Rungwe (mlima)

(Elekezwa kutoka Mlima Rungwe)

Mlima Rungwe ni volkeno iliyozimika ya Tanzania kusini magharibi ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita.

Mlima Rungwe katika Nyanda za Juu za Kusini za Tanzania.
Mlima Rungwe


Ukiwa na kimo cha m 2960 ni mlima mkubwa wa Tanzania ya Kusini.

Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa mm 3,000 kwa mwaka ambao ni wa juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutuba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.

Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

]