusu majimbo linganisha Makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016: [http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf

Viungo vya nje