Mlima Mtorwe (pia: Mtove, Mtorwi) ni mlima mrefu katika milima ya kusini mwa Tanzania. Unainuka juu ya uwanja wa Kitulo na kuhesabiwa kuwa sehemu ya Milima ya Kipengere.

Mlima Mtorwe katika nyanda za juu za kusini za Tanzania

Unatajwa kuwa na kimo cha mita 2961 juu ya UB, hivyo ni juu kidogo kuliko Mlima Rungwe (m 2960). Mguuni pa Mtorwe mto Kimani unashuka kupitia maporomoko kwenda Bonde la Usangu[1].

Marejeo

hariri
  1. Graeme Watson: Tanzania's Other Mountains, The Alpine Journal 1995, uk 117 f