Mlandege (Zanzibar)

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia hapa

Mlandege ni kata ya Jiji la Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Tanzania, ambayo ndiyo makao makuu ya Zanzibar. Kata hiyo imezungukwa na mitaa ya Kwahajitumbo, Michenzani, Mchangani, na Malindi.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 1,861 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 2,213 waishio humo. [2]

Mlandege ni maarufu kwa shughuli za biashara na wengi waliifahamu wakati huo kama ni kitovu cha biashara ya mitumba. Maeneo ya Mlandege yana mchanganyiko wa maduka na makaazi na wengi miongoni mwa watu waishio maeneo hayo ni wafanyabiashara.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz, uk. 245
  2. "Ripoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-03-18. 
  Kata za Wilaya ya Mjini Unguja - Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja - Tanzania  

Amani | Banko | Chumbuni | Gulioni | Jang'ombe | Karakana | Kidongo Chekundu | Kikwajuni Bondeni | Kikwajuni Juu | Kilimahewa Bondeni | Kilimahewa Juu | Kilimani | Kiponda | Kisimamajongoo | Kisiwandui | Kwaalimsha | Kwaalinatu | Kwabintiamrani | Kwahani | Kwamtipura | Kwamtumwajeni | Kwa Wazee | Magomeni | Makadara | Malindi | Mapinduzi | Maruhubi | Masumbani | Matarumbeta | Mboriborini | Mchangani | Meya | Miembeni | Migombani | Mikunguni | Mitiulaya | Mkele | Mkunazini | Mlandege | Mnazimmoja | Mpendae | Muembeshauri | Muembetanga | Muungano | Mwembeladu | MwembeMadema | Mwembemakumbi | Nyerere | Rahaleo | Saateni | Sebleni | Shangani | Shaurimoyo | Sogea | Urusi | Vikokotoni


  Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlandege (Zanzibar) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.